Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Hawezi na hataweza hata akishinda. Hizi ni kauli za kuombea kura tu kwani hata yeye alitakiwa awe amejiuzulu kwa kashfa ya meli ya samaki, ripoti ya CAG kuhusu wizara ya ujenzi, uuzaji wa nyumba za serikali na ununuzi wa vivukoko chakavu. Angeanzia hapo tungemwelewa lakini anabaki kuwa sumu ileile kasoro syringe na sindano. Kwanza hao walioafiki mpango huo ni wanafiki tu nao wana tuhuma zao na wamegeuza chama kama kampuni zao binafsi. Asijidanganye kulianzisha kwani ya Kolimba ameyasahau?
 
Kwani kuikarabati nyumba yako mpaka uhame ndiyo uifanyie mabadiliko magufuli utendaji wake ulotukuka anaweza hana woga hana kundi hakuangalii usoni ni mkweli ataleta mabadiliko makubwa ndani ya chama bega kwa bega na wanachama kwa kauli moja hii ni chama cha mapinduzi
Kama unafanya ukarabati mkubwa utaufanyaje bila kuhama.kwa overhaul hii tunayotaka kuifanyia nchi yetu magufuli haiwezi,msitupotezee muda
 
Tunaamini utendaji wako,ushindi umepata wa kishindo

Ushindi wa kishindo nani atampa huyo..eti atafumua fumua..kwanza anawaogopesha hata wapiga kura wake..eti wafanyakazi serikalini mtakiona nikichaguliwa..wakati..haohao ndo wapiga kura watakupa kweli!..unanyenyekea kwanza ukiingia ndo uwanyooshe! Ni sawa na mtoto kakosa unamwambia ole wako nikukute jioni kata na viboko kabisaa!..oooops ataenda kulala kwa jirani ndugu yangu..vitisho kwa muda huu vinawakimbiza wapiga kura!
 
Kwiikwiiikwiiiii mwambieni hatudanganyiki hapa ni luwassaaa tuuuu
 
Kweli CCM ni ileile. Chagua Magufuli na sio CCM.

Magufuli tunaomba ukiingia ikulu anza na katiba mpya ya wananchi ie warioba.
 
Jaman huku mwanza ukikutana na watu 10 9 ni ukawa!!! Vp maeneo mengine uko mlipo makamandaz
 
I like Magufuli's courage... shida ni kwamba akiingia atageuzwa kuwa kama aliyepita

nakumbuka JK aliingia na mkwara, tukakumbushwa kuwahi kazini, kutosumua watu etc.... three years later, JK akawa anafukuzia per diems kuliko madereva wa DFP

Viongozi wetu, hasa wa CCM ni mabingwa wa lip services
 
Mheshimiwa Magufuli
Kwa kauli hiyo na ninavyokufahamu kura yangu chukua hata kabla ya uchaguzi [hapo awali niliamua kwa mara ya kwanza kutopiga kura ya urais] kwani katika mambo yaliyokuwa yananikera moja wapo ni viongozi kuwashika mkono watoto, wake, wajomba, wapenzi n.k kwenye uongozi wa umma bila ya aibu wala soo kama vile nchi hii ni ya kibwanyeye.
 
Jee Ulitaka atafuata nini? Huu ndio wakati wa utafutaji wa kura kwa kila mgombea, Lowassa nae pia ametoa promise nyingi tuu, na ameahidi hatamnyanganya Sumaye shamba alilolipora na ahadi nyingi tuu

Uzuri mmoja lowassa hajasema atawanyang'anya mademu waliogawiwa nyumba na MUUZA NYUMBA.Kwa hiyo it is even.
 
MAGUFULI AWAPA VIGOGO CCM WAKATI MGUMU!

Mgombea wa urais kupitia CCM, DR JOHN POMBE MAGUFULI,KTKA UONGOZI WAKE,

Asema atafumua mfumo wa utendaji ndani ya Chama

Akerwa na vigogo kuwabeba watoto wao katika nafasi za uongozi

Zikiwa ni takribani siku 20 zimepita toka pazia la kampeni za uchaguzi mkuu zianze mgombea urais wa CCM Dkt. John Magufuli akutana na katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kampeni za chama hicho na kumpa mambo anayotaraji kufanyika.

Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu. Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi. Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe, wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

Asema kabla hajaapishwa anataka Chama chake kiandae utaratibu wa kuwabana wabunge wake hususani kupata ripoti za kila mwezi za kila mbunge juu ya utendaji wake kwa wananchi na mchango wake anapokuwa bungeni. Hii itasaidia kuwa na wabunge wanaochapakazi na kuwatumikia wananchi kuliki ilivyo sasa.

Amesema akiingia Oktoba utaratibu wa kuwapa misamaha ya kodi wabunge imewafanya wasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye biashara wakati wanalipwa vizuri na wanapata posho kubwa sasa amesema atafuta misamaha hiyo ili wajikite kuwatumikia wananchi.

Asema atafumua utendaji wa chama kwa kukijengea chama uwezo zaidi kiuchumi ili watendaji wake na jumuiya zake walipwe vizuri na kuondoa michango ya gharama za kura za maoni na hata kuchangia gharama za uchaguzi kwenye majimbo ili kutoa fursa kwa vijana wanaotoka familia maskini kushiriki nafasi ya kuitumikia nchi yao kuanzia nafasi za mtaa, udiwani na ubunge hata urais. Pamoja na kufuta utendaji kazi wa mazoea.

Asema siku 100 za mwanzo zitakuwa za kufanya mageuzi makubwa ndani ya serikali yake na Chama. Asema kama kuna kiongozi aliyeshiriki ufisadi wowote ajiandae maana atakula nao sahani moja ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo chetu cha habari kinasema hata hivyo Kanali Kinana na Philip Mangula wamemuleza kumuunga mkono kwani ni mtazamo mzuri na watampa ushirikiano japo hautawapendeza wengi.

KWELI MAGUFULI NI JEMBE,KATAPILA: HAPA NI KAZI TU.

Thubutuuuu wajinga ndio waliwao×2
 
Hana Ubavu Huo.. Bado Hajajitambua Kuwa Anatembea Amefungwa Kamba Na Ncha Ya Kamba Hiyo Imeshikwa Na Vigogo Wa CCM, Kila Atakapotaka Kwenda Mbele Zaidi, Vigogo Walioshika Hiyo Kamba Wataivuta.. Nae Atalazimika Kurudi Nyuma..

Una akili kaaama redio mbao wewe ndio shujaa wangu wa mwezi huu aisee.
 
Mheshimiwa Magufuli
Kwa kauli hiyo na ninavyokufahamu kura yangu chukua hata kabla ya uchaguzi [hapo awali niliamua kwa mara ya kwanza kutopiga kura ya urais] kwani katika mambo yaliyokuwa yananikera moja wapo ni viongozi kuwashika mkono watoto, wake, wajomba, wapenzi n.k kwenye uongozi wa umma bila ya aibu wala soo kama vile nchi hii ni ya kibwanyeye.
Wewe ni mmoja wa wadanganyika. Unadanganywa na ahadi zisizo na maana. Ccm inawadanganya wasio na misimamo. Pole mdanganyika
 
Back
Top Bottom