Magufuli na CCM Mpasukwa, Lowassa na Matumaini, na Nyota ya CHADEMA

ni hatari kuwa na Taifa lenye watu wenye maono mafupi, wanaongozwa na hisia za watu au kikundi badala ya Taifa, nimuonavyo Magufuli si lolote si chochote na ni kipindi cha kufunua hata yale yaliyojificha. Tutaanza na report ya CAG ya juzi ndipo turudi kwenye mengine na mseme kama kweli mna uwezo wa kumsimamisha Magufuli
 
Kwa mlioangalia TBC leo JK alikua anamtamburisha magufuli kwenye uwanja wa jamhuri mjini dodoma yan hata robo uwanja haijafika watu. Hii sidhani kama ni sign nzuri na ukizingatia wanachama wengi wa ccm wapo mji huo huo.

Sasa mwenye macho haambiwi ona kama kuna watu bado wanabisha ccm haipasuki watasubiri sana
 
Kwa wanao waza kuwa Lowassa anaweza kukihama Chama nadhani huenda hawako sahihi. Lowassa yuko kwenye maisha ya mwisho, anakokwenda ni karibu kuliko alikotoka. Alichonacho mkononi ni kikubwa kuliko kikubwa au kidogo anacho taraji kupata. Vinginevyo somo la hesabu amelipa kisogo.

Amewekeza sana ktk chama, na kama kuna wanaomshauri ahame, nadhani sasa wanatimiza wajibu wao ktk kumsindikiza ktk safari ya kumaliza kisiasa.
 
Jamani watanzania tusisahau mapema sana CCM haibebeki ni kama gunia la misumari.miaka 50 tumewapa wameshindwa je huu ndo watauweza??
 
siamini kama ccm wako pamoja.zile sura za Jana za majonzi ,machozi halafu wanasema wako pamoja huku mbeleni kitanuka tu!

Ni kweli pale hakuna UMOJA mkuu nakwambia lowassa ametulia kama Kobe kumbe anatunga sheria tu na hakika miezi mitatu iliyobakia kabla ya uchaguzi ni mingi sana kwayeye kufanya kitu pale...'am telling you,just spare my words!!!
 
umenena vyema ndugu...chama chochote ndani ya UKAWA hakitakiwi kumpokea lowassa kabisa maana sio tu kuweza kuleta mpasuko bali watachafua UMOJA huo na kukosa uongozi kirahisi kwa kuonekana wanafki wakati tayari hadi saivi tonge lipo mkononi mwao bado kulila tu ivyo wakiruhusu jamaa ajiunge watalidondosha tonge lao.


Mkuu UKAWA wanachotakiwa kwa sasa ni kuzuia goli la MKono kwa kumdhibiti refa na Kamisaa wa Mechi kama watapanga timu yao vizuri mechi hii 75% wamekwisha shinda.

Kauli hii siyo ya bahati mbaya bali hofu kuu na uhalisia ulioko mbele ya safiri hapo Oct.2015


 
Mkuu umetoa wazo jipya lilotupita wengi.
Ajiunge CDM kama mwanachama wa kawaida. That is a possibility, anaweza kuongeza nguvu kwa mgombea wa UKAWA. Akisimama ACT ushindi utakua wa CCM.
Ila mpaka dakika hii sijaelewa ni lini Jk aliamua kumpiga chini EL na kwa sababu zipi? inasemekana alikua hataki hata kupiga naye picha. Ni nini kilivunja mkataba wao kwamba"subiri zamu yangu iishe?"
 
Heko Mzee Mwanakijiji kwa kuelezea uhalisia..

Hata mimi ningekuwa na hasira za kukatwa kimizengwe mizengwe kama ilivotokea kwa Membe na Lowassa...
Nina uhakika wengi wenu humu hasira zenu zingedumu hadi kizazi cha pili...
Watu wanakata tu majina ya wengine bila hata kuwasikiliza....
Wanapiga kura kijinga jinga tu...
Wanahairisha kutangaza matokeo bila sababu za msingi alafu eti Kidumu chama... NO WAY

LAZIMA HICHO KIDUMU KIPASUKE.... EBO!!

