Magufuli aibua ufisadi wa Sh5 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli aibua ufisadi wa Sh5 bilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,451
  Likes Received: 418,959
  Trophy Points: 280
  *AAGIZA JENGO LA TANROADS LIVUNJWE

  Tuesday, 01 February 2011

  Fidelis Butahe

  WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli amefichua ufisadi wa Sh5 bilioni uliotaka kufanywa katika manispaa tatu za jijini Dar es Salaam kwenye ulipaji wa fidia za ubomoaji wa nyumba kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara.

  Mbali na kufichua ufisadi huo jana, Magufuli ameagiza jengo la Wakala wa Barabara (Tanroads) lililopo ndani ya Kituo cha Daladala cha Ubungo, libomolewe ndani ya siku tano kuanzia jana kwa kuwa lipo ndani ya hifadhi ya kituo cha mabasi yaendayo kasi.

  Dk Magufuli aligundua uozo huo na kutoa maagizo ya utekelezaji jana katika ziara yake ya kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Dk Magufuli, majengo ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini humo, nayo yapo ndani ya hifadhi ya barabara jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Barabara Namba 167 ya mwaka 1967.

  Akizungumza kabla ya kuanza ziara hiyo, Dk Magufuli alisema kuwa Serikali haikuridhika na tathimini ya kwanza iliyofanywa na wathamini kutoka Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke na kuthibitishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali.

  "Gharama za tathmini hiyo ilikuwa Sh27.7 bilioni kwa mali na nyumba 1,487. Lakini kabla ya kulipa, wizara iliona vyema kujiridhisha kwa kutembelea eneo la tathimini husika na kugundua mapungufu kadhaa," alisema Magufuli na kuongeza:

  "Mapungufu hayo ni pamoja na kurukwa kwa baadhi ya mali na nyumba pamoja na gharama za nyumba zenye sifa sawa kutofautiana kutoka manispaa moja na nyingine."

  Baada ya kugundua mapungufu hayo, Dk Magufuli alisema Wizara ilimtafuta mthamini wa kujitegemea ‘Independent Valuer' ili afanye uhakiki na kurudia uthamini pale ilipohitajika kwa maslahi ya taifa.

  "Unajua ilikuwaje? Nyumba zipatazo 61 zenye thamani ya Sh 239,781,542 hazikuonekana, kati ya hizo nyumba 56 zipo katika eneo la barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner na nyumba tano ziko eneo la kati ya stendi ya mabasi ya Ubungo na Kigogo," alisema Magufuli.

  Alisema kuwa baada ya tathimini mpya kufanywa, gharama za nyumba zote ni Sh 22,710,003,114, tofauti na uhakiki uliofanywa na manispaa hizi tatu, uhakiki wa independent valuer umefanya Serikali iokoe Sh5 bilioni.

  Alisema kuwa baada ya matokeo hayo, wizara iliamua kukamilisha tathimini ya nyumba 215 zilizokuwa zimebaki katika mradi ambazo zimethaminiwa na kuwa Sh 2,638,726,633 na kwamba hatua hiyo ilifanya tathimini yote kuwa na nyumba 1580 kwa gharama ya Sh 25,348,729,752.

  "Tathimini hii imesainiwa na wahusika wote tayari kwa malipo kwa wale tu wanaostahili kulipwa kwa mujibu wa sheria ya barabara namba 13 ya 2007. Wanaostahili kulipwa wataanza kulipwa keshokutwa (Alhamisi), waje na vitambulisho vyao, picha zao tunazo hivyo wasijaribu kufanya uhuni,' alisema Magufuli

  Aliongeza, " Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakuu wa wilaya na wakurugenzi, kuweni makini sana na hawa maofisa wa ardhi wa wilaya, wanaweza kuitia Serikali gharama zisizostahili, hizi Sh5 bilioni si zinajenga barabara nyingine."

  Alisema kuwa majina ya wamiliki hao hewa wa nyumba 61 atayakabidhi kwenye mamlaka husika ili wachukuliwe hatua kwa kukiuka taratibu kwa kuwa wamesababisha ujenzi wa barabara hiyo kuchelewa na kuitia Serikali hasara.

  Magufuli alimweleza kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq kuwa manispaa za jijini Dar es Salaam zina watendaji wabaya na kumtaka kuwashughulikia.

  "Afisa ardhi gani anagawa viwanja katika maeneo ya barabara?, tuwachukulie hatua na ikibidi tuwaweke ndani. Wanatuharibia halafu wanakuwa wa kwanza katika vikao vyetu, hawa ndio wanaichonganisha Serikali na wananchi," alisema Magufuli.

