Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Wewe ni mmoja wa wadanganyika. Unadanganywa na ahadi zisizo na maana. Ccm inawadanganya wasio na misimamo. Pole mdanganyika
Hii ni nchi huru na kila mja ana haki na kuwa na mawazo, muono nk kadhalika.Kama kwa kumpa pongezi magufuli kwa kauli yake hiyo imekuuma ni bahati mbaya sana.
Ila uelewe wagombea wote hivi sasa wanatoa ahadi tu.Hali halisi ni baada ya uchaguzi na uundwaji wa serikali
 
Huku ndo kuchanganyikiwa sasa...kageuka mpinzani na kubeba ahadi zote za chadema haitoshi leo hii anajaribu kutulaghai atajaribu kufumua uozo wa ccm? Twende na Lowassa 2015

Ni nani wa kumwamini! Anayechukua mazuri ya mpinzani ayatekeleze, au huyu anayeweka kando anayoyamini!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Jee Ulitaka atafuata nini? Huu ndio wakati wa utafutaji wa kura kwa kila mgombea, Lowassa nae pia ametoa promise nyingi tuu, na ameahidi hatamnyanganya Sumaye shamba alilolipora na ahadi nyingi tuu

lowassa kura yangu unayo, hatawaje na lipi sibadiliki..

Kwani kuikarabati nyumba yako mpaka uhame ndiyo uifanyie mabadiliko magufuli utendaji wake ulotukuka anaweza hana woga hana kundi hakuangalii usoni ni mkweli ataleta mabadiliko makubwa ndani ya chama bega kwa bega na wanachama kwa kauli moja hii ni chama cha mapinduzi

Ndugu hayo alitakiwa ayafanye wakati wenzake wanatangaza nia uli wanaccm wampe kura ya kusimama kama mgombea wao. Labda nikuulize ujenzi Wa chama chake ss tusio na vyama unatuhusu nn?
 
Kuondoa Tawala za Koo ndani ya CCM ni sawa na kujipiga risasi kifuani kuokoa pumbu zako. Ni ngumu sana.
e.g Makongoro Nyerere,Vita Kawawa, Riz Kikwete,Malima,Mwinyi,Msuya, Makamba na hivi karibuni Warioba Jr.
sijui itawezekanaje Dr.Pombe Magufuli uweze kuondoa hili la kubeba familia za viongozi ktk nafasi za utawala.
Kwa kuanzia anza na kuteua Mawaziri wasio na Majina ya Kifamilia za Kisiasa.

Ujanja na ujuaji wangu wote nakiri ni bure kwa usanii wa Magufuli. Sikutegemea wala kuamini huyu bwana amefundishwa kwa muda mfupi na kuhitimu kuliko hata mwalimu aliemfundisha huo usanii. Yaani Magufuli na uzee wetu tena miaka mingi tukiwa kwenye chama chako na wewe umeingia na kutukuta huko na tunaouelewa mfumo wao wa uongozi kuliko hata wewe uweze kubadilisha chochote kwenye huo mfumo? Nakuhakikishia hata kuiongoza serikali utakuwa unapewa miongozo na wenye chama na nahisi kwa hilo utakuwa umeshalishwa kiapo na kupewa tahadhari zote. Hayo unayowaaminisha wananchi kuyafanya ungeweza tu kama ungekuwa nje ya mfumo wa ccm. Hayo yanaweza kufanywa tu na chama cha upinzani au mgombea huru kama angeruhusiwa. Vinginevyo ndugu zangu mkisikia Magufuli kashinda uraisi basi msahau katiba iliyopendekezwa na wananchi bali inaenda kupigiwa kura ile iliyoandikwa na bunge la katiba na maendeleo na ukuaji wa uchumi wa taifa hili utaendelea kusimama tena kwa miaka yote kumi.
 
Ni vigezo (vinavyopimika) gani unavitumia kumhukumu Magufuri? Kwa houa hiyo hiyo, ni vigezo gani unatumia kuamini kuwa mamluki wa CCM UKAWA wataleta mabadiliko. Nisaidie ili nitumie kura yangu vizuri.
 
No way usitudanganye ;huwezi mbana baba yako.After all alirudia maneno haya mara nyingi "SITAWAANGUSHA"
 
Isee CCM hakunaga jipya hizo porojo zao zimeanza toka1995 tunawajua hata waseme nini wamweke nani mwaka huu hatdanganyiki, mshawishi aliekuwepo enzi zile ni mwalimu jk Nyerere hawa wengine wote waliobaki ni walafi tu, lazima CCM wakae kando na vyama vingine vifanye waliyoshindwa, kama CCM mna hatimiliki ya nchi hii mwaka huu inavunjwa hata kama ilitoka mbinguni, ata mungu anaaccept kabisa kwa ufirauni mlioufanya kwa waTz kwa zaidi ya miaka 50 nchi mmegawana watu wasiozidi 100, hivi hamna aibu na kumwogopa mungu waTz zaidi ya m45 wanateseka nyie mnakula bata ndani na nje ya Tz hamna isee. Inauma sana.
 
