Hata wewe pia kama mwenzako hauelewi capitalistic economic system inavyofanya kazi!
Ni hivi kipato cha mfanyakazi kinaendana na uzalishaji (productivity) yaani jinsi uzalishashaji unavyoongezeka ndivyo kipato kinavyoongezeka na ndio maana kuna nchi za kipato cha chini, cha kati na juu kabisa, ukienda Uchina hapo mwanzo ilikuwa ni nchi ya kipato cha chini wakapiga kazi bila ya kulala na sasa wamepanda na kuwa kipato cha kati na wanaedelea kupiga kazi kuelekea kipato cha juu!
Ukienda Uchina kuna watu wanalala kwenye mabweni asubuhi wanaamkia kazini jioni wanarudi bweni na hawa wametoka vijijini huko lkn wanafanya tena kwa kipato kidogo sana unajua ni kwanini bado wanafanya kazi kwa kujituma? Ni kwa sababu wanajua ili waweze kupata kipato kikubwa ni lazima kwanza waongeze uzalishaji ili kiwanda kiweze kupata fedha zaidi na hakuna njia nyingine!
Sasa wewe unataka mfanyakazi TanZania alipwe kipato cha juu wakati nchi yetu ni ya kipato cha chini hiyo hela ya kulipa hiyo mishahara mikubwa muwekaji ataitoa wapi? Kumbuka huyu aliyewekeza kama ni kiwanda au sijui Hoteli amekopa fedha kwa ajili ya uwekezaji na ni lazima alipe dani, sasa atalipaje deni kama hakuna Uzalishaji?
Hivyo basi ni lazima kwanza sisi kama WatanZania tukubali kujifunga mkanda tufanye kazi kwa mshahara mdogo na kwa bidii bila ya kuchoka ili tuongeze uzalishaji, uzalishaji ukiongezeka ina maana Kampuni/Kiwanda chetu kitakuwa na fedha ambazo sasa inaweza kumudu kutuongeza mshara pmj na mapato mengine ya serikali pia kuendelea kuajili watu!
Hakuna njia nyingine wote hao unawaona kama ni Ujapani, Ulaya au Marekani wamepita huko, huwezi kudai Mshahara mkubwa kwenye nchi kama TanZania ambayo hakuna kitu kinafanya kazi, huyu muwekezaji inabidi atumie jenereta yake kuzalisha Umeme anunue mafuta ya jenereta, akienda Air port hakuna ndege na wakati mwingine maua yanaharibika kwa maana ni lazima yasafirishwe kwa wakati, hakuna Maji inabidi atafute ya kwake kwa kuwa hakuna hiyo miundo mbinu, madawa ambayo anayatumia kwenye mimea yake kama mbolea, au kuuwa vijidudu ni lazima aagize ktk nje ya nchi kwa maana TanZania hakuna mtu anayetengeneza hizo dawa, kwa kifupi ni lazima aimport kila kitu kuanzia viatu, gloves, mpaka nguo za kazi sasa hizo fedha za kulipa mishahara mkubwa atazitoa wapi?
Usisahau pia TanZania watu skilled hakuna au ni wachache sana mtu anamaliza Chuo hakuna anachojua na inabidi wewe mwenye Kampuni uingie gharama ya kumfundisha hii itakuchukuwa miaka 2-3 ili aweze kufanya kazi independently hii yote ni kwa gharama ya muwekezaji sasa hiyo fedha ya kumlipa mfanyakazi mshahara mkubwa itatoka wapi?
Acha tu kuongea kwa hamaki jaribu kuangalia mambo kwa uhalisia wake nchini kwetu ni ngumu sana kufanya biashara na kufanikiwa vizingiti ni vingi sana, jaribu tu hata kufungua ofisi ya stationary, wiki nzima hauna Umeme inakubidi ili uuze utafute jenereta na kununua mafuta sasa hiyo fedha itatoka wapi? Kumbuka hapo umekopa CRDB au TIB na unatakiwa ulipe deni, halafu hapo hapo mfanyakazi anakudai mshahara mkubwa wakati unapata umeme mara mbili au tatu kwa wiki wewe utatoa wapi fedha ya kumlipa mshahara mkubwa?