Magufuli aagiza wanafunzi, wasafiri bure

Magufuli aagiza wanafunzi, wasafiri bure

Sasa wewe unataka kufananisha umati wa kigamboni na ni mjini upande panton bure,running cost nani ata incur? Mbona tunakuwa na vichwa vigumu kuchambua mambo?,uchumi wa mtwara ni sawa na dar?, population ya watu wanaovuka kwenda msanga mkuu ni sawa na wanaovuka kwenda kigamboni?,angalia fuel consumption,maintenance ya kivuko

Population inahusiana vipi na priority ya wanafunz wa mtwara dhidi ya wale wa kigamboni? Acha unazi
 
Eti asiye na nauli avae sare za shule nae atavuka bure unamdanganya nani asiyekujua?
 
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?



Kivuko cha mil 3.3 kimekuwa bajaj??
 
Huyu baba na sura yake mbaya wallah hawezi kuwa Rais wangu.
 
Back
Top Bottom