Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Ningemshauri Raisi Magufuli kwa kuwa ameonyesha nia ya dhati ya kuinua Uchumi wetu kwa kuongeza uzalishaji amsikilize huyu Mzungu kwenye hiyo video ambaye anamiliki shamba la maua Arusha, ameajiri WatanZania mia nane (800 ) kwa hesabu ya haraka haraka kama kila mwajiriwa anahudumia familia ya watu 4 ina maana WatanZania 3200 wanategema kufanikiwa kwa hili shamba, hivyo msikilize malalamiko yake ikiwezekana muite Ikulu muongee ana kwa ana ili muangalie ni jinsi gani mnaweza kumuondolea vikwazo ambavyo vinapunguza uzalishaji wa maua!
Kwani kulingana na maelezo yake kama vikwazo vikiondolewa au kupunguza ana uwezo wa kuzalisha zaidi na kuajiri Watu wetu wengi zaidi na hiyo ni win win situation kwani itaongeza mapato serikali kwa kuuza kuingiza fedha za kigeni kutokana na export!

Last edited by a moderator: