Magufuli: 2017 Mwaka wa Tanzania Mpya

Magufuli: 2017 Mwaka wa Tanzania Mpya

Maigizo yakizidi kuendelea. Hataki tena Watanzania tuishi kama mashetani? Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi vipi!? Ataacha matumizi ya trilioni za shilingu au zaidi ambayo matumizi hayo hayajaidhinishwa na Serikali? Kutohesimu katiba ya nchi vipi? Kuvuruga sheria za nchi ili tu awaweke watu rumande na huku akiwanyima dhamana pamoja na kesi zao walizombambikiwa kuruhusu dhamana vipi? Kutaka mashetani waifunge mitandao yote nchini vipi? Ataamuru Serikali ifute kesi dhidi ya Maxence Melo na Lema? Ataruhusu uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Watanzania kujadiliana mambo mbali mbali muhimu ya mustakabali wa nchi yetu bila vitisho na kuitwa wachochezi!?

Mwaka huu mpya 2017 utakua mwaka wa Tanzania mpya kwa wananchi wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John pombe Magufuli amewatakia Watanzania wote, wafanyakazi na wafanyabiashara wote
heri ya mwaka mpya wa amani na amesema utakua mwaka mzuri katika huduma mbalimbali na maboresho mbalimbali.

Chanzo: Mtanzania
 
ni za kupuuza tu tuendelee kufanya yetu
 
Apandishe madaraja aachie ajira aruhusu watu kuhama atoe nafasi kwa wanasiasa kufanya siasa.Adhibiti mianya ya rushwa atende haki bila kuangalia kabila wala chama mwaka 2017 utakuwa wa neema
Ndicho atakachofanya sab alishasema ajira na stahiki zake ni kabla ya mwaka wa fedha kuisha
 
Maigizo yakizidi kuendelea. Hataki tena Watanzania tuishi kama mashetani? Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi vipi!? Ataacha matumizi ya trilioni za shilingu au zaidi ambayo matumizi hayo hayajaidhinishwa na Serikali? Kutohesimu katiba ya nchi vipi? Kuvuruga sheria za nchi ili tu awaweke watu rumande na huku akiwanyima dhamana pamoja na kesi zao walizombambikiwa kuruhusu dhamana vipi? Kutaka mashetani waifunge mitandao yote nchini vipi? Ataamuru Serikali ifute kesi dhidi ya Maxence Melo na Lema? Ataruhusu uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Watanzania kujadiliana mambo mbali mbali muhimu ya mustakabali wa nchi yetu bila vitisho na kuitwa wachochezi!?
Anazuia dhamana kwani yeye mahakama? Unadhani aliyezuiliwa dhamana ni lema tu? Hiyo ni sheria ya nchi inamruhusu DPP kuzuia dhamana ya mtu yeyote bila kuulizwa.
 
Mikopo mbona inapatikana tu mradi utimize mashart ya mikopo
 
Anazuia dhamana kwa sababu yeye ni DIKTETA UCHWARA, Kesi ya Lema ina dhamana na kusema Magufuli atakufa ni ukweli na siyo siri na kutoa kauli kama hiyo hakuna sababu yoyote ya kufunguliwa mashtaka.

Anazuia dhamana kwani yeye mahakama? Unadhani aliyezuiliwa dhamana ni lema tu? Hiyo ni sheria ya nchi inamruhusu DPP kuzuia dhamana ya mtu yeyote bila kuulizwa.
 
Anazuia dhamana kwa sababu yeye ni DIKTETA UCHWARA, Kesi ya Lema ina dhamana na kusema Magufuli atakufa ni ukweli na siyo siri na kutoa kauli kama hiyo hakuna sababu yoyote ya kufunguliwa mashtaka.
Kila kitu kwenye kesi ya lema kinakwenda kisheria ndio maana hakuna mwanasheria wa lema au kutoka uongozi wa chadema anayelalamikia uwepo wa kesi bali wanapambana na DPP atoe zuio la dhamana ambalo lipo kisheria pia. Kosa la lema sio kumwambia rais atakufa kwa sab kila binadamu atakufa bali kosa la lema ni kumtajia mh rais siku ya kufa ambayo kisheria ni kosa ni sawa na kutishia kuua kwa maneno hiyo ndiyo kesi inayomkabili na hata lema mwenyewe anajua ni kosa ndio maana kwenye mahojiano kabla ya kukamatwa alisema siogopi hata ikibidi kufunguliwa kesi.
 
