Magufuli aagiza wanafunzi, wasafiri bure

Magufuli aagiza wanafunzi, wasafiri bure

chaikavu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2015
Posts
760
Reaction score
473
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

"Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu," alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

"Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming'oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu" alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?

Nitawaona Wanamtwara watu wa ajabu sana kama wakiamini hizo propaganda.
Ila walinifurahisha sana walivyoususia mkutano wao na uzinduzi wa hicho kivuko.
 
Inamaanisha leo.ndio.kaenda mtwara...ama.ameupat uwaziri.leo hii..sikuzote alikuwa wapi..shtuken watz..
 
magufuri njoo iringa ufukie lile shimo katika ya barabara lililosababisha ajali.
 
Changamoto kubwa kwa watanzania ni za uchumi duni, viongozi waje na mkakati wa kuongeza kipato kwa wakulima ambao wanakadiriwa kuwa 80% ya population vinginevyo tutakuwa tunadanganyana. Watanzania wapewe nyavu na si samaki hapo tutafika.

Lakini pia udhibiti wa rasilimali za taifa na matumizi mabovu ya fedha za umma yaangaliwe kwa jicho pevu
 
Halafu akitwaa urais atawageuka walipe huyo ndo buldozer magufuli
 
Nitawaona Wanamtwara watu wa ajabu sana kama wakiamini hizo propaganda.
Ila walinifurahisha sana walivyoususia mkutano wao na uzinduzi wa hicho kivuko.

Kivuko kilikuwa kimeshazinduliwa na Hawa Ghasia sasa etiJK naye kajakuzindua tena...yani uzinduzi juu ya uzinduzi....mwisho magufuli naye atakuja kuzindua tena.
 
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?

Hizi ni kampen kabla ya wakati
 
Kivuko kilikuwa kimeshazinduliwa na Hawa Ghasia sasa etiJK naye kajakuzindua tena...yani uzinduzi juu ya uzinduzi....mwisho magufuli naye atakuja kuzindua tena.

Duuuuuhhhh mambo juu ya mambo,ama kweli tunafanywa Mabwege ile mbaya.Hebu nikuombe kama unazo picha za uzinduzi uliofanywa na Mh. Hawa Ghasia tuwekee ili hawa wakubwa wajuwe na sisi tuna akili,siyo wao tu.Au Mh.Rais kapigwa changa la macho...
 
Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Mkuu hiyo figure hapo imekaa vizuri kweli..? milioni tatu au..? Maana na kampeni zao hizi za mapema wanaweza kukosea mpaka figure za ukweli..
 
Kivuko kilikuwa kimeshazinduliwa na Hawa Ghasia sasa etiJK naye kajakuzindua tena...yani uzinduzi juu ya uzinduzi....mwisho magufuli naye atakuja kuzindua tena.

Magufuli pia si alikuwepo siku ya uzinduzi? Wanajaribu kumuuza huyu jamaa sana ila hauziki.
 
Hatukawii kuasikia wamachinga wasibuguziwe popote pale watakapofanyia biashara,
Boda boda waache huru kufanya kazi zao katika ya jiji kwani wanajipatika riski,
Mama ntilie, Wamachinga na wapika vitumbua katikati ya jiji ni marufuku kuwakamata kwa sasa kwani serikali ya awamu ya tano itakuja na mipango mkakati wa kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu masuala haya.

Kidumu chama cha Mapinduzi.........!!!

Kali nyingine aliyoitoa siku iyo ni alipowaambia wanafunzi bure na wazazi wao wakitaka kupanda bure wavae sare za shule
 
Hizi ni dalili za wazi za kuchanganyikiwa na mafuriko ya UKAWA !

Kwanza muongo....serikali ina fweza gani wakati madeni yamewazidi kimo...?

Huko mnajisumbua mlishatesa watu na kuwapiga sababu ya gesi....sasa hata mgawe malori kwa kila kaya mtapigwa chini tuuu
 
Back
Top Bottom