Naomba kupinga hoja kwamba labda hana washauri wazuri. Sifa ya kwanza aliyonayo na inayomuangusha ni kwamba haamini katika ushauri wa wengine. Yeye kama alivyokuwa Idi Amini wanaamini kuwa wana akili, uwezo na uzalendo kuliko yeyote duniani. Pia pamoja na usadism aliokuwa nao , lakini kaudikteta kake kanalazimisha wote wanaomzunguka wamuambie maneno anayopenda kusikia. Sahau kuhusu ushauriKwakweli alianza vizuri sana ukitilia maanani kwamba uadilifu ndio karata iliyomuibua kutoka kusikojulikana
Ila nadhani kuna watu wanamshauri vibaya kwamba anaweza tatua matatizo ya wananchi kutumia shortcuts za maneno ya kisiasa badala ya kuyatatua matatizo kama yalivyo
Kuna uwezekano vile vile hali ya kutoaminiana (wenye mikia na waliokatwa)na makundi ktk chama kumemfanya sasa ajenge usuhuba na watu ASIOFANANA NAO
Mengi yanakuja
Lipi ni jema,kuonekana huko nnje kuwa hafai au kufaa ndani kwa Watanzania?Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
Hao wanaomuhitaji magufuri waambie tuwaazime japo mwezi mmoja waonje umaskini na kutafuta mlo wa siku mojaMwanzoni Rais wetu alipendwa sana na mpaka baadhi ya nchi zikatamani kumuazima akatawale kule kwa siku kadhaa au miezi kadhaa, hii ilileta picha kwamba ama Magufuli alikuwa anafanya vema mwanzoni au aliazna na vipaumbele ambavyo ni matataizo sugu ya nchi nyingi duniani mfano rushwa na uwajibikaji,
Tuwe wakweli Mpaka wapinzani wa hapo Tanzania akina mbowe na Lipumba walisema kwamba Magufuli anatekeleza ilani yao hafanyi ya kwake,
Zitto kabwe akafika hatua akasema sasa nchi ina rais kwa kweli,
Pale Kenya na nchi baadhi zilizoedesha uchaguzi baada ya Magufuli kuingia madarakani walitamani hata wale wanaenda kuwachagua wawe katika viatu vya Magufuli,
Pro Lumumba mpaka akaanzisha neno maarufu la Magufulification of Africa
Pale Autralia na Madagascar ilikuwa maandamano yakitaja kwamba tunataka kuwa na kiongozi kama Magufuli,
Ulaya walisema kuna kanchi kameibuka huko afrika kana Rais anaitwa Magufuli,
Magufuli Magufuli Magufuli aal over the world then
Je kuna jinsi alitafsiriwa vibaya mwanzoni baadae wakagundua kwamba siyo, au labda ameyafanya mazuri wakayazoea ikaonekana jambo la kawaida?
Au bado anakubalika kwa wale mnaotembea tembea huko?
BADO DUNIA INAMUONA MAGUFULI KAMA MWANZO? KAMA SIYO UNAHISI NINI KIMESHUSHA UMAARUFU HUO? NA JE ANGEFANYA NINI ILI ANEDLEEE KUAMINIKA KWA KILA MTU?
Usiwe mvivu wa kufanya utafiti wako. Ingia katika youtube channel ya Dr Mumbi Saraki kwa kuanzia tu kasome comments za watu.Leta ushahidi!
Wengi walisema hivyo hivyo kama wewe wakati Prime Minister Zedawi sasa angalia nchi yake inavyokwenda kwa kasi. Uhuru wa kujieleza wa matusi kama Mange mliyekua mnamshangilia ama wa kumtukana ndiyo demokrasia? Mnaiga wamatekani wale wenzetu wana miaka zaidi ya 300 kufika pale walipo. Mila na desturi tofauti Ulaya unaweza kumuita baba yako kwa jina lake na kumuita muongo ikawa sawa lakini hapa kwetu hiyo inaitwa ni utovu wa adabu.Mwanzoni na Mimi nilikuwa naye,in fact bado ana nafasi ya kuwa role model hasa kama ataruhusu Uhuru wa kujieleza na democracy kwa ujuma. Kiongozi lazima awe na ngozi ngumu,lazima akubali kukisolewa. Pale sasa ndiyo tutampa big up.
Ha ha haaa...Acha Ushabiki wa ajabu, nchi gani imtamani Magufuli hapa Duniani? Yaani waache kuwatamani viongozi reasonable wamtamani huyo?
Labda alitamaniwa na Alshabab au Boko Haram
Mwanzoni Rais wetu alipendwa sana na mpaka baadhi ya nchi zikatamani kumuazima akatawale kule kwa siku kadhaa au miezi kadhaa, hii ilileta picha kwamba ama Magufuli alikuwa anafanya vema mwanzoni au aliazna na vipaumbele ambavyo ni matataizo sugu ya nchi nyingi duniani mfano rushwa na uwajibikaji,
Tuwe wakweli Mpaka wapinzani wa hapo Tanzania akina mbowe na Lipumba walisema kwamba Magufuli anatekeleza ilani yao hafanyi ya kwake,
Zitto kabwe akafika hatua akasema sasa nchi ina rais kwa kweli,
Pale Kenya na nchi baadhi zilizoedesha uchaguzi baada ya Magufuli kuingia madarakani walitamani hata wale wanaenda kuwachagua wawe katika viatu vya Magufuli,
Pro Lumumba mpaka akaanzisha neno maarufu la Magufulification of Africa
Pale Autralia na Madagascar ilikuwa maandamano yakitaja kwamba tunataka kuwa na kiongozi kama Magufuli,
Ulaya walisema kuna kanchi kameibuka huko afrika kana Rais anaitwa Magufuli,
Magufuli Magufuli Magufuli aal over the world then
Je kuna jinsi alitafsiriwa vibaya mwanzoni baadae wakagundua kwamba siyo, au labda ameyafanya mazuri wakayazoea ikaonekana jambo la kawaida?
Au bado anakubalika kwa wale mnaotembea tembea huko?
BADO DUNIA INAMUONA MAGUFULI KAMA MWANZO? KAMA SIYO UNAHISI NINI KIMESHUSHA UMAARUFU HUO? NA JE ANGEFANYA NINI ILI ANEDLEEE KUAMINIKA KWA KILA MTU?
Shida ya wenzetu hao maslahi yao kwanzaAfrika bado wanamuona kama Mwanzo ila Ulaya na Marekani wanamuona mbaya kwani kawakazia.
unachekesha..hivi ni nani mfano wa kuigwa basi hapa.Tanzania ..kwa demokrasia..kwa sabab hata chama chenyewe kinachojiita cha demokrasia hakina demokrasia hata hiyo zero huipati..utapata demokrasia negative..Kwenye demokrasia JPM ni ziro
Lipi ni jema,kuonekana huko nnje kuwa hafai au kufaa ndani kwa Watanzania?
P, ni kweli anabaki kuwa yeye kwani hakuna mwingine kwa wajihi na tabia zake Bali yeye!Kuna watu walidhani ni nguvu ya soda, hii ngoma iko vile vile hadi 2025, Magufuli ni yule yule juzi, jana, leo na hata...
Mimi nimeshauri hivi
PKwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Wanabodi. Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?. Kwa maoni yangu, uchaguzi wa...www.jamiiforums.com
Hao tulikataa masharti yao ya ushoga na usagaji. Wengi Sasa wametuelewa na pia hatutembezi bakuli. Pesa ziko hapa hapa kwetu. Tunataka ushirikiano wa usawa siyo wa ubwana na utwana.Huko ulaya wala huitaji kufika si wanatoa taarifa zao tunasoma, Danmark na USA wamekata misaada sababu Magufuli ni Rais bora kabisa kabisa.
hao wengi ni akina nani kama si mm na ww tuliomo humu twitter, IG na kwingine... ndiyo hawahawa waTZ, usidanganyike ni aghalabu kukuta kijana wa sasa hatumii mitandao ya kijamii....Ukiskiliza maneno ya mtandaoni unaweza kudhan watu wanamchukia Magufuli ila kumbe wananchi wanamkubali balaa.
Bahati mbaya wapiga kura wengi hawana muda wala account jamiiforums ila wanamkubali JPM.
Muwe na wakati mwema.
Kama hataki kukosolewa kama ulivyosema basi ni kiongozi mbaya sana kuwahi kutokea. Hawezi kuwa kiongozi mzuri kama hataki kukosolewa. Hii kwamba ni kiongozi mzuri kulinganisha na waliomtangulia mara nyingi hujengwa na fikra za udini na ukanda na ukabila tu uliojificha kwa ndani mbali sana huko.Binafsi naamini Magufuli ni kiongozi mzuri sana tu ukilinganisha na waliomtangulia kuanzia Mwinyi
Tatizo lake kubwa ni kutotaka kukosolewa kunakopelekea ubabe na uonevu kwa wanaomkosoa
Angerekebisha hapo naamini angekuwa vizuri zaidi