Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,582
Akiiba asisemwe? Nafikiri upinzani unafanya vizuri haumwonei mtu kwao rafiki ni mtu mwadilifu ukiwa fisadi lazima utamulikwa tu ,Magufuli ni JEMBE, mtapoteza muda bure kudunduliza skandali dhidi ya huyu jamaa, mbona mawaziri vilaza cc wako wengi tu, nendeni huko mkafunge magoli!
narudia tena na tena kuwa ndani ya CCM hakuna alie msafi!Hii imetoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyooko chini ya Dr John Pombe Magufuli. Mheshimiwa Spika,baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu ¡°malipo ya madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi usiohalisi hs.252,975,000,000. Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi¡± (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98) Mheshimiwa Spika,fedha hizi ¡°zilizopotea¡±au ¡°kulipwa kifungu hewa¡± ni sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara ifuatazo kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014; i. Barabara ya Usagara-Geita-Kyamyorwa (KM 422) ii. Barabara ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza- Kaliua-Tabora (KM 443) iii. Barabara ya Nangurukuru-Mbwemkulu (KM 95) iv. Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (KM 112) v. Barabara ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264) vi. Barabara ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda (KM 359) vii. Barabara ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi- Londo-Lumecha/Songea(KM- 396) viii. Kuondoa msongamano barabara za Dar (KM- 102.15) Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane (800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya ¨C Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu ¨CGoba (KM 9), zimepotea kutokana na ufisadi huu. Chanzo: hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa msaada Marcossy Albane. Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
jamaa huwa msanii mbele ya vyombo vya habari lakini hakunaga mrejesho.... naweza kukuaibisha mbele ya media badae anakuomba msamaha. anakwambia its politics...
Kwenye vivuko amesema hivi,
1. Shilingi bilioni 3 kununua kivuko kitakachofanya kazi kati ya Dar ES Salaam -Bagamoyo
2. Ujenzi wa maegesho mwambao mwa Bahari ya HIndi katika maeneo ya Magogoni na RUngwe oceanic shilingi bilioni 2.5
fedha zote hizi zipo kwenye fungu 4125 na jumla kwenye kifungu hiki zimetengwa bilioni 5.990.....tafakarini
Mkuu kwani hiyo ishakua kashfa kwa waziri? Wengi tunamuona huyo mCCM jembe.
huu ni uzushi, hakuna ukweli wowote hapo...hizi ni takwimu za kupakana matope na hazitafanikiwa
mtahangaika sana kumchafua pombe lakini itawamwagikia tu na mtanuka wenyewe
mtahangaika sana kumchafua pombe lakini itawamwagikia tu na mtanuka wenyewe
Barabara anazojenga Magufuli zote hazina viwango, mashimo baada ya miezi miwili huku gharama za kujenga ziko juu (800,000,000 kwa kilomita moja). Huyu jamaa utasikia anapigiwa chapuo la kuwa rais kwa huu ubabaishaji na maCCM wenzie. CCM hakuna mwenye afadhali jamani, ngoja tusubiri utetezi wake kwa hizo hela alizokwapua
Hapo nadhani kuna technicalities juu ya ulipaji wa madeni na wala si ubadhirifu. Nasikia miaka ya karibuni serikali imekuwa ikiingia katika madeni makubwa na wakandarasi. Nitapenda kusikia ufafanuzi toka kwa Waziri wa Ujenzi Dr. John Joseph Pombe Magufuli wakati anahitimisha uchangiaji kwenye hotuba yake pamoja na wakati wa kupitisha bajeti kifungu kwa kifungu! Magufuli kama amekula MUKU vile manake akisimama kuongea hata kama ulikuwa unataka kumkamata pabaya unalegea na kumuacha atiririke. Ataanza kuongea kwa taratibu huku akiwa kama anaonyesha kuonewa kisha atashuka na data na kutaja barabara ambazo zipo kwenye jimbo la mbunge husika na mwisho kuwaambia niacheni nifanye kazi; hapo tena kila mtu kimya na matokeo yake ni kumuomba aangalie na barabara zao.
Magufuli kiboko; leo mtamsikia atakavyopangua hayo yote!
Hata kama unampenda mtu kiasi gani sifa lazima ziwe na reservation. Kama kweli anazo data mbona hata siku moja hajawahi kutushawishi kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali? Mbona ndugu yake na nyumba ndogo waliingizwa kwenye mgao hajawahi kukanusha with such cooked data. Wlatini wana msemo "qui omne dict nihil excludit" anayeongea kila kitu hatofautishi kitu. Sio kila mashahiri yake yana maslahi kwa taifa
Na wewe umeshawahi kushawishika kuhusiana na uuzwaji ule? Sababu zake zimewahi kukushawishi wewe au kwa vile walikuwa kundi la walaji wakakubaliana pamoja? Kana kwamba wakiondoka na Ben ndio mwisho wa uwepo wa serikali na viongozi wake , wakauza mpaka nyumba za OCD ndani ya vituo vya polisi kana kwamba ndio mwisho wa kuwa na OCD kwenye vituo hivyo, wameuza mpaka makazi ya SPika , kana kwamba hatakuwepo mwingine leo tunajenga kwa mabilioni wakkati waliuziana kwa bei chee......Kuhusu kuuza nyumba za serikali Magufuli alilishawishi Baraza la Mawaziri na wakaridhia kwa sababu ambazo alizitoa.
Na wewe umeshawahi kushawishika kuhusiana na uuzwaji ule? Sababu zake zimewahi kukushawishi wewe au kwa vile walikuwa kundi la walaji wakakubaliana pamoja? Kana kwamba wakiondoka na Ben ndio mwisho wa uwepo wa serikali na viongozi wake , wakauza mpaka nyumba za OCD ndani ya vituo vya polisi kana kwamba ndio mwisho wa kuwa na OCD kwenye vituo hivyo, wameuza mpaka makazi ya SPika , kana kwamba hatakuwepo mwingine leo tunajenga kwa mabilioni wakkati waliuziana kwa bei chee......