Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Wiselady m'baya, ninasema hadharani,
Hatufai kwenye kaya, amekosa shukurani
Ameikosa hidaya, si mtu mwenye ubani

Na ukuu wa wilaya, haupati asilani
Atabaki anagwaya, hata aende shambani,
Hata aende Ulaya, atakuwa kisirani

Kabila yangu Mhaya, Bukoba napatamani,
Akipenda kuwa yaya, simpeleki nyumbani,
Atakuja sota waya, atoe jasho kwapani,

Wiselady ingia uwanjani,PJ anakutoa thamani
Utungo wako yakini, utamshinda wa kungwini
Ulotulia safiini, mistari iyosheheni
Hazina usiifiche. Wiselady jumuika......
 
Firstlady, Invisible, Mwanakijiji, Afrodenzi, Shosti, bujibuji, preta mpo wapi wajameni???????????????? leteni voco basi!
 
Aisee ngoja nikakariri mistari, nikujibu kishairi.

Kwa sasa wacha nikugongee senksi kwanza.

BRB!
 
Aisee ngoja nikakariri mistari, nikujibu kishairi.

Kwa sasa wacha nikugongee senksi kwanza.

BRB!


Mpwa unascandal kubwa! Kamera ya Salamanda imekumulika. Kwa kukufichia aibu inabidi utununulie ulabu kikao kitakuwa pale samaki samaki ukisiponya hivyo picha na mikanda vitarushwa JF News.
 
Nabofya kibodi yangu, salamu nazituma,
Kwenu marafiki zangu, natumai mu wazima,
Nawaombea kwa Mungu, mjaliwe yalo mema,

AfroDenzi, nakuzimia tangu MWANZONI,
Fikra zake ni huru, pia zina burudani,
Nami ninamshukuru, hachoki tangu zamani,

Yupo dadetu Festiledi, yeye hupenda MAISHA,
Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,
Thanks tele azipata, maana huelimisha,

Michelle yupo, hutaka TUJIELEWE,
Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,
Sifa zake zipo, muhimu apewe,

Mzee Mwanakijiji, MZEE WA CHANGAMOTO,
Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,
Habari hutupatia, yenye midundo mizito,

Kaa la moto Chochote unachoweza,hima weka mchangoni
Hilo ndilo unalowaza,tukakawa hatulioni
Ila sala memaliza,ndio ukatia udhu

Madela wa Madilu keri hazi ghasi, nyimbounawaimbia
Mwenye kukerwa huhisi, hujali humuingia
Hawi zimwi asikisi, ikawa bure tabia.

[SIZE=-1]Pakajimmy amejieneza,sifa zakejamvini, [/SIZE]
[SIZE=-1]Jambo analoliwaza, taarifa kuwapeni, [/SIZE]
[SIZE=-1]Si vizuri kunyamaza, bora awajulisheni, [/SIZE]

Kaiza kaka yetu sote, jitu liloshiba,
Mengi hutaka tuyapate, yale yaliyoshiba,
Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,

[SIZE=-1]Kuwa fundi si ajabu, hilo kwanza eleweni, [/SIZE]
[SIZE=-1]Kuwa fundi ni thawabu, aliyanena Manani, [/SIZE]
[SIZE=-1]Msijempa adhabu, kwa maswali ya kwa nini? [/SIZE]
[SIZE=-1]Drphone ameshasilimu, sasa naitwa FUNDI. [/SIZE]


Rose naye ni rafiki, hutumia DARUBINI,
Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,
Kwenye siasa na urafiki, hutujuza kulikoni,

Mwanajamvi Aspirin, hutuonesha MWANGAZA,
Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,
Kwa ushairi ni vema, post zake zapendeza,


Miss Judith huyo, ana UPANDE MWINGINE,
Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,
Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,

MwanajamiiOne pia, hutuambia AMKENI,
Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,
Daima hukumbushia, tutoke usingizini,

October mwenzetu, utujuzaye maisha,
Wewe ni darasa kwetu, maarifa yaso kwisha,
Wafunza juu ya utu, mengi watuelimisha.

Teamo bado kuchoka, upo kwenye msafara,
Ungali kwenye pilika, kwa zako huru fikra,
Nakuombea baraka, uzidi kuwa imara,

Nilham usiyechoka, asubuhi na jioni,
Nyumbani kuwajibika, halafu pia kazini,
Kisha huachi andika, kutujuza kulikoni,

Mwenzetu ni mwanaharakati, daima usiyechoka,
Wautumia wakati, pasipo yoyote shaka,
Maisha kuwa na chati, daraja la uhakika,

Inkoskaz Upo kwenye mapambano, ujenzi walo taifa,
Hujalala kama pono, wastahili nyingi sifa,
Washika yetu mikono, ili tuzizibe nyufa,

Kiraka mwendo ukaze, usiache harakati,
Mawazo uyaeleze, tena kwa kila wakati,
Ili nasi tujifunze, nawe uwe katikati,

Voiceofreason, mapenzi umeandika,
tangu siku za zamani,
Yale yaliyokufika, na yale ya majirani,
Na kwako alozimika,umesema ya moyoni,

Ndugu yetu Preta, kabobea kwa MAVAZI,
Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,
Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,

Fidel80 nayakumbuka, manenoyo jamvini,
Hakika niliridhika, nami nikakuamini,
Kwako hayakufichika, hata yale ya moyoni,
Hashima siku hizi hakuna labda zamani

Invisible tunamjua, mkuu wetu KIJIWENI,
Sheria apambanua, ili asitupige ban,
Sote tukajitambua, tujijue kina nani,


Mkuu Klorokwini, posti zake ni KITAMU,
Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,
Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,


Mkuu Kashaijabutenge,nakuheshim zamani na sasa,
Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,
Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,


Magulumangu mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,
Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,
Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,


Na Wiselady, siachi kumsifia,
Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,
Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,

Ndugu yangu Rutashunyuma, sitokuwacha nyuma
Posti zako nii ghali sio kama uji
Zinawakuna wa mbali mbaka Tabora na Ujiji

Mjomba Bujibuji, mwingi wa burudani
Posti zako adhimu, zinatupa burudani
Sina wakufanisha hata na mmoja humu ndani.

