Magufuli bila madaraka yukoje?

Mkuu attachment yako in road width tu hamna roadreserve!

Road width ndimo ndani yake kuna roads reserve. kwa kifupi ni kitu kimoja. Sema tu pia kuna sheria ya Barabara ya Mwaka 2007 ambayo imengeza upana wa barabara kutoka mita 45 kwenda mita 60 ukiacha barabara ya morogoro
 
Mi namsupport Magufuli 100% asipoendesha zoezi la bomoabomoa, maeneo yote Dar yatageuka kuwa kebara slams!! huku kwetu sinza watu wamejenga kwenye open space na kuta zao wamevuka mipaka na kushrink barabara zote za mitaa. its really difficult, imagine mtu anajenga gorofa kwenye open space njia za kupita hakuna. Magufuli akaze buti. The problem I see with JK ni mwoga na I think he's scared that Magufuli will overshadow him, atafunikwa!!
 

Kama nilivyoonyesha hapo juu alikuwa kitumia Kanuni za Sheria iliyopoteza uhai kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge mwaka 1999. tatizo lako haujasoma thread wala attachment aya sheria husika unakimbilia kujibu tuu. Hapa lazima wasahabiki wa Magufuli mkubali kuwa wakati wote huu Magufulia likuwa ni muongo, na anatakiwa kuwaomaba radhi watu wote walioko nje ya Mita 22 ambao kwa mika 9 wamekuwa wakiishi kama wavamizi wa barabara kumbe sio kweli hata kidogo. Unafikiri watu hawa wameathirika vipi kiuchumi kwa kushindwa kutumia ardhi na nyumba zao kujiondolea umaskini?

Je unaujua mpango mzima wa fly overs utakavyokuwa na kuwa MT10 tu zinatosha.Ni dhahiri kuwa eneo lolote nje ya Mita 22 kama Setikali italihitaji ni lazima wananchi walipwe fidia. Kama kweli Magufuli alikuwa hodari na jasiri wa kulinda fedha za Serikali asingekuwa katika baraza la Mawaziri ambalo lilibariki mikataba yote mibovu katika mika yote 10 ya Mkapa na karibu 10 ya Kikwete EPA, KAGODA, MEREMETA n.k.
Tukubaline kuw Magufuli ana roho mbaya na watanzania wenzake, ila akina RA wakichota wanavyotaka anakaa kimya
 

Huwezi kutatua matatizo hayo kwa kutumia sheria feki kama anavyofanya Magufuli
 
Kuna msemo wa kidungu unasema " a fish in the pond" na si fish in the ocean, Magufuli anafanya jambo dogo sana na la kawaida sana kwani huu ni wajibu wa waziri yeyote, yeye anaonekana yupo juu kwa sababu mawazir wengine kama si wote kwenye wizara zao bado wanaendeleza sera za ccm za chukua chako mapema na kusinzia. LAKINI ukimdondosha huyu jamaa kwa wanaharakati mfano CDM ni kasamaki ndani ya bahari hutakaona kabisa.
Kwa hiyo magufuli unapomwongelea reference hapa in matter. Ndani ya ccm ni yuko kwenye kundi la afadhali lakini ndani ya wanaharakati ni ICU patient
 
Kubomoa sio shida sana ila fidia ni muhimu pia, haiwezekani watu wanajenga mpaka makazi yanakamilika halafu miaka mingi tuu wanalipa kodi zote including kodi ya majengo gafla unasema makazi si halali then bomoa bila malipo. Ninachofahamu huyu jamaa sasa hivi yupo kwenye ntoke vipi ili azidi kujiandaa na kuchaguliwa 2015
 
Wataalam kama Jatropha mpo lakini mnaacha watu kama Maghufuli wanatufanyia mambo kijanja hivo kama akina Kakobe wanavyofanya na Biblia yetu!
 
Huwezi kutatua matatizo hayo kwa kutumia sheria feki kama anavyofanya Magufuli

Hizo sheria zilipitishwa na vikao halali vya Bunge. Isitoshe ignorance of the law is no excuse... Bila barabara bora hatuwezi kurealize maendeleo lazima tuunge mkono jitihada za Magufuli, watakaoathirika waombe kudra kwa JK walipwe japo fidia kiodogo.
 
Mkuu Mwanakijiji, hii ishu ina sura kadhaa wa kadha, if you know what i mean, iko very TRICKY..Ngoja niendelee kuifwatilia kwa karibu, otherwise my mouth is zipped!
 

Sio lazima aendelee na siasa, kwa miaka hii 21 aliyofanya siasa matokeo yake tumeyaona. Pengine kwa taarifa yenu, Dr. Magufuli ni mwalimu tena mzuri tu, wanafuzi wake watakuwa mashahidi, wakati ule akifundisha somo la kemia.
 
Hivi kwa nini kwa wakati mmoja Raisi na PM wanamwandama Magufuli katika utendaji wake tena hadharaniiiii????????????????????????????
 
Hivi kwa nini kwa wakati mmoja Raisi na PM wanamwandama Magufuli katika utendaji wake tena hadharaniiiii????????????????????????????
Mambo yake Maghufuli anayafanya hadharani vilevile. Kila anakoenda na Tv mgongoni!
 
we Jatropha inaelekea ni mmoja wa waathirika wa bomoabomoa ndiyo maana unaongea even out of context. Nijuavyo mimi ipo ramani ya jiji zima la Dar, ukiangalia ramani hiyo na hali halisi on the ground ni kichekesho. Yaani watu wamejenga kiholela sana na walifanya hivyo kwa kudanganywa na maafisa ardhi kuwa ramani ingebadilishwa in their favour, hiyo ilikuwa miaka kama 10 au 20 iliyopita, hatua zisipochukuliwa basi daima hatutakuwa na barabara zenye ubora. njia pekee ni kubomoa baadhi ya nyumba ili kupisha ujenzi wa barabara, na hatua hii ni kwa faida ya taifa lote kwa ujumla. As I see it labda muombe fidia kidogo kwa JK.
 

Yet wananchi wakamchagua awe mbunge wao! uchafu wa magufuli unaweza kuwa nje ya jimbo lake kama akina EL, RA n.k lakini siyo kwake! issues za land mikoani siyo tatizo! kuna viwanja vinauzwa eka 15,000!!

You will need to have evidence though, maan pro-magufuli watakurarua tu!
 

Mkuu maada yako ni tata sana! hasa ukidefine neno mamlaka na wajibu wa aliyepewa mamlaka! kama kwajibika kwa magufuli kwa mamlka aliyonayo ni tatizo then we have problem somewhere

Je unaweza kutoa mfano wa asiye na mamlaka na yet ni mpiganaji au mtetezi wa mali ya umma
Pili je ulitaka magufuli afanye nini bungeni ili aonekane kuwa anapigania haki na kufabya unavyotaka wewe?

Baada ya majibu hayo je ili uonekane mpiganaji lazima

1. uandike article sana
2. useme sana bungeni (kama mbunge)
3. Jamii yote ijue wewe ni mpiganaji?

Je wale wasio na nafasi ya kujulikana kwa vigezo utakavyoonyesha wanaweza kuwa wapiganaji?

Je unaweza kutoa mfano mmoja wa waziri mmoja wa sasa na serikali zilizopita ambaye ni mpiganaji from bungeni mpaka serikalini na OUTPUT yake imeonekana?

Magufuli ulivyo-m-rate umetumia standard gani? job descritption yake inasemaje?

cheers
 

Akichagua bluu nitaona si mtu aliye na msimamo hata kidogo.
Wenzake wameshamshtukia na hivyo hawataweza kumpa hiyo nyekundu! CCM ni wezi na wanalindana. Hata siku moja hawawezi kumpa mtendaji.
 
Kulikuwa na kiongozi mmoja wa dini aliyemtembelea muumini wake wa kike, wakati wanazungumza wawili tu chumbani, kiongozi akamtamani, akaanza kumshika miguuni huku akimuuliza. Mama fulani nikishika mguu wako nitakosea? Muumini wa kike akajibu hapana baba. Kiongozi akasogeza mkono wake kwenye mapaja ya muumini, akamuuliza nikishika hapa nitakosea mama fulani? Muumini akajibu, hapana. Kiongozi wa dini akasogeza mkono wake, akamshika kiunoni akamuuliza tena nikishika hapa ni vibaya, muumini akajibu hapana, baadaye mambo yaliyoendelea mwayajua.Kiongozi huyu angeambiwa hapana???
 
Waberoya, umetoa maswali na hoja nzuri. Hatujatenda haki kwa huyo jamaa anayejaribu kutumikia jamii. Tena kuna kitu ambacho kimeniuma sana...yaani mtu anaomba kwa raisi aruhusiwe kutekeleza majukumu na sheria alizoapa? Yaani kutenda haki na wajibu sasa hivi mpaka ulambe miguu ya kiongozi wa mfumo unaotawala??? Hii ni hatari na hapo lazima nguvu itokayo juu iingilie kati
 
Dr. Magufuli atakumbukwa kwa misimamo ya KIJINGA eti anasimamia SHERIA kwa kuwafanya watu wazidi kuwa mafukara...tayari zaidi ya nusu yetu tunatumia CHINI YA DOLA MOJA kwa siku.....anampango sasa tutumiae CHINI YA NUSU DOLA kwa siku....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…