Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Husomi magazeti mzee na kufuatilia tafiti za uchaguzi?

Tafiti zipi hizo?Tafiti za mara ya mwisho zilionyesha kama uchaguzi ungefanyika mamvi alikuwa anaongoza tokea hapo sijasikia nyingine na aliyekuwa anamfuata karibu ugambani alikuwa pinda sasa hizo nyingine ni zipi??????????????
 
Ni vigezo (vinavyopimika) gani unavitumia kumhukumu Magufuri? Kwa houa hiyo hiyo, ni vigezo gani unatumia kuamini kuwa mamluki wa CCM UKAWA wataleta mabadiliko. Nisaidie ili nitumie kura yangu vizuri.

Madhambi yote unayoyaona yakifanywa na viongozi walioko madarakani na kupigiwa kelele na wananchi yasingewezekana kama sio kulizika kule Zanzibar azimio la Arusha. Baada ya baba wa taifa kungatuka na kuwaachia madaraka viongozi aliofikiri aliwaamini bila kujua walijivisha tu ngozi za mbuzi upesi upesi walikwenda Zanzibar na kulizika Azimio la Arusha huko lililokuwa na misingi mizuri ya namna nzuri ya kuendesha nchi, miiko ya kiongozi n.k. Yote hayo yalifanyika muasisi wake akiwa bado hai. Alipopata taarifa hizo pamoja na kuhuzunika sana aliuliza kwanini hata yale mazuri wasiyachukue? Sasa kuanzia hapo ndio ikawa ruhusa kwa viongozi kuwa na hisa kwenye makampuni, kumiliki mali n.k. Tukaanza kushuhudia ukwapuaji mkubwa wa fedha za wananchi na rasilimali nyingine,uuzwaji wa mashirika ya umma tena kwa bei za kutupwa na nyumba za serikali hadi viongozi kujimilikisha migodi na hazipo hatua za kisheria kama kuwafikisha mahakamani zilizochukuliwa.Yapo mambo mengi yamefanyika na wewe unayajua lakini hatua za kisheria hazichukuliwi.Mambo kama haya ndio yanayoifanya serikali na chama tawala kuchukiwa na wananchi kutokana na mfumo huo wa kuleana,kuogopana,kuoneana haya na kubebana. Hawawezi tena kuwajibishana ile misingi walishaiacha.Wanaogopa kufichuliana siri na zenyewe ni jinsi kila mmoja alivyoiba kivyake na kila mmoja anaelewa mwingine alikoficha alichoiba.Katika utawala wa sheria huwezi kuletewa orodha ya wauza madawa ya kulevya ukaogopa kuwashtaki. Kuwaambia wezi lipa deni pole pole hutapelekwa mahakamani. Anaetoka madarakani ataungana na wastaafu wenzie kumwonya anaeingia asije akafikia kuwashughulikia kwa lolote ovu analolijua juu yao.Akikomaa wanamwacha wanamtafuta atakaekubaliana na matakwa yake na awapitishie chochote watakachokitaka wakati wa uongozi wake. HIYO NDIO HOFU YANGU KWA MAGUFULI SI UTENDAJI WAKE.
 
Si vizuri kujumuisha watu wote kabla ya kuwa na takwimu za kutosha. Mathalani, katika kila awamu ya utawala wa Rais, ni viongozi wangapi (wasio wadilifu, wasio wajibika, wala rushwa, mafisadi, nk) wamewajibishwa kwa njia moja au nyingine (km kuvuliwa madaraka, kushitakiwa, kuhamishwa sehemu za kazi, kutelemshwa madaraka, nk)? Takwimu hizo zitasaidia kumhukumu kila Rais katka awamu yake.

Kati ya mgombea wa CCM na UKAWA bila ushabiki anayeongelea rushwa na ufisadi japo tu jukwaani, kuonyesha ni kero kubwa ya Watz ni nani?

TAFAKARI FANYA UAMUZI ULIO SAHIHI
 
Hatudanganyiki

Umeshadanganyika, ulitaka udanganywe tena na tena, huna akili ya kukuzinduwa kwenye hilo singizi la uzembe. Umedanganywa na viongozi wako kumkubali Yule yule jana waliekuambia ni Baba la mafisadi na leo wanakuambi ni kiongozi Baba wa ukombozi, kidogo wa waneona aibu kukulazimisha kuwakubali marafiki na mafisadi wenzake.
 
Mwandishi wa Makala hii nafikiri ana mahaba sana na mtu binafsi la sivyo anaota. Kwa hiyo Magufuli ni chama cha upinzani ndani ya Chama? Maana sioni hayo yakitekelezwa. Yeye kama mtu binfasi atayafanyaje bila kupitia taasisi za chama ambazo zina hao watu anaotaka kuwashughulikia? Hao anaowatuhumu watoto wao kuingia katika siasa ndiyo wanaompigia kampeni - wakiwemo na hao hao watoto - haiingii akilini leo awaseme na kuwa kesho atawashughulikia! Ya familia yake sitaki kuyasemea maana ni maamuzi yake na inategemea kazingatia nini? Ukiwauliza watu wa kijijini kwao wanaweza kuelezea...
 
Si vizuri kujumuisha watu wote kabla ya kuwa na takwimu za kutosha. Mathalani, katika kila awamu ya utawala wa Rais, ni viongozi wangapi (wasio wadilifu, wasio wajibika, wala rushwa, mafisadi, nk) wamewajibishwa kwa njia moja au nyingine (km kuvuliwa madaraka, kushitakiwa, kuhamishwa sehemu za kazi, kutelemshwa madaraka, nk)? Takwimu hizo zitasaidia kumhukumu kila Rais katka awamu yake.