mkuu!...naona umenena kihisia zaidi lakini huo ndo ukweli halisi asee na sio wewe au mie tu ila uku mtaani kila mtu ashaelewa mchezo uliochezwa Jana baada ya kura kupigwa tuu alafu wakaambiwa waondoke matokeo kesho kwanini?...kama sio wamepindua matokeo pale ni nini??...namimi na uhakika asilimia zote yule BALOZI.AMINA.S.ALI alishinda na sio maghufuli maana team lowassa wote walimpigia yule Mama ili kumuangusha maghufuli sio kwa ubaya ila ni kumkomoa kikwete na wenzake uzandiki wao walioleta kumkata lowassa bila mashiko yoyote maana anawezaje kupitia January abaki lowassa?...na ndio style hihii waliyotumia team lowassa kummaliza membe na kumwacha JK akiwa hana chaguo lengine zaidi ya maghufuli maana wangempa yule Mama wangeliona anguko lao mwezi October maana kuna makabila hasa ya huku bara kitendo cha kuongozwa tu na mwanamke ni tatizo,pia kwa TANZANIA ilipofikia hii leo sio ya kuongozwa na mwanamke kwa hiyo waliliona hilo na ikabidi wafanye uzandiki wa kumchagua maghufuli ata kama hakumzidi yule Mama kwa kura kabla ya mchezo mchafu kuchezeka....yani chama Kile kimeshindikana michezo michafu hadi ndani kabla ya uchaguzi kitaifa...si hatareee hii??
 
Team Lowasa lilikuwa genge la wapigadebe wasio na msimamo wala falsafa. Hivi ni nani intellectual stalwart aliyekuwa kichwa cha team ile? Rostam? Kingunge? ......

Watu waliochemka mchana kweupe wakati wa utawala wa Kikwete ndo walijazana kwa Lowasa na wengi inaonekana walikuwa wako driven zaidi na chuki dhidi ya kikwete kuliko nia thabiti ya kuleta alternative thinking katka serikali. Intellectually team Lowasa ilikuwa mufilis na migawo ya fedha ndo ilikuwa nguvu yao.

Rostam si mjinga kuwa ataendelea kuwekeza fedha yake kwa losers kama wale. Lowasa licha tu ya kuwa siasa za upinzani haziwezi, hana nguvu ya kimwili na kiakili ya kupambana akiwa peke take. Nguvu yake ulikuwa mtandao ambao umeshayeyuka!

Chama chochote kitakachompokea kinahatari ya kuvaa joho la ufisadi alilovalishwa Lowasa na akashindwa kulivua.
 
Utamuungaje mkono Magufuli ambaye amelelewa, kama alivyosema mwenyewe jana hadharani, na chama cha mapinduzi ambacho ni chama kilichogubikwa na ufisadi, rushwa, wizi, ujangili na ubabe wa kupindisha sheria kwa kiwango cha juu? Kamwe huwezi kumtenganisha aliyelelewa na CCM na tayari ana kashfa chungu nzima za kifisadi na chama kilichomlea.

ataondoa udini ulioletwa na aliyemrithi,,,,,,,,,,,Tb Joshua atamwambia asipotenda haki hataingia mbinguni,,,,,,,,hana makundi ndani ya chama cha majizi,,,,yupo pale kwa bahati mbaya tuu,naunga mkono Magufuli atawale miaka yake kumi,,,,,2025 ndiyo tutaanza kufikiria Ukawa kwani wameshindana kwenye makubaliano japo hawajashinda uchaguzi mkuu,,,,,Mbatia kazi yake ni kutisha wenzake kila siku mara hooo tunajitoa Ukawa Lipumba na vibaraka wake ndiyo kabisaaaa hawaeleweke,,,,,MAGUFULU NITAKUUNGA MKONO LAKINI SIYO CHAMA CHAKO!!!!!!!!!
 
