Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,424
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo.

Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana.

Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile.

Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
 
Magufuli bado ni trainee kwny ajira yake hii mpya, bila shaka anahitaji sana msaada wa ushauri toka kwa watangulizi wake....kuwadhalilisha hadharani ni nzuri kwa upande wake hasa akihitaji sifa za waliomchagua, ila ni mbaya sana pale atakapohitaji msaada toka kwa kaka zake, mfano kwny mgogoro wa Zanzibar kina Mkapa na Kikwete wanahitajika sana#

Hebu tujikumbushe ya Mkapa alieingia madarakani akiwa msafi hana doa (Mr Clean), lakini alikuja kumaliza uongozi wake akiwa amechafuka kupindukia!

Kila lakheri Dk Magufuli, ila angalia usije ukatukana mamba kabla hujavuka mto!
 
Kuna mambo kama tusipobadilika hali yetu itazidi kuwa mbaya zaidi,Taifa zima kuanzia viongozi hadi wananchi tunapaswa kubadilika.Magufuli yote aliyoongea ni ukweli tuache unafiki
 
Hakumponda raisi,raisi hyo ni kazi yke kwenda nje na kujenga mahusiano Mazuri na nchi jirani..aliponda baadhi ya safari za Idara za serikali kwenda nje hovyo hovyo..Mimi hapa mwenyewe nashuhudiaga wakurugenzi wa Idara za benki kuu wakienda kutanua Malaysia na Singapore kila baada ya mieZi mitatu
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.
 
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa
 
Huenda ni mbinu take ya kumsogeza mbali na ikulu ili asijegeuka remote. Kujihami ini muhimu katika uongozi ili kuwakwepa wabia hasa wastaafu. Au ni mwendelezo wa mnyukano wa Mr.tabasamu na Mr. Clean unaendelea? Rejrlea chaguzi za kujaza nafasi mbalimbali muda wa lala salama Kama ulikuwa na sababu za msingi. Ni mtazamo tu.
 
Wapi amemsema Kikwete,Magufuli alikuwa anazungumzia ngazi za chini sio ngazi ya uraisi
 
JPM anafanya kazi aliyowaahidi Watanzania, haya mengine ni majungu tu. Fanya kazi JPM tupo nyuma yako hawa walafi walizoea kufuja pesa za walipa kodi. Tunataka maendeleo ya kikweli sio safari za kujifariji na ulaji.
 
hatutaki wanafki kulindalindana
bora amesema kweli

mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!
 
Ukweli, Mzee Kikwete alipewa za uso hadi aibu!

Aliimba tutaisoma namba,sasa yeye ndiye anayeisoma namba,Rizmoko Jana macho yalikuwa yanamtoka balaa,naamini masikio yalikua yanapitisha upepo balaaa
 
Udhalili upi kusema safari za nje mbona hilo ni ukweli sio kudhalilisha watendaji walikua wakijipangia tu wanapoona kwao ifaa bila kijali kama ni upotevu wa pesa za walipa kodi
 
Aache mabovu ya watangulizi wake, achukue mengi mema yao aunganishe na dhamira yake njema ktk kuelekea Nchi ya ahadi aliyotuahidi.

Tuwashukuru wazee hawa ktk zama zao na salama walotuachia na sasa tumuombee Magufuli atende impendezavyo Mungu na kuiepusha Tanzania kuwa ni nchi ya visingizio.

Nimefurahia neno moja jana "NCHI HII NI TAJIRI" JPM....Admission hiyo ni wazi amedhamiria kuonyesha UTAJIRI WETU ambao tangu JKN ,AHM,BWM na JMK walishindwa kutamka neno hilo hadharani.
 
Watanzania hamueleweki? Mnalalama matumizi ya serikali makubwa halafu Kaja mtu msema kweli anaguza maeneo ya kuthibiti na Anglia tena Huyu mleta Uzi anasema nini. Nahisi huyu bwana Ana bifu n.a. Magufuli n.a. atapinga chochote atakachokifanya. Poor you.
 
Mbona huyu JPM akiwa WAZIRI alikuwa anatetea safari za raisi na kusema zilikuwa na tija ndiyo maana mabarabara yamejengwa? Hapo hakuwa mnafiki? Namuunga mkono kupiga marufuku safari za nje zisizo na tija ila naye akiwa waziri alikuwa anamtetea raisi wake. Iweje leo?
 
Back
Top Bottom