Hatua zozote atakazochukua Magufuli zenye lengo la kuwafanya viongozi wa umma kama wabunge wawajibike kwa wananchi hazitafanikiwa kama hazitakuwa na nguvu ya kisheria/kikatiba. Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba ilitoa mwarubaini wa hili tatizo. CCM wakaikataa! Hivyo hapa tena Magufuli anaifanyia kampeni Ukawa.
 
Ni vigezo (vinavyopimika) gani unavitumia kumhukumu Magufuri? Kwa houa hiyo hiyo, ni vigezo gani unatumia kuamini kuwa mamluki wa CCM UKAWA wataleta mabadiliko. Nisaidie ili nitumie kura yangu vizuri.

Kimsingi Ukawa wanasimamia rasimu ya katiba ya Warioba ambayo inatoa taratibu za kikatiba za kuwawajibisha viongozi.
 
MAGUFULI AWAPA VIGOGO CCM WAKATI MGUMU!

Mgombea wa urais kupitia CCM, DR JOHN POMBE MAGUFULI,KTKA UONGOZI WAKE,

Asema atafumua mfumo wa utendaji ndani ya Chama

Akerwa na vigogo kuwabeba watoto wao katika nafasi za uongozi

Zikiwa ni takribani siku 20 zimepita toka pazia la kampeni za uchaguzi mkuu zianze mgombea urais wa CCM Dkt. John Magufuli akutana na katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kampeni za chama hicho na kumpa mambo anayotaraji kufanyika.

Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu. Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi. Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe, wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

Asema kabla hajaapishwa anataka Chama chake kiandae utaratibu wa kuwabana wabunge wake hususani kupata ripoti za kila mwezi za kila mbunge juu ya utendaji wake kwa wananchi na mchango wake anapokuwa bungeni. Hii itasaidia kuwa na wabunge wanaochapakazi na kuwatumikia wananchi kuliki ilivyo sasa.

Amesema akiingia Oktoba utaratibu wa kuwapa misamaha ya kodi wabunge imewafanya wasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye biashara wakati wanalipwa vizuri na wanapata posho kubwa sasa amesema atafuta misamaha hiyo ili wajikite kuwatumikia wananchi.

Asema atafumua utendaji wa chama kwa kukijengea chama uwezo zaidi kiuchumi ili watendaji wake na jumuiya zake walipwe vizuri na kuondoa michango ya gharama za kura za maoni na hata kuchangia gharama za uchaguzi kwenye majimbo ili kutoa fursa kwa vijana wanaotoka familia maskini kushiriki nafasi ya kuitumikia nchi yao kuanzia nafasi za mtaa, udiwani na ubunge hata urais. Pamoja na kufuta utendaji kazi wa mazoea.

Asema siku 100 za mwanzo zitakuwa za kufanya mageuzi makubwa ndani ya serikali yake na Chama. Asema kama kuna kiongozi aliyeshiriki ufisadi wowote ajiandae maana atakula nao sahani moja ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo chetu cha habari kinasema hata hivyo Kanali Kinana na Philip Mangula wamemuleza kumuunga mkono kwani ni mtazamo mzuri na watampa ushirikiano japo hautawapendeza wengi.

KWELI MAGUFULI NI JEMBE,KATAPILA: HAPA NI KAZI TU.

Asitudanganye .siku 100 za kwanza atarekebisha chama cha ccm akiwa kama Nani kwenye chama.!!?? Wakati kikwete bado ndio mwenyekiti.hii inaonyesha jinsi Magufuli anavyo mwaga ahadi za uongo .
 
Kimsingi Ukawa wanasimamia rasimu ya katiba ya Warioba ambayo inatoa taratibu za kikatiba za kuwawajibisha viongozi.

Wao wenyewe viongozi wa UKAWA wamesigina Katiba zao kwa kumsimamisha mamluki katika siku chache, hao kweli ndiyo niwape kura yangu. HAPANA

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
No way usitudanganye ;huwezi mbana baba yako.After all alirudia maneno haya mara nyingi "SITAWAANGUSHA"

Kuyaelewa maneno ya wanasiasa inabidi uwe na akili ya ziada. Magufuli anaposema "SITAWAANGUSHA" Anamaana kuwa hatatuangusha watanzania katika kuleta maendeleo nchini na kuwashughulikia mafisadi.
 
ahadi zake hutekelezeka kwani amethubut akiwa anawajibka kwa rais, ushind wake wa urais ni mamlaka kamili. hatuitaji uongo usotekelezeka kama kumleta balali, toka tuskie kaul hii balal angekwishaletwa hata kama anakaa umbal wa jua.
 
Kuyaelewa maneno ya wanasiasa inabidi uwe na akili ya ziada. Magufuli anaposema "SITAWAANGUSHA" Anamaana kuwa hatatuangusha watanzania katika kuleta maendeleo nchini na kuwashughulikia mafisadi.
Magufuli alishamaliza kazi Dodoma.Yule ni mtumishi wa CCM hana kipya atafanya CCM wanataka
 
Back
Top Bottom