Mageuzi hadi vijijini mpango wa Mungu-Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mageuzi hadi vijijini mpango wa Mungu-Mbowe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUNTEMEKE, May 18, 2011.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Na Tumaini Makene

  MWENYEKITI wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amesema kuwa kasi ya mabadiliko ya siasa za mageuzi hadi vijijini si
  matokeo ya nguvu za viongozi, bali ni mpango wa Mungu juu ya ukombozi wa wanyonge.

  Akionekana kuguswa na namna wananchi wanavyokiunga mkono CHADEMA katika harakati zake za kuuhamasisha umma wa Watanzania kutimiza wajibu, kudai haki na uwajibikaji wa viongozi katika suala zima la maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla, Bw. Mbowe alisema 'sifa hizi mkinipatia mimi au viongozi wenzangu mtakuwa mnatutwisha mzigo tu, hii ni kazi ya Watanzania wote...ni mpango wa Mungu.

  Bw. Mbowe ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliyasema hayo juzi na jana katika mkutano wa hadhara pamoja na mkutano wa ndani alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho wa mjini Njombe, katika mfululizo wa mikutano ya Operesheni Sangara na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

  "Unajua mpaka wakati mwingine unaogopa, unatishika...maana haiwezekani ghafla tu nchi nzima unaona wananchi wanakubali mabadiliko, wanahitaji ukombozi na mabadiliko kwa kasi ya ajabu ambayo haijawahi kuonekana... waanzilishi wa mageuzi kama Mzee Nyimbo (Thomas) wanajua ugumu tuliowahi kupambana nao huko nyuma, lakini sasa ni wazi Watanzania wanadai ukombozi.

  "Wananchi wanatuunga mkono kwa ari ya ajabu, demand (uhitaji) ya CHADEMA inakuwa kwa kasi mno, wananchi wako mbali katika kuhitaji mabadiliko kuliko hata ambavyo sisi viongozi tunafikiria...hawasikilizi tena propaganda zozote zile...ndiyo maana nasema huwezi kusema hii ni kazi yangu, wala ya viongozi wenzangu ni mpango wa Mungu.

  "Maana haiwezekani ghafla tu CCM wamegeuka kuwa wezi, wanaiba mchana kweupe mpaka kila mwananchi anajua...ghafla ufisadi unaogharimu maendeleo ya watu na nchi unafanyika kila mahali, mchana kweupe, serikali yao haijali, wananchi wanafahamu kwamba nchi yao na wao wenyewe walistahili maendeleo kutokana na rasrimali zao lakini zinaliwa na watu wachache," alisema Bw. Mbowe.

  Katika mikutano yake Jimbo la Njombe Kusini, CHADEMA kilibaini vitendo vya kifisadi, baada ya wananchi kupewa nafasi ya kueleza kero zinazokwamisha maendeleo jimboni humo, ambapo walitoa madai ya 'kutapeliwa' takribani sh. milioni 57 walizochangishwa kwa ajili ya mradi wa maji mwaka 2008 kwa ahadi ya kupata maji ndani ya miezi sita, lakini mpaka leo hakuna chochote na hawajui zilivyotumika.

  Wananchi hao, hususan wa Kijiji cha Lugenge walitoa malalamiko ya kwa viongozi wa CHADEMA, juu ya ubovu wa barabara inayoingia kijijini hapo lakini wamesikia mbunge wao, Bi. Anne Makinda (Spika wa Bunge) alijenga barabara mbili usiku ili wageni waliokuwa wakienda katika msiba wa mama yake, waweze kupita kwa uzuri, wakihoji bajeti hiyo imetoka wapi wakati wao 'hawaangaliwi' miaka yote wanayoteseka.

  Kwa upande wake, Bw. Nyimbo, alisema watu wa mkoa huo, sasa wamegundua kuwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hayatapatikana kupitia CCM kwani kimefikia ukomo wa uwezo wa kuwaongoza.

  Naye Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA kutoka Iringa Mjini, Bi. Chiku Abwao, alisema kuwa wao kama wabunge watachukua kero za wananchi hao na kuzifuatilia, kwani wamegundua kuwa wananchi wa jimbo hilo hawana mwakilishi tangu mbunge wao walipochaguliwa kuwa spika wa bunge.
   
 2. p

  pikadili Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata nyuki walisikiliza ukumbozi,kweli kazi ya Mungu,BABA MBINGU NA NCHI APEWE SAFA NA KUABUDIWA MILELE NA MILELE AMINA
   
 3. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Saa ya ukombozi ni sasa,hakuna awezae kupinga.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kasi hii Mukama sijui kama anaijua ila mwache kwanza ahutubie wanafunz huko Bunda then ataishia kuongea na wazee wa nyumba kumi ndipo aatajua CCM ni gamba gumu . Watanzania wana mateso mengi mno kuanzia haki zao had kula na kuugua.Hawana msada na walio wachagua akina Makinda wana angusha maghorofa Kijitonyama na wala si kijijini kwake . Sasa wameona mkombozi Chadema .
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kutambua kuwa kuna mchango wa Mungu katika harakati ni Hekima ya pekee.
  Imezoeleka kwa wanasiasa kulewa sifa badala ya kurudisha utukufu kwa Mtakatifu.
  As tunapoelekea "mpaka kieleweke" Mungu aendelee kuwa nasi.
   
 6. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Endeleeni tu na harakati kwani saa ya ukombozi imewadia, wanaifanya hii nchi kama mpira wa kona kiasi kwamba kila mtu anajichukulia mali kivyake.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  eeee sasa moto umewaka!! endeleeni kuwafungua wananchi,, to emanticipate themselves from mentally slaves ya kudhani upinzani ni machafuko kama ccm wanaviojaribu kuhadaaaaaa. mbombo gya kyala jiwukhe nkeni
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Hivi Mbowe anaongelea Mungu yupi hapo? Wengine hatuamini kama Yesu ni Mungu au mtoto wa Mungu! Asituletee udini hapa.
   
 9. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We wa wapi?
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tupoamoja makamanda
   
 11. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Maneno yako na jina lako la mwisho "foxy" vinashabihiana.
   
 12. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  acha kimbelembele ww alikuwa anaongelea mungu wa wapagani
   
 13. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  ww ndo mdini ,unajifanya unamjua mungu au huyo mungu wako wa majini anakuzingua watu wanahitaji ukombozi ,ni heri uchi wa mnyama kuliko wa akili yako faizafisi
   
 14. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  wewe elewa maandiko yesu sio mungu yesu ni yesu na mungu ni mmoja tuu hapa hajasema yesu kasema mungu na mungu ni mmoja tu kwa hata yesu humuomba mungu pia.
   
Loading...