Magufuli aagiza wanafunzi, wasafiri bure

Mkuu hiyo figure hapo imekaa vizuri kweli..? milioni tatu au..? Maana na kampeni zao hizi za mapema wanaweza kukosea mpaka figure za ukweli..

Itakuwa ni Bilioni 3.3. Maana kwa milioni hata mie ningekuwa na cha kwangu pale mto lukuledi.
 
hatukawii kuasikia wamachinga wasibuguziwe popote pale watakapofanyia biashara,
boda boda waache huru kufanya kazi zao katika ya jiji kwani wanajipatika riski,
mama ntilie, wamachinga na wapika vitumbua katikati ya jiji ni marufuku kuwakamata kwa sasa kwani serikali ya awamu ya tano itakuja na mipango mkakati wa kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu masuala haya.

Kidumu chama cha mapinduzi.........!!!

kigumu sana ccm....!!!!
 
Kwanza hao watu waliojipendekeza kwenye huwo kiuzinduzi kake mchwara Ni wadogo kama viJicho vyake
 
Mbona kivuko kutoka Kigamboni kwenda Magogoni ni bure kwa wanafunzi, wazee, na walemavu!
 
Bahati mbaya kwake anatoa rushwa kwa kundi lisilopiga kura (wanafunzi), kwa wenye ulemavu hiyo ni sawa!!
 
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?

Alishasahau alipo waambia wana kigamboni wote kuwa hasiye kuwa na uwezo wa kulipia nauli ya kivuko APIGE MBIIZI?
 
ni upuuzi mtupu na ni rushwa, sasa kama ameanza ufisadi mapema kabla hata hajawa rais, je akiwa presdent si ndo baraa jingine litawakumba watz na hili litakuwa zaidi ya escrow: wanamtwara hatutadanganyik kura ni kwa EL tuuu
 
Duuuuuhhhh mambo juu ya mambo,ama kweli tunafanywa Mabwege ile mbaya.Hebu nikuombe kama unazo picha za uzinduzi uliofanywa na Mh. Hawa Ghasia tuwekee ili hawa wakubwa wajuwe na sisi tuna akili,siyo wao tu.Au Mh.Rais kapigwa changa la macho...

Ccm wote ni wasanii tu
 
Wanafunzii kataei kupanda bure mwambieni manataka kupiga mbizi.
 
Wanafunzi na walemavu wajitahidi kuitumia hiyo nafasi vizuri manake deadline yake ni october 25th kama ccm ikishinda..na wategemee huyohuyo aliyewaambia ni bure atakuja kuwaambia wapige mbizi..
 
Vivuko vyote ni bure kwa wanafunzi na walemavu
 
Magufuli ni mtendaji sana ila shida kina Kikwete ( familia) wanatamtumia kulinda maslahi ya kibisness.
 
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?

Magufuli yuko sahihi. Hawa wanafunzi sidhani kama wengi ni wapigakura. Kuwasaidia wanafunzi ni jambo la msingi. Kwa namna wanafunzi wanavyonyanyasika, ndivyo tunavyojenga Taifa la watu wenye chuki kwa Serikali. Ukiwaona watoto/wanafunzi wanavyoomba lifti wakati wa kwenda au kutoka shule, na namna wanavyoachwa; ni wazi utakubali kuwa kizazi cha aina hii lazima kiwe cha kulipiza kisasi. Mwanafunzi wa aina hiyo, siku akipata kazi ya umma hoja yake itakuwa: "Sikusaidiwa, kwa hiyo na mimi sina sababu ya kumsaidia mtu." "Taifa halikunilea, na kwa sababu hiyo siwezi kuwa na uchungu na Taifa." Tujitahidi kuwasaidia wanafunzi hawa ili baadaye wawe wazalendo kwa Taifa letu.
 
Pombe-11Agust2015.jpg

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

“Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu,” alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

“Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming’oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu” alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

CHhanzo: NIPASHE

Swali langu: Nakumbuka Magufuri alishawahi kuwambia wananchi wa Kigamboni kwamba asiye na hela ya kulipia pantoni apige mbizi.

Lakini hivi karibuni Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM ameagiza wanafunzi na walemavu wasafiri bure kwenye kivuko huko Mtwara, je hii sio rushwa ya kutaka kupata kura 25 oct?
sioni hoja yako hapa. kwani kasema watu wapande bure hata sasa? kasema wanafunzi na walemavu. mbona una akili ndoko kiasi hiki we nyumbu?
 
Back
Top Bottom