  Akitoa ufafanuzi wa watu wanaostahili kulipwa katika upanuzi wa barabara inayoanzia Stendi ya Mabasi ya Ubungo mpaka Jengo la Klabu ya Yanga lililopo Ilala, Magufuli alisema kuwa waliojenga nyumba zao kuanzia Mabibo Mwisho mpaka Ilala Mchikichini, hawatalipwa.

  "Eneo la Klabu ya Yanga mpaka Ilala Mchikichini kabla ya kuvuka daraja, waliojenga nyumba pembeni ya barabara hii watalipwa fidia kwa kuwa eneo hilo halipo katika sheria ya 167 ya mwaka 1967 na pia halipo katika sheria ya barabara kifungu cha 13ya mwaka 2007," alisema Magufuli.

  Akiwa anapita katika barabara hiyo na kusimamisha magari huku akiwaeleza wananchi kuhama maeneo hayo, Magufuli alisema wengine watakaolipwa katika upanuzi wa barabara hiyo, ni wale waliojenga nyumba zao kuanzia Ubungo Kisiwani hadi Mabibo Ward na kwamba nyumba 201 ndio zitakazolipwa. Alisema mradi huo utagharimu Sh 4,429,336,710.

  "Nyumba zilizojengwa katika eneo la barabara ambazo zipo, Mbuyuni, Mabibo Farasi, Mabibo Matokeo, Mburahati Kisiwani, Kigogo Mkwajuni na Kigogo Kati, hazitalipwa kwa kuwa eneo zilizopo ni kwenye Highway Ordinance chini ya Sheria namba 167, na pia zipo katika Sheria ya Barabara Namba 13 ya mwaka 2007," alisema Magufuli.

  Mbali na kutembelea barabara hiyo, Magufuli pia alikagua ujenzi wa barabara ya Jet Corner - Yombo Vituka- Davis Corner na kusema kuwa mradi huo utagharimu Sh 11,989,526,692. Alisema wananchi wote waliojenga pembezoni mwa barabara hiyo, watalipwa.

  "Barabara hii ina urefu wa kilomita 10.3. Hawa wote watalipwa isipokuwa katika maeneo ambayo kulifanyika ulipaji kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege, ujenzi wa Daraja la Mwinyi, nyumba zipo 766," alisema

  Aliongeza, "Nyumba 149 zilizopo maeneo ya Kiwalani Kigilagila na Nyambwela bado zinafanyiwa uhakiki kwa kuwa pia zilihusika katika ulipaji wa fidia wa mradi wa Jet-Lumo miaka ya nyuma, uhakiki zaidi unahitajika."

  Magufuli ambaye alifanya mkutano na kuzungumza na wananchi wa Yombo mara baada ya kuikagua barabara hiyo, alisema kuwa barabara hizo ni kubwa hivyo hazitawekewa matuta bali kutakuwa na alama za barabarani.

  Alisema kuwa wananchi watakaochelewa kubomoa nyumba zao zitabomolewa na Serikali na hawataambulia chochote kwa kuwa kila kitu kitachukuliwa na Serikali kwa kuwa nyumba hizo zitakuwa zimeshalipiwa fidia na Serikali.

  Alisema kuwa Serikali itatumia sh 17,973,091,427 kwa kulipa fidia.

  "Kama nyumba yako imeingia nusu ndani ya eneo la barabara, itabomolewa hiyo nusu na wewe utalipwa kulingana na ulivyobomolewa, hatuwezi kulipa gharama ya nyumba nzima wakati umebomolewa nusu," alisisitiza.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,451
  Likes Received: 418,959
  Trophy Points: 280
  Magufuli na Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lipo njia panda kwa upande mmoja Magufuli anawatetea watendaji ndani ya TANROADS na kwa upande mwingine anakiri kuna wimbi zito la ufisadi ndani ya taasisi hiyo.......huku wabunge wakidai mchujo usifanyike ndani ya TANROADS na hivyo kuashiria kuridhika na wimbi la ufisadi ndani ya taasisi hiyo.........................

  Ukweli unabakia ya kuwa bila ya kuisafisha TANROADS hata hizo barabara hazitajengwa kwa bei na ubora ambao jamii inategemea.........................

  Tunahitaji fyagio la chuma lianzie kusafisha hapo TANROADS na mikakati ya ujenzi wa barabara itafuata baadaye..................
   
 3. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Well done John Pombe:clap2:
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nimepapenda hapo
   
 5. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Usiishie hapo tu wachukulie hatua kali wote waliotaka kuitia serikali hasara. Watanzania tutafurahi kuwaona watendaje kama hao na wao wakiwa magerezani
   
 6. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huu sio mda wa kumpongeza magufuli kwa kazi nzuri! Mambo kama haya ndio yanafanyika kila siku ndani ya serikali! Kwa maana nyingine bile Magufuli hakuna udhibiti wa Ufisadi kama huu!

