Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,263
- 684
Kijana sasa nimekukumbuka anyway take from me vyovyote vile lakini kwenye ukweli nitausimamia...............
Tueshimiane we sho**** nani kakwambia mim kijana
Kijana sasa nimekukumbuka anyway take from me vyovyote vile lakini kwenye ukweli nitausimamia...............
Wewe ungefanya la busara ukaweka CV yako usimshusie hadhi ilhali wewe mwenyewe huna busara na ujumbe wako unadhihirisha hayo! Nina wasiwasi na elimu yako mkuu.................
Maggid na Shossi,
Tatizo la wengi humu JF ni kwamba ni wapenzi damu wa Chadema na kukiwa na criticism zenye kuwaumbua Chadema hun'gaka na kutoa maneno ya kejeli ili kumdiscredit yule aliyetoa mada aonekane mpuuzi. Hii ni dalili kuwa either mtoa hoja amewaambia ukweli au mna chuki na mtoa hoja. Sasa binafsi mtazamo ambao ni bias huwa siupendi maana huchangia kupelekea kwenye bias conclusion na wrong interpretation. Chadema nawaambia tena fikra za mwenyekiti zidumu ni mfumo hauna tofauti na CCM na hilo litapelekea chama kufa na kama sio kupotea kabisa. Ni vizuri mkajichunguza na kujipima kwani hata wale waliokuwa wanawaunga mkono kwa mbali hawatakuungeni mkono tena 2015. Waswahili hunena ukiumwa na nyoka hata nyasi zikitikisika mtu hukimbia vilevile mtu akisikia tena Chadema baada ya kuwachukia hatasikiliza hata hoja gani inazungumzwa. Sasa ushauri wangu kwenu wawili ni kwamba toeni hoja kwa misingi unayoitambua wewe ndio maana ya kuitwa msomi lazima uwe na misimamo unayoiamini. Kuna watakaokubaliana nayo na wengine kuipinga but mwisho wa siku ujumbe umefika.
Majid said:........Na changamoto za kisiasa hazikimbiwi, hukabiliwa kwenye majukwaa ya kisiasa. Wabunge wa CHADEMA hawakuwa na sababu za msingi za kutoka nje ya bunge. Badala yake, wangepambana kwa hoja ndani ya Bunge. CHADEMA si wanajua, kuwa hatma ya jambo lile lilikuwa ni kupigiwa kura. Kwamba wangeshindwa. Ni sehemu ya mapambano ya kisiasa
......Badala yake, wangepambana kwa hoja ndani ya Bunge. CHADEMA si wanajua, kuwa hatma ya jambo lile lilikuwa ni kupigiwa kura. Kwamba wangeshindwa. Ni sehemu ya mapambano ya kisiasa.
Makindi, yote uliyoyaandika ni UONGO MTUPU, umeyaandika bila chembe ya haya. Hata hivyo, naheshimu uhuru wako wa kujieleza. Umefika mahali unaandika kuwa nilitoa msimamo kuwa ni kwa nini nitampigia kura JK! Kama una ushahidi wa hilo uweke hapa hadharani, ukishindwa useme tu samahani kama una chembe za uungwana.
Niliyoyaandika ni maoni yangu. Niliandika nikijua nachochea mjadala na si wote watakaokubaliana nami. Ni kawaida, mie mpenzi wa Simba, kuna hata Simba wenzangu wanaonichukia.
Mwaka juzi kulikuwa na sakata la mchezaji Athumani Iddi kufungiwa na TFF kucheza soka kwa vile Simba hawakumpa kibali cha uhamisho. Simba walisema wako tayari kumwona Athumani Idi akiuza ndimu kuliko kumruhusu kurudi Yanga. Niliandika makala kwenye gazeti la Sayari kumtetea Athumani Iddi. Niliweka bayana kuwa, kuwa nilikuwa mpenzi wa Simba lakini kwa lile nilisimama upande wa Athumani Iddi.
Siku ile nilipigiwa simu nyingi na kutumiwa sms za WanaSimba wenzangu wenye hasira. Ikafika hata mmoja wa viongozi wa Simba alinipigia na kuniambia; " Maggid wewe si Simba mwenzetu, ni kondoo uliyevaa ngozi ya Simba!"
Na juzi usiku nimeshambuliwa vikali na Redio Imaan ya Morogoro. Nimeambiwa maneno mengi ikiwamo kuwa mimi mnafiki, mchochezi , na kuwa natumiwa kupambana na Waislamu. Kisa? Niliandika kwenye Raia Mwema kuwa redio hiyo inachochea uhasama kati ya Wakristo na Waislamu!
Tatizo langu ni kuandika mawazo yangu kwa uhuru. Ndio maana naamini, kuwa kuna CHADEMA wanonichukia, lakini kuna wanaonipenda pia. Hivyo hivyo kwa CCM, CUF, Waislamu, Wakristo na wengineo. Lakini naamini pia, kwa jinsi nilivyo, wote hao wanaweza pia kuniheshimu. Ni matumaini yangu.
Mkuu twende taratibu kidogo, kusema kwamba Majjid anaona kwa jicho la tatu ni kututukani sisi kwamba ni mambumbu hatuoni mbali, na unamweka Maggid kwenye hadhi ya umungu kwamba yeye hawezi kukosea, hapana mkuu wote humu tuna akili timamu na hatutompa mtu yeyote au niseme sitompa mtu yeyote nafasi ya kufikiri kwa niaba yangu. Maggid ni binadamu na huwa anakosea na ananunulika vilevile ushahidi upo japo hapa sio mahakamani na kama anabisha ajitoze sasa hivi kwenye hii thread nilimlipuwe sasa hivi
ONYO: KAMA UNAISHI NYUMBA YA VIOO USIMCHOKOZE KICHAA. TUMO HUMU KWA SURA MBALIMBALI. KARIBU MAGGID.