Nakumiss mzee wa malivdavi ulie kaburini
Baada ya posti mbili wadau wakakupa bani
Kifo chako historia ndo mana nakutilia ubani

Ewe nawe The Finest usinung'unike,
Tena uingie ndani nawe ufarijike,
Utuambie amkeni, wanajamvi tubadilike
Tushikane kwa imani wanajamvi tunusurike.

Wozawoza wewe mshari jahili,
Kama huoni dalili, kebehi si jambo kupigania,
Twatetea kwa ukali, siambe tunatania
Kiwa sio zetu sisi, dini hizi ni za nani?

JF Moderator1 huyu wa ajabu, wala hataki mchezo
Kuwatia watu adabu, bila kuleta mizozo
Katoa watu ububu kukumbatia kuozo
Lazima tumpe thanks, Wanajamvi tumfurahie.

JF Moderator2 huyu ni hodari, Mtauni humkani
SIHABA baba jasiri, wala hataki utani
Hakuna kutafakari, mwanajamvi si muhuni
Pongezi tumpe na jamvi kulifurahia.

Mwenzetu huyu si mgeni, Samora10 mwamjua
Mwenzetu si limbukeni, kusema anayoyajua
Samora10 hana utani, kwenye uovu hufichua,
Ni kijana muadilifu si kijana wakuchakachua.

Jaluo Nyeupe mwamjua, bilashaka mwamuona
Ni yeye tunaemjua, hakika yupo bayana
Haki huitetea, bila kubaguana
Jaluo Nyeupe ni rafiki hana kubaguana.

Na Lizzy na Husniyo msisite, ikawa tusionane
Wala tusijikokote, mlonayo muyanene
Mllipo mji wowote, mambo tuelimishane
Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie

Nyani Ngabu, Babaubaya, michango nileteeni
Ninyi ndugu pia, shime tujitokezeni
Muhimu ni zetu nia, na wala sio thamani

Lizzy fanya kuniandikia, wapi yako maskani
Ndipo nitapokwambia, mchango umpe nani
Na mimi tafatilia, nizitie kibwetani

Hongera niwatumie, Kibunango na Babu Atakasema sirisiri
Na duwa tuwaombee, Rabi awape kivuli
Mungu awazidishie, duniani na peponi

Masikini_Jeurina na Gurudumu hawa harambee, wapiga debe jamvini
Hawana ila ushee, imekuwa hamkani
Wamejifanya wazee, wao ndio makarani
Posti nyingi wanaandika hapa jamvini,

Muhogo mchungu kwa siri au dhahiri , atoae yujamvini
Uziitazo ghururi , mwenyewe amezibuni
Unenayo yafikiri, usijeitwa fatani

Mwaminifu thread ulozitunga,zitawafika wahunzi
Wale wasije kulonga,uloanza mwanafunzi
Wapita ukiwachonga,kwa vile una kurunzi

Ki Mey hutenda mengi ya dini, habanduki kanisani
na posti nyingi jamvini, hukaribisha na wageni
na ibada za nyumbani, hatutaki hata wageni.

Maxishimba uchunge mwenendo wako , wende mwendo wa kupima
Utunze twabiya zako , ujuwe baya na jema
Kama hujali wenzako , kutenda ya kuwauma
Ngoja nawe siku yako , utendwe bila huruma

Kakajambazi, yeye huyu si mwizi, na tena ye si jambazi
Kanilaghai kiujuzi, kwa jinale jamvini
Huyu yeye si jinamizi, akatuchuna na ngozi
Kakajambazi ni mwema mwenzetu jamvini.

Mawazo1109 ni wetu sote, hima tusaidiane
Wa mbele tuwafuate, haya tusioneane
Kwa hili natusitete, bali tusikilizane
Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie.


Nami MWAJAMVI MIMI, Mohammed Shossi
Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,
Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,


Ambao sijawataja, lipo shairi jingine,
Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,
Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,

Mkuu nimekukubali wewe mkali hats off! Easy na Wozoza
 
GT wake mdogodogo mwendo, wajulikana zamani
Mwendo usio vishindo, haufeli abadani
Asoweza huwa kando, awezae huwa ndani
 
Im speechless ndugu!
You rock! Muda uliotumia na akili uliyoweka kutoa utenzi huu si mchezo.Keep it up.

Na wewe umo pia

WomanOfSubstance
Na kama wapendelea, usitajwe hadharani
Kwa kuwa unahofia, mambo fulani fulani
Ninakuhakikishia, taweka siri moyoni
 
Na wewe umo pia

WomanOfSubstance
Na kama wapendelea, usitajwe hadharani
Kwa kuwa unahofia, mambo fulani fulani
Ninakuhakikishia, taweka siri moyoni

Bora iweke moyoni , hiyo siri mwana flani
Siri ibaki sirini, siyo tena hadharani
Hapo utaweza wini, ewe mtunzi makini
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom