.
Misrepresentation and the fallacy of equivocation at work in terms of red text. Rais hakusema maneno hayo. Read my original thread again.
Wewe ndiye unayefanya misrepresentation ya mambo
1. Rais amezungumzia 'marufuku' si katika mkutano mmoja.
Tueleze,ulimwelewa kwa kauli alizotoa katika mkutano gani kati ya aliyozungumzia.
2. Tukichukulia hoja ya hotuba ya viwanja vya Biafra ndiyo 'base' ya argument yako, bado hujamkariri vema. Alichosema ni kuwa '..uchaguzi umekwisha anataka kutekeleza aliyoahidi kwa wananchi. Kwamba, madiwani na wabunge waende wakazungumze kwa bidii katika maeneo yao'
Hapo alimaanisha hoja za kisiasa zipelekwe bungeni au kwa baraza la madiwani.
Kwa mtazamo wa baadhi, ni ujumbe makundi hayo yasifanye siasa nje ya maeneo yao
Hili ni baada ya wabunge wa upinzani kutaka mikutano kueleza nini kinaendelea bungeni.
Ikiwa ni hivyo, kuna ukiukwaji wa katiba na sheria za msajili wa vyama zinazotoa fursa kwa mtu kushiriki shughuli za kisiasa kwa kufuata taratibu zilizoanishwa
Pia kuna tatizo, wananchi wa kawaida wanaachwa nje ya mfumo wa kisiasa,unaogusa maisha yao kila dakika, saa na siku. Ukimsikiliza, aliomba jeshi la Polisi lisadie kazi hiyo
Kumbuka, ni jeshi la Polisi lililozuia mikutano bila sababu za maana kabla ya hapo.
Si kazi ya jeshi la Polisi kusimamia kipindu pindu, au magonjwa yasiyojulikana.
Jeshi la Polisi lina enforce sheria zilizopo na halipaswi ''kutunga sheria''
Kauli za magonjwa zinatolewa na wizara au idara husika na kuwa enforced na jeshi
Ikiwa afisa Afya, Daktari wa manispaa, mkoa au wizara hawajapiga marufuku mikusanyiko, jeshi la Polisi linapata nguvu kutoka wapi ku enforce kisichokuwepo?
Lini mazishi yamekuwa tukio la kisiasa hata kama linagusa wanasiasa?
Kwanini Mazishi ya Mwanza yalikuwa na matatizo, juzi kada wa CCM Arusha amezikwa kwa mkusanyiko kama ule wa Mwanza?
Na kama tukisema 'any form' ya mikutano, tuna maana hakuna shughuli za kisiasa.
Ikiwa ni hivyo, hii violation of human right kwa mujibu wa katiba ya nchi inapaswa kugusa jamii nzima na si sehemu ya jamii au makundi fulani
Ni vipi mahafali yenye hadhi za kipa imara,ndoa au harusi limekuwa tukio la kisiasa?
Na tukio la mahafali linakiuka sheria gani ya nchi kiasi cha jeshi kuingilia ili ku enforce
Kuruhusu CCM kuendelea na shughuli ni discriminations ambayo kikatiba imekatazwa.
Endapo ni specific form za mikutano, CCM wanaweza kuendelea na mkutano wao.
Hoja inakuwa, kwanini Zitto na ACT walikatazwa specific form pale millennium tower?
CCM hawafanyi mkutano kwa taratibu za usajili wa vyama.
Huu ni mkutano wa ziada katika kalenda yao, kwa maana kuwa siyo 'binding'
Wasipochagua mwenyekiti watakuwa hawajakiuka sheria yoyote ya vyama vya siasa.
Hivyo hoja kuwa ni kikao kinachozingatia sheria za usajili wa vyama ni misrepresentation!
Hoja inabaki , CCM wanafanya mkutano usio katika 'any forms au specific form'
Tunauliza, Polisi linawapa 'go ahead' kwa vigezo gani ambavyo wapinzani hawakukidhi.
Na Rais amepiga marufuku aina gani ya mikutano kati hizo mbili anazotetea Deus?