Magufuli mtake Samwel Sitta aondoke kwenye Jumba la Spika Masaki

Hana unafiki wowote bali alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake ili kulinda kitumbua chake
 
Mkuu linapokuja swala la kuwavunjia/kuwaondoa walala hoi hakuna mjadara ila kwa makada wa chama inaku ni mchakato mreefu.mzee sita ni kauzu sana wasipo mtoa kwa nguvu hataondoka hapo milele

Na ndio maana mpinzani kwao ni adui mkubwa kuliko Al Shabaab. kwa kulinda wizi wao
 
Lakini Tanzania haishi vichekesho vikao vya bunge ni Dodoma ,nyumba ya spika ipo Dar Es Salaam ambako hakuendeshwi vikao vya bunge,kwa hiyo Spika anakaa Dar kufanya kazi Dodoma,kwanini nyumba ya spika isiwe Dodoma na spika akae Dodoma ?,akija Dar aje matembezi tu ya kupunga upepo wa bahari ya Hindi?

Kuna office ndogo za bunge pale posta, Dar es Salaam. Nafikiri hayo nayo ni makazi madogo ya speaker. Watasema tu ukiwauliza hawaishiwi majibu wale.
 
Aslaam Aleykum,

Kama ulivyojinadi kuwa serikali ya Magufuli na sio ya CCM itatatua matatizo ya wananchi naomba uanze na hili la Samwel Sitta kukaa kwenye nyumba ya spika wakati muda wake ulishapita ,sina uhakika ni pesa kiasi gani zimetumika kwa ajili ya makazi ya aliyekuwa Spika wa kipindi kilichopita Anne Makinda wakati nyumba iliyojengwa kwa kodi za wananchi inatumika ndivyo sivyo .

Ifike wakati sasa uanze kutumbua majipu ya chama chako maana huku kushtukiza kwa wakurugenzi wa taasisi mbalimbali kumesha anza kuzoeleka na ndio maana kina Sitta wanapata ujasiri wa kusema umeshauriwa vibaya wakati yeye ni Miongoni mwa waliokuwa mawaziri wa wizara hiyo.

Si ajabu alishauziwa kitambo. Sisi tunabwabwaja tu. Serikali yetu tenaaa...
 
Si ajabu alishauziwa kitambo. Sisi tunabwabwaja tu. Serikali yetu tenaaa...

Kuna uwezekano mkuu walisha muuzia au alipewa kama zawadi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuchakachua maoni ya watanzania kwenye katiba mpya
 
Back
Top Bottom