Magufuli: Kuna njama za kumuangusha Nape

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema amepata taarifa kwamba kuna njama zinaandaliwa kwa lengo la kumuangusha mgombea ubunge Jimbo la Mtama kwa tiketi ya chama hicho, Nape Nnauye.

Dk. Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Alisema Nape anaandaliwa njama ili asipite katika kinyang'anyiro cha ubunge jimboni humo kwa sababu aliwataka baadhi ya wana-CCM wajivue gamba wakati chama hicho kikiwa katika mchakato wa kufanya mabadiliko.

Hata hivyo, Dk. Magufuli alisema Nape ni kiongozi mzuri ambaye endapo yeye (Dk. Magufuli), angekuwa na uwezo wa kumhamisha, -angemhamishia kwenda kugombea katika jimbo lake la Chato.

"Nape amekuwa jasiri kuwasema wezi serikalini na ndiyo maana anaandamwa ili wamwangushe…..sasa kwa sababu mimi ndiye nitakuwa rais kwa vyovyote vile, namtaka Nape -ili nifanye naye kazi….wananchi msikubali hila hizo nataka mmlete huyu," alisema Dk. Magufuli.

Aidha, Dk, Magufuli alisema anawapenda wanachama wa vyama vya upinzani wakiwamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa sababu anajua nao wanampenda na watampigia kura kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Alisema matatizo yaliyoko kwenye jamii kama maji na umeme, yanawagusa wananchi wa vyama vyote vya siasa, hivyo aliwaomba waweke pembeni masuala ya vyama na wamchague yeye kuwa rais wa awamu ya tano.

Alisema rais anayehitajika ni yule atakayeleta mabadiliko ya kweli na kwa kasi kubwa na si kwa mbwembwe za kuzungusha zungusha mikono kama wanavyofanya wagombea wa upinzani wanapojinadi.

Chanzo: Nipashe.
 
Nani ahangaike na Nape? Ukawa inajipanga na masuala mapana ya kitaifa. Tunashughulika na fikra za Tanzania ijayo. Maana tutapewa ridhaa na watanzania hapo tar 25-10 ya kuongoza nchi hii.
 
Sio njama ni kauli zake yeye mwenyewe nape ndizo zitakazomuangusha. Unaposema utawazuia wananchi kwa kidole ili wasilete mabadiliko maana yake ni nini wakati hata mgombea wake wa urais anazungumzia mabadiliko hiyo ni dharau kwa wapiga kura.
 
Anaongea sana.
Hapa ndio anatwambia ataleta mabadiliko wakati anayemsifia ndiye kukiharibu chama!
 
EasyFit
Hivi wewe mgombea ubunge wa CCM huko Chato bado hujajiuzuru tu? Mgombea wako wa uraisi angependa Nape awe badala yako!

Ajabu nyingine; raisi anayehitajika si yule mwenye mbwembwe za kuzungusha zungusha mikono ila anayepiga push up na kurusharusha miguu
 
Last edited by a moderator:
Hakuna jimbo ccm watakaloshinda katika mkoa wa lindi, watapata 2 mkoa wa pwani yaani Kibaha na chalinze, na moja la nanyumbu mkoani mtwara licha ya nguvu kubwa ya kampeni wanayotumia CCM hasa mama salma katika ukanda huo wa Pwani.

Mods nimeanzisha mada mbili zote zikimhusu Nape Nnauye na jimbo la Mtama lakini katika hali ya kushangaza mada zote mbili zimeondolewa bila sababu za msingi.Ikiwa kuna mods wameamua kuwa mashabiki wa CCM ni bora wakatujuza tuache kuandika mambo yasiyoipendeza CCM.

Jana Dr Pombe Magufuli kakiri mwenyewe Nape kakaliwa vibaya katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Mtama nategemea MODS watayarejesha mabandiko yangu na kunitaka radhi.

Nakala Paw Invisible

Moderator, JamiiForums, Mhariri
 
Last edited by a moderator:

Hata hivyo, Dk. Magufuli alisema Nape ni kiongozi mzuri ambaye endapo yeye (Dk. Magufuli), angekuwa na uwezo wa kumhamisha, -angemhamishia kwenda kugombea katika jimbo lake la Chato.

Chanzo: Nipashe.
Naomba kujuzwa jamani, hivi mgombea wa Ubunge jimbo la Chato ni nani?
 
Huyu nyau hatakiwi pita kamwe

Mkuu Root nilisema Nape kashindwa kufanya mkutano jimbo la Mtama kwakuwa watu hawamtaki wanasema Nape wa kuja anaitwa Yahaya sawa na mgombea ubunge Moshi Mjini Bwana Davis Mosha.Wakajitokeza watu wa kumtetea lakini pamoja na utetezi wengi walikubali hali si shwari Mtama.

Nape anasomba watu majimbo mengine Mtama hana watu sijui Nape ana hisa JF ghafla bandiko linaondolewa sasa wapingane na Dr Pombe Magufuli.
 
Last edited by a moderator:
Ngongo

Mimi sijamuelewa huyu Magufuri kwamba kumkataa Nape ni njama? sasa nini maana ya uchaguzi? Nape amefungiwa Duniani mpaka mbinguni sasa wanategemea nini? kwani wamejipangaje?
 
Last edited by a moderator:
Mods nimeanzisha mada mbili zote zikimhusu Nape Nnauye na jimbo la Mtama lakini katika hali ya kushangaza mada zote mbili zimeondolewa bila sababu za msingi.Ikiwa kuna mods wameamua kuwa mashabiki wa CCM ni bora wakatujuza tuache kuandika mambo yasiyoipendeza CCM.

Jana Dr Pombe Magufuli kakiri mwenyewe Nape kakaliwa vibaya katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Mtama nategemea MODS watayarejesha mabandiko yangu na kunitaka radhi.

Nakala Paw Invisible

Ukiona hivyo ujue umeleta utumbo.
 
Last edited by a moderator:
Bora angesema kumkataa Lowassa ni njama ningemuelewa lakini Nape msema chochote.

Mimi sijamuelewa huyu Magufuri kwamba kumkataa Nape ni njama? sasa nini maana ya uchaguzi? Nape amefungiwa Duniani mpaka mbinguni sasa wanategemea nini? kwani wamejipangaje?
 
Ampeleke chato basi, lakini Mtama noooo!, halafu apunguze kuongea hovyo , sasa mgombea wa ccm chato akisikia hivyo atajisikiaje?
 
Back
Top Bottom