Magufuli: Kuna njama za kumuangusha Nape

Magufuli: Kuna njama za kumuangusha Nape

Alisema rais anayehitajika ni yule atakayeleta mabadiliko ya kweli na kwa kasi kubwa na si kwa mbwembwe za kuzungusha zungusha mikono kama wanavyofanya wagombea wa upinzani wanapojinadi.
....................................................
Kuna wengine wanapojinadi kwenye mikutano ya kampeni wanapiga pushup.
Tangu lini pushup zikaleta maendeleo?
#CCMHapaZikaTu.
 
Siasa za kitoto sana CCM kwa heri, wanasera nyepesi na mambo kuona watu wote ni wajinga. CCM hoi taabani
 
Nyie ongeeni,sisi vitendo tu ndipo mtakapojua kelele zenu ni bure,magufuli awe mshindi
 
Sasa hizo njama za kumuangusha huyo nepi zinafanywa na nani?
Kama si wenyewe hao hao?
 
Mods nimeanzisha mada mbili zote zikimhusu Nape Nnauye na jimbo la Mtama lakini katika hali ya kushangaza mada zote mbili zimeondolewa bila sababu za msingi.Ikiwa kuna mods wameamua kuwa mashabiki wa CCM ni bora wakatujuza tuache kuandika mambo yasiyoipendeza CCM.

Jana Dr Pombe Magufuli kakiri mwenyewe Nape kakaliwa vibaya katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Mtama nategemea MODS watayarejesha mabandiko yangu na kunitaka radhi.

Nakala Paw Invisible
Pole sana mkuu jf ya sasa hivi ukiishika pabaya ccm lazima ukatwe.
 
Samahani sana kwa kutoa hii

Tambua katika maisha kujua mbinu za wizi na husikamatwe ni ujuzi na elimu lakini kujua namna ya kuzuia wizi ni ujuzi na elimu zaidi.

Hapa chini nawaletea ‘kuntu’ wizi wa kura unavyofanyika na namna ya kuuuzuia.(Utaratibu huu unatumiwa na nchi mbalimbali duniani

Zipo mbinu nyingi lakini leo nitaongelea mbinu moja nay a kipekee inayotegemewa kw asilimia 85 maana nyingine ni pata potea.

Vituo hewa vya kupigia kura.
Hivi vipo tayari katika orodha ya vituo vya kupigia kura na vina wapiga kura hewa,hata vyama nje ya kile chama chetu hawajui huu mchezo utakavyochezwa.

Kosa kubwa hapa wafuasi wa vyama wao wanaongelea suala la kulinda kura,hilo halisaidii kuzuia hii mbinu.

Kinachofanyika.
Kwa mfano kata moja ya Mwanakuja katika jimbo la Kyelwa kuna vituo 8 kati ya hivyo nane vituo 4 ni hewa vya Maganzo,Twila,Kulele na Mutwi katika jimbo la Kyelwa,Vyama vitajikita katika kuweka mawakala katika vituo 4 halali bila kujua kuwa kuna vituo vingine 4 hewa.

Hivyo vituo hewa vimepewa wasimamizi hewa,walinzi hewa,mawakala hewa nk,vitapigiwa kura ofisini na kuandika matokeo ya hivyo vituo na kutoa takwimu za wagombea wote kulingana na walivyogombea lakini hapa mlengwa ni wa chama Fulani.

Wakati wasimamizi ‘HALISI’ wakirejesha matokeo ya takwimu kutoka vituo vyao kwa mkurugenzi tayari watakuta na wasimamizi ‘FEKI’ wamekwisha ejesha takwimu kutoka vituo FEKI.Mkurugenzi atajumlisha.Kabla ya kupiga kura mgombea X atakuwa na kura 0 huku Y akiwa na kura 2,000 katika kata.

Kazi hii ya kupigisha kura hizi bandia itaanza kufanyika October 22-24.kabla ya kupiga kura October 25.

Namna ya kudhibiti huu Wizi.
Wawakilishi wa vyama ni kupata IDADI halisi ya vituo katika kata na kuvitambua vyote kwa majina,wakipewa orodha husika iwe imesainiwa na mkurugenzi kuwa hivyo ndo vituo halali.

