Mageuzi makubwa CCM

Mageuzi makubwa CCM

Mahesabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2008
Posts
6,759
Reaction score
6,851
Tarehe22/12/2016,
Asubuhi saa2, Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole atakuwa Clouds Tv na Uhuru Fm akizungumzia mageuzi Makubwa Ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Usikose.
 
Jamani halahala tunaomba TOT msiibadlishe ktk hayo mageuzi yenu.... Mbele kwa mbele
 
UKAWA karibuni Mkodoe Macho TV zenu ukiwa ume Tune Clouds Tv, Mshuhudie Chama Kubwa CCM linavyoongozwa.
Karibuni sana UKIWA.
 
Usanii tu Mkuu. Chama kinachotoa rushwa kwa Wabunge wake ili wapitishe muswaada uchwara kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinadhani bado tuko kwenye mfumo wa chama kimoja na hivyo kutoiheshimu katiba ya nchi kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinapora bilioni 16 za wahanga wa tetemeko kamwe hakiwezi kubadilika. Chama kinachodai kwamba mahakama ya ufisadi kutokuwa na kesi ni ishara nzuri wakati kuna mafisadi chungu nzima ambao hawaguswi na mkono wa sheria kamwe hakiwezi kubadilika.

Mageuzi na CCM wapi na wapi?!
 
Mkuu kwa kweli hapo umemaliza kila kitu..!!
 
Tusubiri wakati ukweli tunaujua? Unakumbuka kulivua gamba iliishia wapi? Hakuna mageuzi ndani ya CCM zaidi ya danganya toto. Huwezi kufanya mageuzi huku umewakumbatia watoa rushwa, wapokea rushwa, wakwapuzi wa pesa za wahanga wa tetemeko, majangili na wahuni wengine mbali mbali. Angalia kuhusu mahakama ya mafisadi, baadhi ya Watanzania walioamini usanii wa kuhusu mahakama hii wakaamini huu usanii. Sasa tunaambiwa eti mahakama hiyo iko idle kwa sababu inakosa kesi za mafisadi!!!! Kweli mafisadi wote hawa wa Lugumi, Escrow, IPTL, boti uozo n.k. halafu mahakama inakaa idle!!! Kweli!? Acheni kutuzuga banaa na kutufanya wapumbavu wa kutupa.

Si msubiri??
 
Back
Top Bottom