Miradi iliyoachwa na Hayati Magufuli yatesa mafisadi

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Mafisadi wanahaha kila kona jinsi ya kujinasua na hii miradi ya matrilioni iliachwa na Magufuli na ambayo inaonwa na wananchi kama kipimo cha utendaji kazi wa serikali ya sasa. Bila kukamilika kwa hiyo miradi wananchi hawataielewa hiyo serikali.

Mafisadi wanajiuliza wauache vipi mradi wa bwawa la Nyerere ili wakimbilie kwenye gesi?

Mafisadi wanajiuliza wamzuie vipi kandarasi anayechimba bandari ya Dar ili wakimbilie kusaini bandari ya Bagamoyo?

Pia makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lisu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.

Ni miaka sita sasa tangu Tundu Lisu aitabirie Tanzania mabaya ikiwemo kushitakiwa MIGA , ndege kukamatwa, uchumi kufilisika, kunyimwa misaada mbalimbali. Mpaka sasa hakuna hata kitu kimoja kilichotabiriwa na Lisu kilichotimia maaana yake aliwadanaganya watanzania, yani licha ya kusoma kwa kodi za watanzania yeye anakuja kufanya kazi ya kuwadanganya watanzania!

Kinyume na utabiri wa Lisu, Tanzania ya sasa imeingia uchumi wa kati, hatujashitakiwa MIGA na viwanda vya kuchenjua dhahabu vimejengwa Mwanza. Mapato ya madini yamepanda kutoka billioni 100 hadi billion 500, ndege hazikamatwi na watanzania ni wamoja zaidi kinyume na utabiri wake.

Baada ya kuona aibu Tundu Lissu na Lema badala ya kuwaomba msamaha Watanzania wao wamekimbilia Ulaya kwenda kulishwa bure na wazungu.

Lema na Lissu rudini nyumbani muwaombe msamaha Watanzania muanze kuishi kwa jasho lenu kwa kufanya kazi na siyo kulelewa.
 
Back
Top Bottom