Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Sasa hapa sijakuelewa, amechuja kwa sababu haonekani kwenye magazeti au amechuja kwa kutotumikia taifa? Wakati mwingine sio kila kitu kiwe kisiasa, kuna mengine tuyatazame kama binadamu. Hivi wewe ulitaka watumishi wa uma waendelee na uzembe? Majizi serikali yaendelee kula na hao wafanyabiashara waendelee kutunyonya? Huyu unae mpondea ndio atakae boresha maisha yako, maisha ambayo mzazi wako alishindwa kukuboreshea.
 
Meli ya uvuvi ya China mpaka Leo inalipwa na Serikali .
 
Kazi ya kukusanya kodi wamepewa mapolisi barabarani na vi makxmalipo vyao ole wako uingie kwenye anga zao utajuta
 
kisa tu aliamua kuzuia vibali pasipo kutafakari wala kuitathimini wala kushauriana na bodi ya sukari , sasa kuna Richmond ya sukari inakuja mda si mrefu si unajua wajanja hupenya pale pale kwenye uhaba .
Sukari ni hewa?!?!?! hebu tafuta mbadala maisha yaende tuko kwenye mageuzi. Vumilia shida ya mwaka mmoja ufurahie maisha miaka 9!
 
Ngoma ikivuma sana hupasuka haraka .Magu zilikuwa ni mbio za sakafuni zimeishia ukingoni.
 

Yote uliyoyasema ni kweli kabisaa lakini wanyonge sie na magufuri, tutajitahidi kumwombea kwa Mungu hakati mirija ya fitina , uongo, Vita ya mabwanyenye anakaribia kuishinda kwani inabidi arudishe kidogo sera za ujamaa, ambazo baadhi wanaziita ujima.
 
Binafsi hua kamwe sipendi viongozi wenye mlengo wa ukomunist/ujamaa hua ni idealistic,imaginary na wapenda sifa na hatimaye kuharibu maendeleo.Sasa huyu ndo tumempata tutapiga marktime mpaka tushangae
 
Umenena vema mkuu
 
Maskini Magufuli ana nia njema sana na nchi hii tatizo sijui ni mbinu anazotumia au ni wanaomshauri binafsi kuna vitu namuelewa sana ingawa hili la uhuru wa vyombo vya habari simuelewi kabisaaaaa
Chukua like milioni 6 baby..
 
Kufanya mambo kwa sifa ni hatari sana.tulianza kwa kusomewa taarifa za mapato na TRA kila mwezi kwenye TV Leo huu mwezi wa pili huu kimyaa .kuendesha nchi hakuhitaji mbwembwe.
 
Binafsi hua kamwe sipendi viongozi wenye mlengo wa ukomunist/ujamaa hua ni idealistic,imaginary na wapenda sifa na hatimaye kuharibu maendeleo.Sasa huyu ndo tumempata tutapiga marktime mpaka tushangae
Hilo ni moja kati ya matatizo ya Mkulu wetu
 
Nonsense kabisa.
Magufuli ameshawah kukwambia anataka umaarufu?
Au unafikiri Magufuri ni kama msanii anaetoa wimbo ili ukubarike mitaani?
 
Tembo anabebeshwa ubongo wa kuku

Haya yanayotokea ni matokeo ya mifumo mibovu iliyowekwa kwa watu wenye fedha zao kuwa na maamuzi ikitokea mabadiliko kama haya anayoyafanya JPM ni lazima waathirika watakuja huku wataka hali iliyozoeleka iendelee.

lkn wananchi walinganishe na namna gari ukipaki mlimani wakati wa kuondoka itaonekana kurudi nyuma na baada ya hapo itaendelea na safari hivyo kwa juhudi hizi za makusudi nataraji kuona maisha bora muda si mrefu ingawa lazima kwa kuanza mikono itaota sugu kiasi
 
Nimeona hali inabadirka sana.Watanzania wepesi wa kusahau haraka sana
 
Yaani...sikutegemea karne hii kama nchi hii tungeishi maisha ya Nyerere..

Eti sukari imeadimika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…