Ukishaona Rais haweki kipaumbele kwenye Elimu na walimu,kilimo na ufugaji,umeme maji na afya,madini na biashara ujue hamna jipya!
Elimu imedoda hasa sayansi na technolojia na maabara kazipotezea.pesa ya elimubure ingeboresha mashule kupata maabara,library na vyoo kwanza.
Kilimo na ufugaji, wanakimbizana wakulima na wafugaji huku wakitumia elimu duni,teknolojia dhaifu na ubahatishaji Wa mvua na lishe.
Umeme,maji na afya. Tanesco hawajielewi wanapoenda,maji Safi ni lulu hasa vijijini mabomba nitokaenzi za mkoloni na afya na matibabu ni kitendawili,hata chanjo kwawatoto inatushinda.
Madini na biashara, hakuna mabadiliko yoyote yamanufaa kwenye sekta ya madini yanayozidi kuisha Pia biashara zinaanguka na zinafanyika kiholela bila mifumo ya kuzitambua na kuzisaidia kukuwa ili tushindane kimataifa na tupate kodi.
Sasa sijui ni kwa miujiza gani tunaweza tarajia manufaahuko tuendako. Shame!!
Usisubiri miujiza hama nchi tu
 
Hakuna sheria yoyote ya kumfungulia mtu kesi kwa kutamka tu kwamba Rais atakufa. Lema angekuwa na kosa angetamka kwamba atamuua Rais lakini kusema Rais atakufa si kosa na wala si kutishia kuua.

Kila kitu kwenye kesi ya lema kinakwenda kisheria ndio maana hakuna mwanasheria wa lema au kutoka uongozi wa chadema anayelalamikia uwepo wa kesi bali wanapambana na DPP atoe zuio la dhamana ambalo lipo kisheria pia. Kosa la lema sio kumwambia rais atakufa kwa sab kila binadamu atakufa bali kosa la lema ni kumtajia mh rais siku ya kufa ambayo kisheria ni kosa ni sawa na kutishia kuua kwa maneno hiyo ndiyo kesi inayomkabili na hata lema mwenyewe anajua ni kosa ndio maana kwenye mahojiano kabla ya kukamatwa alisema siogopi hata ikibidi kufunguliwa kesi.
 
Hakuna sheria yoyote ya kumfungulia mtu kesi kwa kutamka tu kwamba Rais atakufa. Lema angekuwa na kosa angetamka kwamba atamuua Rais lakini kusema Rais atakufa si kosa na wala si kutishia kuua.
Ametaja siku ya kufa sio kusema atakufa. Kusema atakufa sio kosa kwa sababu kila mtu duniani atakufa infact kila kiumbe kitaonja mauti bali kumtajia mtu siku ya kufa ni sawa na kutishia kuua. Halafu ngoja nikurekebishe ulivyosema HAKUNA SHERIA YOYOTE YA KUMFIKISHA MAHAKAMANI KWA KOSA....... kwa kawaida kesi zote zinazopelekwa mahakamani kuanzia mahakama ya mwanzo mpk mahakama kuu lazima ziendane na sheria za kanuni ya adhabu za nchi na zina majina yake kwahiyo haiwezekani kwa namna yoyote kupeleka kesi mahakama yoyote ambayo haimo kwenye kanuni za adhabu haiwezekani kabisa hata wanabambikiziwa kesi wanapewa kesi ambazo zipo kwenye kanuni ya adhabu isipokuwa wanakuwa hawajafanya kosa husika kwa maana hiyo hakuna malalamiko ya lema kuonewa au kubambikiwa kesi kutoka kwa mawakili wake bali malalamiko yao ni zuio la dhamana kutoka kwa DPP ambalo ni la kisheria kabisa lkn linaweza kupingwa kwa kukatiwa rufaa mahakama kuu au mahakama ya rufaa ndicho kinachofanywa na mawakili wa lema kwa sasa . Nadhani hapo umepata darsa kidogo la kisheria kama una kitu kingine cha kisheria unataka kujua kuhusu kesi ya lema karibu.
 
Mungu naye yupo bize....Kuna watu ambao dhahiri ilibidi awachukue mapema wakadeki mabanda ya kuku huko mbinguni...kuwapa uongozi hapa duniani ni aibu,hata mungu mwenyewe anatushanhangaa!
Shubaaamit!
Lowassa ndiye anayefaa
 
Back
Top Bottom