Magufuli na Serikali yako hamaki yenu inampandisha chati Lissu

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
22,036
51,751
Kitendo cha kuhamaki, kutishika na kumuogopa Lissu kiasi cha kuamuru vyombo vya habari visirushe habari zake kinazidi kumpa mileage ya umaarufu na ushawishi.

Kitendo hiki:-
1. Kinajenga hamu kwa wananchi kutaka kumsikiliza Lisu.
2. Kinajenga hasira kwa wananchi wengi hata waliomo ccm.
3. Kinawafanya watu waanze kumuonea huruma Lisu na kumchukia Magufuli. Na sasa Magufuli anajianika kwa watanzania kuwa ni mtu mpenda shari, visasi na sifa.

Lisu anazidi kukita mizizi mioyoni mwa watanzania na kuendelea kupendwa zaidi.

My take:
JPM na serikali yake wanajighamba kuwa wamefanya makubwa yanayoonekana. Hofu hii kwa Lissu inatoka wapi?
 
Hakuna aliyehamaki..yeye lissu ndio amehamaki sababu kila anachofanya anaona serikali haina habari nae..

Alipofika alijua ataguswa, akaona wamempotezea.

Akawaambia wenzie wabadilishe wimbo wa taifa akadhani ataguswa akaona kimya.

Akaenda uwanja wa taifa na msafara kinyume cha utaratibu akadhani ataguswa watu wakamuambia ageuze kwa amani.

Sasa amebaki anapayuka tu mara nataka mjadala na magufuli, mara rais wa hovyo hovyo, mara magufuli anasema akipita atajiongezea muda.

Yaani anajichanganyachanganya..tutaona mengi. Ila ajue akijaa watu wanatumbua..mwache aendelee kugalagala.
 
BBC wamepigwa faini kwasabb gani vile? Hebu jibu kwanza swali ndipo tuendelee na mjadala.
Wamekosa weledi na ni aibu kwa shirika kubwa kama hilo kutozwa faini..huwezi kuruhusu hewani habari ya kutuhumu bila kupata mrejesho kwa mtuhumiwa..

Hiyo katika uandishi inaitwa story balancing. Hapo wamesaidiwa kuongezewa skills za uandishi.
 
Ngoja nimsaidie kujibu: BBC wamepigwa fain kwa kurusha matangazo ya mahojiano yao na Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia CHADEMA Ndugu Tundu Antipas Lisu.

Kwa ujibuji huu ndo maana o-level nilipata one
Kama wameonewa waende mahakamani. Hili si ni shirika la kimataifa.
 
Kweli inashangaza sana jinsi serikali inavyomhofia Lissu, manake kuna kitu kikubwa hapa... Pia jinsi wanavyozidi kuzuia habari za Lissu ndio wanawasha moto zaidi. Navyoijua serikali hii itavurunda sana mwaka huu hadi tufike October.
 
Hakuna aliyehamaki..yeye lissu ndio amehamaki sababu kila anachofanya anaona serikali haina habari nae..

Alipofika alijua ataguswa, akaona wamempotezea.

Akawaambia wenzie wabadilishe wimbo wa taifa akadhani ataguswa akaona kimya.

Akaenda uwanja wa taifa na msafara kinyume cha utaratibu akadhani ataguswa watu wakamuambia ageuze kwa amani.

Sasa amebaki anapayuka tu mara nataka mjadala na magufuli, mara rais wa hovyo hovyo, mara magufuli anasema akipita atajiongezea muda.

Yaani anajichanganyachanganya..tutaona mengi. Ila ajue akijaa watu wanatumbua..mwache aendelee kugalagala.
Mkuu zungumzia ili la BBC.
 
Mmefanya mazuri mengi sana,namnadai mnakubalika sasa uoga wa nini wapinzani kusikika? Miaka minne mnasikika peke yenu
 
Hakuna aliyehamaki..yeye lissu ndio amehamaki sababu kila anachofanya anaona serikali haina habari nae..

Alipofika alijua ataguswa, akaona wamempotezea.

Akawaambia wenzie wabadilishe wimbo wa taifa akadhani ataguswa akaona kimya.

Akaenda uwanja wa taifa na msafara kinyume cha utaratibu akadhani ataguswa watu wakamuambia ageuze kwa amani.

Sasa amebaki anapayuka tu mara nataka mjadala na magufuli, mara rais wa hovyo hovyo, mara magufuli anasema akipita atajiongezea muda.

Yaani anajichanganyachanganya..tutaona mengi. Ila ajue akijaa watu wanatumbua..mwache aendelee kugalagala.
Hapo akijaa watu wanatumbua sijaelewa maana yake mkuu sheiza.
 
Kweli inashangaza sana jinsi serikali inavyomhofia Lissu, manake kuna kitu kikubwa hapa... Pia jinsi wanavyozidi kuzuia habari za Lissu ndio wanawasha moto zaidi. Navyoijua serikali hii itavurunda sana mwaka huu hadi tufike October.
Serikali haijazuia habari za lissu ila vyombo vya habari imeona anaongea pumba zaidi..kama ak8jirekrbusha wakati wa kampeni watampa airtime.
 
Wamekosa weledi na ni aibu kwa shirika kubwa kama hilo kutozwa faini..huwezi kuruhusu hewani habari ya kutuhumu bila kupata mrejesho kwa mtuhumiwa..

Hiyo katika uandishi inaitwa story balancing. Hapo wamesaidiwa kuongezewa skills za uandishi.
Kuweka sawa BBC hawajapigwa faini ,wamepigwa star tv kwa kurusha mahojiano hayo ya BBC.
 
Hakuna aliyehamaki..yeye lissu ndio amehamaki sababu kila anachofanya anaona serikali haina habari nae..

Alipofika alijua ataguswa, akaona wamempotezea.

Akawaambia wenzie wabadilishe wimbo wa taifa akadhani ataguswa akaona kimya.

Akaenda uwanja wa taifa na msafara kinyume cha utaratibu akadhani ataguswa watu wakamuambia ageuze kwa amani.

Sasa amebaki anapayuka tu mara nataka mjadala na magufuli, mara rais wa hovyo hovyo, mara magufuli anasema akipita atajiongezea muda.

Yaani anajichanganyachanganya..tutaona mengi. Ila ajue akijaa watu wanatumbua..mwache aendelee kugalagala.
Haina Habari naye au wanamhofia hajarudi kichwakichwa. Na ana exposure yakutosha ughaibuni.
 
Back
Top Bottom