  Its time tuiwajibishe serikali! Tuandamane kupinga wizi wa scale hii serikali inaangalia tu! Rais yuko kimya why??
   
 7. r

  rmb JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi kweli kweli! Mama Tibaijuka naye kaishia wapi tena mbona kimya?
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huyu baba ni balaa.....
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wabongo kila mradi kuna dili! Hivi hata huku Tanroads nako ni Rosatam? nadhani kila familia inae ROSTAM mmoja, na itakapobidi mapambano dhidi ya ufisadi yaelekezwe nyumba kwa nyumba, tuwatoe mmojammoja na kuwachoma moto ndio kitaeleweka!
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,451
  Likes Received: 418,959
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Well done John Pombe:clap2:
  Magufuli ni lazima aelewe kazi hizi za umma hawezi kuzifanya pekee yake................zinahitaji kuimarisha miundo mbinu ya kitaasisi..............vinginevyo atashindwa..................akumbuke kidole kimoja hakivunji chawa.............................
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,451
  Likes Received: 418,959
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Usiishie hapo tu wachukulie hatua kali wote waliotaka kuitia serikali hasaraWatanzania tutafurahi kuwaona watendaje kama hao na wao wakiwa magerezani
  majukumu hayo yako Takukuru ambako Dr. Hosea alikwisha kusema nchi hii haina rushwa na ile iliyopo yaani ufisadi bosi wake JK kampiga "stop" asishughulikie....................................na ndiyo maana hakuna ufisadi wa maana ambao hadi leo kuna mtu katiwa hatiani mahakamani.......................................
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,451
  Likes Received: 418,959
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Nimepapenda hapo
  Hapo ulipopapenda ndipo serikali yetu italizwa mahakamani na kutakiwa kulipa mabalioni ya fidia...........huyu Magufuli sijui ni msingi gani ulitumika kumpa Wizara ya Miundo Mbinu..............................

  Ukiisha ibomoa nyumba ya mtu hata iwe ni kidogo au nusu.............................maana yake umeidhoofisha na haifai kuendela kwa matumizi ya Binadamu.......na usipoilipa yote na kuimalizia kuibomoa utajikuta unadaiwa fidia ya nyumba yote na gharama nyinginizo za faini kwa kumtoa mtu kwenye pango lake nma kumsababishia maumivu ya kukodisha kwingineko..........................
   
 13. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Magufuli

  Kaza Mwendo baba na endelea na juhudi hizo hizo.

  Tanroads kuna UOZO WA KUNUKA.

  5yrs back mpk sasa eti mapato ya Kivuko cha kigamboni ni Sawa yaani hesabu ni ile ile kwa siku
  teh teh teh tehe

  Yaani wa2 wanakula mpk wanajisahau
   
 14. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
   
 15. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mimi sina neno na mtazamo wa watu.... ila ningefurahi sana kama ningejua HUYO PRIVATE VALUER kaliwa shilingi ngapi maana usije ukakuta amelipwa 4.9bl alafu sisi tunabakia kusifia tu.

  Ni vizuri tuambiwe gharama za huyo private value ndo tupime uokovu uliojitokeza
   
 16. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ka wahalifu wengi, Pombe kamata piga hao ndio wanaangamiza taifa hao kila siku kula rasilimali zetu,taifa limewasomesha kwa gharama kubwa kisha wanakwapua,hongera pombe :clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
   
 17. g

  gamaliely Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Dr. magufuli endelea hivyo hivyo, Watanzania tunawahitaji watu kama nyinyi
   
 18. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Colleagues,

  We should know the tricks of our current leaders. Anachofanya Magufuri ni kiini macho tu kwa wantanzania. Jiulize kwa nini hakupewa nafasi hiyo na JK miaka mitano iliyopita? Inamaana hawakujuwa kuwa Magufuri angelileta mabadiliko kama haya for the last five years. I tend to believe that what is being done now by those we call/know as good leaders within CCM are trying to pave their way for the next election. I do not expect much from them unless I see JK ordering Hosia of TAKUKURU to resign; DOWANS payment ceased and those concerned with the deal including Mwanasheria Mkuu...
   
 19. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Itakuwaje Wenye Nyumba wasilipwe kwa Sheria ya Mwaka 2007 wakati kuna waliojenga Nyumba kabla ya mwaka huo?.
   
 20. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Our leaders are not futurustic ndo maana kila siku ni mambo ya kufidia tu
   
Loading...