Kati ya mgombea wa CCM na UKAWA bila ushabiki anayeongelea rushwa na ufisadi japo tu jukwaani, kuonyesha ni kero kubwa ya Watz ni nani?

TAFAKARI FANYA UAMUZI ULIO SAHIHI
Naunga mkono kauli yako ya kwanza ya takwimu, lakini hii ya kuongelea usiwaamini sana wanasiasa. Wanaongea wanachojua unataka kukisikia hata kama hakitekelezeki. Hakuna awamu hata moja katika tawala zetu rushwa, au ufisadi kama inavyojulikana sasa, haiongelewi lakini tujiulize inaongezeka au inapungua? Rushwa ni adui wa haki, sitapokea au kuvhukua rushwa, ilikuwa ahadi yetu uwe mwanachama au siyo mwanachama wa TANU.
 
Si vizuri kujumuisha watu wote kabla ya kuwa na takwimu za kutosha. Mathalani, katika kila awamu ya utawala wa Rais, ni viongozi wangapi (wasio wadilifu, wasio wajibika, wala rushwa, mafisadi, nk) wamewajibishwa kwa njia moja au nyingine (km kuvuliwa madaraka, kushitakiwa, kuhamishwa sehemu za kazi, kutelemshwa madaraka, nk)? Takwimu hizo zitasaidia kumhukumu kila Rais katka awamu yake.

Kati ya mgombea wa CCM na UKAWA bila ushabiki anayeongelea rushwa na ufisadi japo tu jukwaani, kuonyesha ni kero kubwa ya Watz ni nani?

TAFAKARI FANYA UAMUZI ULIO SAHIHI

Nakujibu kwa mara ya mwisho kwani nimegundua kinachokusumbua ni ukada wa chama lakini walio wengi wamenielewa tu.Njia ya kumwajibisha raisi yeyote aliepo madarakani kihalali ni kwa njia ya kura na huwezi kumshusha cheo. Wanaoshushwa vyeo au kuondolewa kwenye nafasi zao ni mawaziri na watumishi wengine na ujue hata m-bunge huwezi kumshusha cheo au kumwondoa madarakani bila kura za wananchi anaowakilisha.Hayo ya majukwaani sina la kukujibu uridhike labda tuwaulize wachangiaji ufisadi,rushwa na uhujumu mali za wananchi upo chama gani watajibu.
 
MAGUFULI AWAPA VIGOGO CCM WAKATI MGUMU!

Mgombea wa urais kupitia CCM, DR JOHN POMBE MAGUFULI,KTKA UONGOZI WAKE,

Asema atafumua mfumo wa utendaji ndani ya Chama

Akerwa na vigogo kuwabeba watoto wao katika nafasi za uongozi

Zikiwa ni takribani siku 20 zimepita toka pazia la kampeni za uchaguzi mkuu zianze mgombea urais wa CCM Dkt. John Magufuli akutana na katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kampeni za chama hicho na kumpa mambo anayotaraji kufanyika.

Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu. Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi.Tueleze atawezaje kufanya hayo mabadiliko ndani ya ccm wakati hana nafasi yoyote ya uongozi katika chama? unasahau kuwa kikwete ataendelea kuwa mwenyekiti wa ccm hadi 2017?
 
Haitakuwa rahisi kuwabana vigogo ki hivyo,aliweza Mwl. tu naye kwasababu zama zile ziliruhusu na si leo.Yetu macho..
 
Umeshadanganyika, ulitaka udanganywe tena na tena, huna akili ya kukuzinduwa kwenye hilo singizi la uzembe. Umedanganywa na viongozi wako kumkubali Yule yule jana waliekuambia ni Baba la mafisadi na leo wanakuambi ni kiongozi Baba wa ukombozi, kidogo wa waneona aibu kukulazimisha kuwakubali marafiki na mafisadi wenzake.
Usipoteze muda kunishawishi wapoteza muda mie ni Lowasa Lowasa Lowasa Lowasa,Sema Lowasaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kwan kipnd chote akiwa wazir hakuliona hilo aache danganya Toto anakumbuka shuka wakati kumepambazuka ? Elly ngoyai ndyo habar ya mjn

Kwani yeye alikuwa na mamlaka kuliko rais?? Magufuli ndo habari ya mjini na vijijini.
 
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia Suluhu Hassan akimsalimia Katibu wa CCM mkoa wa MorgoroRojas Rumuli wakati wa mapokezi yake, alipowasili mkoani Morogoro kufanya mikutano ya kameni katika mkoa huo leo
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mgombea Ubunge Jimbo la Gairo, Sadik Murad wakati alipowasili mkoani Morogoro, kufanya mikutano ya kampeni mkoani humo.
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungua mkono wananchi waliofika kumlaki alipowasili mkoani Morogoro leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Inocen Karogeresi
​
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Gairo A, kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro.
​
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jimbo la Gairo leo.
​
Katibu wa CCM, mkoa wa Morogoro, Rojas Romuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Gairo A katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
​
Mgombea Ubunge jimbo la Gairo Sadik Murad akihutubia wananchi atika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hio mkoani Morogoro
​
Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Gairo A, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogpro
​
Mwananchi akionyesha bango la kumfagilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro

​
 
Back
Top Bottom