Magufuli mtake Samwel Sitta aondoke kwenye Jumba la Spika Masaki

UncleBen

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
9,616
12,074
Aslaam Aleykum,

Kama ulivyojinadi kuwa serikali ya Magufuli na sio ya CCM itatatua matatizo ya wananchi naomba uanze na hili la Samwel Sitta kukaa kwenye nyumba ya spika wakati muda wake ulishapita ,sina uhakika ni pesa kiasi gani zimetumika kwa ajili ya makazi ya aliyekuwa Spika wa kipindi kilichopita Anne Makinda wakati nyumba iliyojengwa kwa kodi za wananchi inatumika ndivyo sivyo .

Ifike wakati sasa uanze kutumbua majipu ya chama chako maana huku kushtukiza kwa wakurugenzi wa taasisi mbalimbali kumesha anza kuzoeleka na ndio maana kina Sitta wanapata ujasiri wa kusema umeshauriwa vibaya wakati yeye ni Miongoni mwa waliokuwa mawaziri wa wizara hiyo.
 
hili jambo lmeshajadiliwa humu kitambo!kama bado yuko kwenye NYUMBA Hiyo tatizo siyo lake.
 
Na bado yupo humo? Kwani kule Urambo alijenga ofisi tu ya Spika siyo na makazi pia?

Kuna Porsche Cayenne nyeupe ya mwanae inapaki hapo yenye private number "BS" Ben Sitta Hiyo ofisi ya urambo inabidi ibinafishwe na serikali iwe hata sehemu ya kujifungulia wakina mama wajawazito
 
Samuel ni uadilifu upi ulionao kama hadi leo unaishi nyumba ya spika ? Jitathmini mzee wangu .
 
hili jambo lmeshajadiliwa humu kitambo!kama bado yuko kwenye NYUMBA Hiyo tatizo siyo lake.

Mkuu ni kweli limeshajadiliwa kitambo ila sasa hivi kuna mtumbua majipu ndio tunamsikilizia achana na yule nyoka asiekua na meno
 
Samuel ni uadilifu upi ulionao kama hadi leo unaishi nyumba ya spika ? Jitathmini mzee wangu .

Waadilifu ccm ni Hayati Julius Nyerere na Sokoine wengine mtanisaidia kuwa taja ,kumbukumbu zangu zimeishia kwa hawa wawili
 
huyu mzee hata haya hana.

nakumbuka tangu 2010 hakutoka kwenye hiyo nyumba baada ya kukosa uspika Makinda alikuwa anakaa kwenye nyumba yake binafsi.

alikuwa anakaa humo kwa kigezo cha yeye kuwa waziri nafikiri alijua mke wake atakuwa waziri ndio maana mpaka leo yupo kwenye hiyo nyumba.

Sita toka kwenye hiyo nyumba Ndugai unataka akae wapi?
 
Makinda alikua anakaa kwake Makumbusho kama sikosei lakini vilevile na posho ya nyumba lazima alikua anapewa,anakaa kwa kigezo cha uwaziri kwani hiyo nyumba ni ya mawaziri ? Si angeenda Mikocheni kwenye Zile nyumba za mawaziri kuna viongozi wangapi wa serikali wanaoishi hivyo? Ni mabilioni mangapi ya walahoi wa Tanzania yameishia kwenye matumbo ya viongozi wa aina hii ,Wasira mwenyewe hapa kwake Masaki nyumba anayokaa ni ya shirika gani sijui ,nyumba kama ya nne kutoka kwa Marehemu Jaji Lewis Makame
 
Labda atahama alitegemea jana kwenye zile Wizara 4 zilizobaki angechaguliwa ili aendelee kukaa kama waziri, nafkiri sasa anajuta kumpigia magufuli chapuo siku za kampeni ameisoma namba 6, kama uchaguzi wa T.bara ungerudiwa naamini angeungana na kina Kingunge na Sumaye kumpigia kampeni Lowassa.
 
Kuna Porsche Cayenne nyeupe ya mwanae inapaki hapo yenye private number "BS" Ben Sitta Hiyo ofisi ya urambo inabidi ibinafishwe na serikali iwe hata sehemu ya kujifungulia wakina mama wajawazito
Halafu anajifanya anachukia ufisadi,wazee wengine kweli wana uso wa kauzu
 
huyu mzee hata haya hana.

nakumbuka tangu 2010 hakutoka kwenye hiyo nyumba baada ya kukosa uspika Makinda alikuwa anakaa kwenye nyumba yake binafsi.

alikuwa anakaa humo kwa kigezo cha yeye kuwa waziri nafikiri alijua mke wake atakuwa waziri ndio maana mpaka leo yupo kwenye hiyo nyumba.

Sita toka kwenye hiyo nyumba Ndugai unataka akae wapi?
Lakini Tanzania haishi vichekesho vikao vya bunge ni Dodoma ,nyumba ya spika ipo Dar Es Salaam ambako hakuendeshwi vikao vya bunge,kwa hiyo Spika anakaa Dar kufanya kazi Dodoma,kwanini nyumba ya spika isiwe Dodoma na spika akae Dodoma ?,akija Dar aje matembezi tu ya kupunga upepo wa bahari ya Hindi?
 
Labda atahama alitegemea jana kwenye zile Wizara 4 zilizobaki angechaguliwa ili aendelee kukaa kama waziri, nafkiri sasa anajuta kumpigia magufuli chapuo siku za kampeni ameisoma namba 6, kama uchaguzi wa T.bara ungerudiwa naamini angeungana na kina Kingunge na Sumaye kumpigia kampeni Lowassa.
Kkkk akikusikia atarusha ngumi hewani
Nalog off
 
Maadam imeandikwa humu JF nadhani habari itamfikia yeye mwenyewe na wahusika wengine wa serikali ili huyu mzee ahame upesi iwezekanavyo kwani anaingizia serikali hasara; ilikuwa hivyo hivyo kwa DHAIFU baada ya Magufuli kuapishwa akaendelea kutumia zile gari bullet proof za Ikulu mpaka pale alipokumbushwa kuwa zile gari ni za mpangaji wa magogoni tu na yeye alikuwa sio mpangaji tena na akapewa Toyota V8!!
 
Henry-vs-AIK-Solna-800x428.jpg
 
Back
Top Bottom