Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Magufuli kuwabana vigogo wa CCM

Robethn

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
2,103
Reaction score
354
MAGUFULI AWAPA VIGOGO CCM WAKATI MGUMU!

Mgombea wa urais kupitia CCM, DR JOHN POMBE MAGUFULI,KTKA UONGOZI WAKE,

Asema atafumua mfumo wa utendaji ndani ya Chama

Akerwa na vigogo kuwabeba watoto wao katika nafasi za uongozi

Zikiwa ni takribani siku 20 zimepita toka pazia la kampeni za uchaguzi mkuu zianze mgombea urais wa CCM Dkt. John Magufuli akutana na katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kampeni za chama hicho na kumpa mambo anayotaraji kufanyika.

Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu. Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi. Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe, wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

Asema kabla hajaapishwa anataka Chama chake kiandae utaratibu wa kuwabana wabunge wake hususani kupata ripoti za kila mwezi za kila mbunge juu ya utendaji wake kwa wananchi na mchango wake anapokuwa bungeni. Hii itasaidia kuwa na wabunge wanaochapakazi na kuwatumikia wananchi kuliki ilivyo sasa.

Amesema akiingia Oktoba utaratibu wa kuwapa misamaha ya kodi wabunge imewafanya wasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye biashara wakati wanalipwa vizuri na wanapata posho kubwa sasa amesema atafuta misamaha hiyo ili wajikite kuwatumikia wananchi.

Asema atafumua utendaji wa chama kwa kukijengea chama uwezo zaidi kiuchumi ili watendaji wake na jumuiya zake walipwe vizuri na kuondoa michango ya gharama za kura za maoni na hata kuchangia gharama za uchaguzi kwenye majimbo ili kutoa fursa kwa vijana wanaotoka familia maskini kushiriki nafasi ya kuitumikia nchi yao kuanzia nafasi za mtaa, udiwani na ubunge hata urais. Pamoja na kufuta utendaji kazi wa mazoea.

Asema siku 100 za mwanzo zitakuwa za kufanya mageuzi makubwa ndani ya serikali yake na Chama. Asema kama kuna kiongozi aliyeshiriki ufisadi wowote ajiandae maana atakula nao sahani moja ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo chetu cha habari kinasema hata hivyo Kanali Kinana na Philip Mangula wamemuleza kumuunga mkono kwani ni mtazamo mzuri na watampa ushirikiano japo hautawapendeza wengi.

KWELI MAGUFULI NI JEMBE,KATAPILA: HAPA NI KAZI TU.
 
Dah, I can't wait to opt for magufuri, nimefurahi sana kuwaambia hata make wake aachwe aendelee na chaki make kusema kweli urais siyo wa familia, hatutaki rais wa kusongwa songwa tu na mamluki na watu kibao kana kwamba ni ufalme wa pepo ..Magufuri amenifanya nijisikie raha sana moyoni ..Hapo kazi tu mbwembwe mpe Lowassa
 
Huku ndo kuchanganyikiwa sasa...kageuka mpinzani na kubeba ahadi zote za chadema haitoshi leo hii anajaribu kutulaghai atajaribu kufumua uozo wa ccm? Twende na Lowassa 2015
 
watashindana na hawata.shinda.Hatudanganyiki kirahisi.Go Lowaaasa go.
 
Kuondoa Tawala za Koo ndani ya CCM ni sawa na kujipiga risasi kifuani kuokoa pumbu zako. Ni ngumu sana.
e.g Makongoro Nyerere,Vita Kawawa, Riz Kikwete,Malima,Mwinyi,Msuya, Makamba na hivi karibuni Warioba Jr.
sijui itawezekanaje Dr.Pombe Magufuli uweze kuondoa hili la kubeba familia za viongozi ktk nafasi za utawala.
Kwa kuanzia anza na kuteua Mawaziri wasio na Majina ya Kifamilia za Kisiasa.
 
Mbinu hizi alitumia Kinana ktk ziara zake za mikoani kukiponda chama.Mgombea awe REALISTIC .
 
Tatizo langu atayatekeleza? maana urais ni taasisi na urais si maguful na chama ni mfumo na mfumo sio maguful!
 
Duh, kumbe hata wao wenyewe wanakiri. Hakuna haja ya kumsubiri kuja kufanya. October 25 tutafanya mabadiliko wenyewe kukomesha hayo.
 
Back
Top Bottom