Kwa wanao waza kuwa Lowassa anaweza kukihama Chama nadhani huenda hawako sahihi. Lowassa yuko kwenye maisha ya mwisho, anakokwenda ni karibu kuliko alikotoka. Alichonacho mkononi ni kikubwa kuliko kikubwa au kidogo anacho taraji kupata. Vinginevyo somo la hesabu amelipa kisogo.
7
Amewekeza sana ktk chama, na kama kuna wanaomshauri ahame, nadhani sasa wanatimiza wajibu wao ktk kumsindikiza ktk safari ya kumaliza kisiasa.
Short, precise and clear na imebeba ujumbe mzito na mzur sana. K kudos kwako kk
 
magufuli kaokota embe dodo chini ya mwarobaini..ana kazi kubwa huko mbele pengine akaonekana the worst president ever kama atashinda...nchi ngumu hii na kwa hali ya mwaka huu mbona atapelekekeshwa ninachokiona si jk bali mkapa ndo atakuwa rais kivuli
 
Kwa wale wanaotaka mabadiliko ya kweli CDM na washiriki wake wanatakiwa kujionesha wanaelewa kadi walizonazo mkononi na ni zamu yao kucheza kwani za CCM tumeziona zilivyochezwa na wamebaki na magarasa tu. Ni wakati wa CDM kuita "Last Card".


MMM

MwanaKijiji...
sisi wengine tunao elewa vema DHANA ya maandishi yako hatuna shida na topic zako....haya naweza kusema..

1.Unatamani sana CCM waangushwe..tena saaaana,hata kama ingekuwa ni kwa namna yoyote nje ya Sanduku la KURA
2.Unatambua fika kabisa na kuamini kwamba kwa CCM iliyo moja,ni vigumu kabisa kabisa Upinzani kushinda.
3.Unasahau kwamba CCM ina ma Master-Politicians ana Wazee na kusawazisha mambo hata kwenye dhahama
4.article zako hivi karibuni zimekuwa ni za WISHFUL THINKING,ukijaribu kuwadanganya Wana CCM humu,ukidhani kwamba bado wanachukua suggestions na analysis zako na kufuata kama Ushauri.........

mimi sio mwanachama wa chama chochote....lakini sina noma na CCM,wala sina noma na Chadema

Hivi ni kweli unampenda sana Lowasa na kutamani mafanikio yake,hadi ati ujifanye unamshauri aende ACT?....tunajua wewe ni chadema...kama unampenda na kumtakia mema,kwanini usitake aje chadema?-----facts ni kwamba unatamani sana aondoke CCM ili ccm imeguke...na ukidhania kwamba ikimeguka ati atleast chadema watakuwa na chance(cha ajabu ni kwamba husemi kinaga ubaga kwamba bila ccm kumeguka hatutashinda---na hata upinzani ukishindwa,unajua story utakazoanzisha).

Mimi ninakushauri mwanakijiji uanze kuamini kwamba ndani ya CCM kuna watu wanaojua siasa sana(just assume kama mtu kama mimi nisiye mwanasiasa,ninaelewa nini unachokitaka kwenye meseji zako hizo),sembuse na vile vizee vya ki-mafia ndani ya ccm?

Mimi ninadhani Mwanakijiji utasubiri saaaaana sana kuona ndoto zako zinatimilizika---yaani upinzani kushika dola...nchi yetu bado sana upinzani kupata u rais(ingawaje hili haliwezi kusemwa hadharani nanyi---ndio maana mnatamani hata bomu lianguke wakati viongozi wote wa ccm wapo mkutanoni...hehehe).

Acha hasira Mwanakijiji....

acha kutoa ushauri kwa kuandika kile unachotamani kitokee

ukweli ni huu
1.Lowasa hatoki ccm
2.magufuli ni rais october hii
 
Prophets of doom wa hapa JF mnachosha sasa...
Angalau huyo Magufuli atadhibiti mapato na kutumia mda mwingi kuifikiria utendaji
uwezo wake utakapoishia basi
angalau ni mtu tofauti na approach tofauti

Bossman wewe naona ni closet Magufuli fanboy.

Unaonyesha una matumaini naye sana.

Yeye kuwa mtu tofauti wala si hoja. Hata Mwinyi, Mkapa, na Kikwete walikuwa ni watu tofauti.

Heck, kwanza kila mtu ni mtu tofauti na mwingine.

Tatizo ni chama. He is a product of his environment, CCM. How much different is he really going to be?

Hataunda serikali na watu wa kutoka sayari ya Mushtara huko.

Ataunda serikali na wanachama wenzake wa CCM. Sitashangaa nikiona watu wale wale wa siku zote wakirudi serikalini i.e. baraza la mawaziri.

Binafsi sitegemei jipya kutoka kwake na chama chake.

If you think JK was bad, watch this space.
 
Back
Top Bottom