mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 12,294
- 9,233
Kwa
Kwa kawaida Tanzania haina Wasomali,ila hawa wamehamia miaka mingi ,hawa ni Watanzania,pia kuna mabrush(Baluch)pale Rujewa/Mbalali wapo hapo vizazi na vizazi ni watanzania hawa,kwa hiyo tuache kushangaa sana juu ya Mungai.Babu yake ndio alikuwa Mkenya lakini baba yake na yeye na watoto zake ni Watanzania.Kwa wale wanaofatilia historia mtakumbuka kuwa kuna wakati miaka ya ya 1960 mwanzoni, Rais wa kwanza Tanganyika na Rais wa kwanza Kenya walikubaliana kuruhusu baadhi ya raia kutoka kenya hasa kabila la wakikuyu kuhamia Tanganyika kwenye baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro, Iringa na Rukwa. Rais wa Kenya aliomba wakikuyu waje huku kwakuwa walikuwa na shida kubwa ya ardhi. Kuna baadhi ya maeneo hayo mpaka leo ukienda unakuta wakikuyu wengi tu wanafuata mpaka mila za kikuyu. Kwa mfano ukienda Rukwa wilaya ya nkasi kijiji cha kipande kuna wakikuyu ambao wapo mpaka leo wapo. Hata Sumbawanga mjini wapo wakikuyu wengi tu wanafanya biashara.
Kwa wale wenye kumbukumbu utakumbuka kuwa timu ya Young Africans walikuwa na golikipa maarufu alikuwa anaitwa Patrick Nyaga. Wengi tulifahamu kuwa alitoka Morogoro , lakini wazazi wake walikuwa wakikuyu waliohamia wakati huo. Hata jina Nyaga ni la kikuyu. Kwa upande wa Iringa ndio akina Mungai.
Hili sio jambo geni katika ulimwengu huu. Kuna nchi nyingi amabazo wanapokea wageni wahamiaji kwa makubaliano na wakapata uraia. Hata leo hii kuna wakimbizi wakisomali na warundi ambao wanahamia na kupatiwa uraia wa Tanzania.