Kwa mtu yoyote yule kuna njia nyingi za kuonyesha kuwa jambo fulani hujaridhishwa nalo. Mwingine anaweza kupiga kelele, mwingine akalia n.k.
Mimi nafikiri Majid anaelewa yote haya lakini kuna kitu kinamfanya asiweze kusema ukweli. Ni masilahi binafsi au ushabiki. Mengi yameongelewa kuhusu suala la wapinzani kuunganisha nguvu n.k. Kuna mambo lazima tujiuulize nini kinaendelea sasa kwenye siasa za Tanzania?. Shida ya watanzania ni vyama kuungana? au kero kuondoka?. Kuna wakati kuna maswali najiuuliza muungano huu unaotakiwa ni kwa maslahi ya nani?. Inaniwia viguma sana kupata jibu kwa sababu matatizo ya Tanzania ni kuwa kuna misingi madhubuti imechezewa na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwenye jamii.
MA anaongoza maadam mambo yao wanayao yataka yametimizwa.
JE kuna faida yeyote kwa vyama vya siasa kuungana kwa mwananchi wa kawaida? J ibu ni kwamba hakuna, kama vyama hivyo kimoja au zaidi havikidhi haja ya wananchi.
Mimi nigependa kuongelea hoja ya CUF na CHADEMA kuungana bungeni huku sehemu zote za chini wakiwa pia ni mahisidi wa kisiasa. Katika mjadala huu TLP, NCCR haviongelewi sana kwa nini?
Nimemsikia Julius Mtatiro akiwashutumu vikali CDM kuwa ni kama masikini ameamka tajiri kwa hiyo amechanganyikiwa, nimemsikia Hamad rashid akijinadi kuwa yeye ni mkongwe wa siasa. Hizi hoja zote zina mchango wote kwa maisha ya kila siku ya mtanzania (mtanganyika)? . Nimeiweka mtanganyika kwa maana halisi nitakayo ieleza . Lakini nilimsikia bwana rashid akijaribu kutoa mfano eti wa mafanikio ya vyama vya Liberal na Conservative - Uingereza.
Kwa hali ya kawaida kama angejua shida wanayopata watu wa uingerza sasa nafikiri singetoa mfano huo, ni mfano mgumu hata waingereza unawapa shida kwa sababu vyama vikuungana wakati sera hazijaungana hapo ni shida kubwa.
Kimsingi vyama vya CUF, CCM, CDM ni vyama ambavyo vimesajiliwa kufanya siasa, na vote havijaona umuhimu wa kuungana na kuvivunja vingine miongoni mwao sasa muungano wa bungeni tu ni kwa maslahi ya nani?.Shida kubwa ya wanasiasa wetu ni kufikiri wako smart wakati hawajui hata wafanyalo, naa zaidi wanapojifikiria wao na kujiona bora.
Mimi nimefanya utafiti mdogo tu na kugudua kuwa kuna shida kubwa ya kiungozi chini kwani viongozi wengi wanafikiria temporary solutions za muda huo ili waweze kuongoza kwa kipindi kile bila kuangalia mbele.
Moja ya vitu ambavyo sijaelewa, ni hiki kitu kinaitwa serikari ya umoja wa kitaifa, kinachonifanya nisielewe ni kwa sababu mpaka sasa sijui kwamba Zanzibar inaongozwa kwa sera za CCM au CUF au sera mchanganyiko. Au serikali ya Zanzibar inaongozwa kwa kutumia busara za viongozi tu, Zaidi ya yote najiuliza kama sera mchanganyiko zikifanya vizuri kila mtu atafurahi na mimi nitafurahi. Lakini zikifanya vibaya hapa ndiyo kuna shida zaidi na unagundua tatizo lingine zaidi. Nani atalaumiwa? Ni CUF au CCM?, Jibu ni kwamba vyote viwili vinawajibika. Utamu utaongezeka zaidi vikifanya vizuri, kwani sijui itakuwaje tujagueni kama tulivyo au vipi?. Nimeandika haya kwa sababu hay ni miongoni mwa maswali magumu kwenye kila umoja yanajitokeza.
Ningeweza kusema na kuandika mengi lakini ninaomba wanajamvi muishia hapa na kuwapa swali la kuderive Equation ya yaliyotolea 1984 kwenye CCM na haya yanayotokea leo . Ni mategemeo yangu kuna picha unaweza kuipata bila chenga, wenye masikio na wasikiena wenye macho na waone.
Mwisho.
Hakuna faida yoyote kwa mtanzania wa kwaida kwa vyama vyovyote vya siasa kuungana , labda faida inayotakiwa ni ya viongozi tu.