Magufuli amefanya haya Katavi ndani ya Miaka Mitano

jijiletublog

Member
Jul 23, 2020
31
74
STAND YA MABASI
SAT, chini ya uongozi wa raisi JPM imefanikiwa kujenga stand ya mabasi mkoani Katavi wilaya ya Mpanda na kuipatia jina la stand ya mabasi ya Mizengo Pinda kwa heshima ya waziri mkuu mstaafu mheshimiwa Mizengo Pinda. Ujenzi wa stand hii ulianza tarehe 22/5/2015 na kumalizika tarehe 1/12/2018. Stand hii ilijengwa kwa ghharama za shilingi bilioni 4.3 ikihusisha ujenzi wa stand ya mabasi, kituo cha polisi, vibanda kwa ajili ya wafanyabiashara na wakata tiketi Pamoja na fence ya kuizunguka stand hiyo. Stand hii inauwezo wa kupaki magari makubwa 64 ya aina ya Yutong yenye urefu wa mita 13, ina mageti manne kwa ajili ya kuingia na kutoka na moja kwa ajili ya abiria wanao ingia ndani ya stand.

MRADI WA UMEME

SAT, imefanikiwa kupeleka huduma ya umeme wilayani Mpanda, unaoweza kuhudumia vijiji 30 mpaka sasa ikiwa ni vijiji 55 katika bajeti. Upatikanaji wa huduma hii ya umeme umewarahisishia Maisha wakazi wa wilaya ya Katavi kwani sasa wanaweza kuendesha shughuli mbalimbali zinazotumia umeme kama kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kufyatua tofali na kutengeneza samadi. Pia umeme huu unawafaa majumbani, kwenye vituo vya afya na pia ni nishati mbadala badala ya kutumia kuni ama mkaa kama ilivokuwa hapo awali. Pongezi zimuendee raisi magufuli kwa kuwa kiongozi bora aliyeweza kusimamia serikali yake ikawafikishia huduma watu wa Katavi. Anastahili miaka mitano tena aweze kumalizia mradi huu na kuongeza mingine kwa manufaa ya watanzania.

MRADI WA BARABARA

Barabara iliyojengwa mkoani Katavi wilaya ya Mpanda ina urefu wa kilomita 35 na ni umbali wa km 135 tu unaoiunganisha reli ya kisasa na mkoa wa Katavi. Ujenzi wa barabara hii umeleta manufaa kwa wanaKatavi kwani umewapunguzia kero za ukosefu wa usafiri kwa ajili ya miundombinu mibaya ya barabara na kuwasogezea huduma za treni ya kisasa kwa ukaribu Zaidi. Barabara hii ni manufaa kwa wanakatavi kwani sasa wakulima wanaweza kusafirisha mazao yao toka mkoa wa Katavi mpaka mikoa mingine na hivo kuwaongezea kipato. Wana Katavi, wanaishukuru SAT Pamoja na raisi JPM kwa kuwafikishia huduma hii, wataonesha Imani yao kwa kumuongezea raisi JPM miaka mitano tena ili aendelee kuleta maendeleo mkoa wa Katavi.

MRADI WA MAJI

Mradi wa maji wilayani mpanda mkoa wa Katavi unauwezo wa kuhudumia wananchi Zaidi ya 300,000 mpaka sasa, na umefanikiwa kupunguza tatizo la maji katika vijiji vingi wilayani humo. Maji haya yanatumia umeme wa solar kupandishwa kutoka kwenye vyanzo vyake mpaka kwenye matenki special kwa ajili ya kutunzia maji yaliyowekwa. Kwa sasa maji haya yanaweza kuhudumia majumbani mpaka kwenye vituo vya afya ambako kulikuwa na shida ya maji hapo awali na hivyo kupunguza magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji machafu na tatizo la kina mama kufata maji umbali mrefu. Pia maji hayo yanapatikana kwa gharama nafuu kwani ni sh moja kwa lita, hivyo ndoo ya lita kumi ni shilingi kumi. SAT, chini ya uongozi wa raisi JPM imefanya kazi kubwa katika kuboresha huduma hii kwa wakazi wa mpanda.
 
Katavi wanapaswa kumshukuru Jakaya Kikwete kwa kumfanya Pinda kuwa waziri mkuu, kisha Pinda kubabeba huko. Ujio wa Magufuli umedumaza kasi ya maendeleo ya Katavi kwa zaidi ya 50%.
 
Juzijuzi nilikuwa Kibaoni kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda nilichokishuhudia kula ni Wapimbwe wanaishi katika umasikini mkubwa sana
 
Back
Top Bottom