Utaratibu ukibadilika nitawajuza

Share mpaka iwafikie mawakala wa Ukawa: Viongozi wa Ukawa: Nec na mafisisiem
 
Mnaosema Magufuli atabadilisha system mmemsikia anamuomba Nape afanye naye kazi!Kwa hiyo ndio Mawaziri wake hawa dah
 
Hivi wewe mgombea ubunge wa ccm huko Chato bado hujajiuzuru tu?!! Mgombea wako wa uraisi angependa Nape awe badala yako!

Ajabu nyingine; raisi anayehitajika si yule mwenye mbwembwe za kuzungusha zungusha mikono ila anayepiga push up na kurusharusha miguu
Magufuli amechanganyikiwa kabisa kabisa...........Anatia huruma, hajui anachoongea wala kufanya wala hajui hadhari za maneno yake na matendo yake.
 
EasyFit
Anamaanisha kwamba hao walioshindwa kuyatatua walikuwa wanayashughulikia kwa mtindo wa visasi vya kipolitike?
 
Last edited by a moderator:
Anamaanisha nini anaposema atakuwa Rais kwa vyovyote vile??

Hawa watu waangalie sana kauli zao....nchi yetu na amani yake ni muhimu sana kuliko chochote...
 
Wana bodi. Nape Nnauye hali ni mbaya jimboni anakogombea ubunge. Hakujua kwamba atakutana na upinzani mkali namna hii. Na mbaya zaidi ameanza kutafuta visingizio vya kushindwa! Amamwambia Magufuli eti ''kuna njama za kumwangusha zinafanywa''. Na Magufuli katika kuonyesha kukata tamaa akasema ''angekuwa na uwezo angemhamishia jimboni kwake, Chato akagombee huko'' Jisomee mwenyewe:
 
Wana bodi. Nape Nnauye hali ni mbaya jimboni anakogombea ubunge. Hakujua kwamba atakutana na upinzani mkali namna hii. Na mbaya zaidi ameanza kutafuta visingizio vya kushindwa! Amamwambia Magufuli eti ''kuna njama za kumwangusha zinafanywa''. Na Magufuli katika kuonyesha kukata tamaa akasema ''angekuwa na uwezo angemhamishia jimboni kwake, Chato akagombee huko'' Jisomee mwenyewe:


Home
Siyo nepi tu huku mtaani watu wanahasira kama vile mtu aliye mfumania mke wake ccm ipo kwenye hali mbaya!
 
Magufuli hizo haziitwi njama bali ni kampeni za uchaguzi ya kila mmoja kumpigia kampeni yule anayemfaa na wala si dhambi.
 
Ampeleke chato basi, lakini Mtama noooo!, halafu apunguze kuongea hovyo , sasa mgombea wa ccm chato akisikia hivyo atajisikiaje? Yaani Nape mwenye kinywa kichafu ni bora kuliko yeye??

Kweli nimeamini ccm ni ile ile. Yaani hata wangetokezea Magofuli 10 kutoka ccm hakuna Mabadiliko. Yaani ccm ukijua kutukana matusi ndo unaheshimika kabisa. Kumbe Benjamini hajayatoa kwingine ni ndani ya ccm. Sasa Nape na mitusi yoote bado anaambiwa Mungu alikosea kumzalia huko kusini bali alitakiwa azaliwe Chato kwani kule hakuna Mwanamume mwingine aliyebakia baada ya Magofuli kuondoka na kuugombea urais.
Mengine yasikie tuu. Jimbo zima la Chato hakuna kidume mpaka anatamani awapelekee nyape ndio anawafaa. Sasa wana chato yasikieni maneno na kejeli za mwanenu JPM. Tukisema huwa anatembea na dawa mfukoni kina Lizaboni wanatukana, tukisema alienda kunywa kikombe cha babu Loliondo kupunguza upunguani mnasema tunakebehi. Haya sasa jioneeni wenyewe
 
Magufuli safari hii angegombea chato angepigwa chini. Sio kiongozi ila ni mtz mkurupukaji maarufu
 
Ampeleke chato basi, lakini Mtama noooo!, halafu apunguze kuongea hovyo , sasa mgombea wa ccm chato akisikia hivyo atajisikiaje? Yaani Nape mwenye kinywa kichafu ni bora kuliko yeye??

Hujajua kuwa jamaa betri imeover shoot kwa hiyo anasema hovyo tuu? Kaulize Vunjo, yule mgombea wake aliyesema alitaka kupewa milioni 250 akamtosa baada ya kumuona Mrema. Ili ashangiliwe ikabidi aseme mchagueni Mrema.
Jamaa siku hizi ana ropoka kama kabugia viroba.
 
Back
Top Bottom