Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 222
- 201
Idadi ya watu Duniani inatarajiwa kufikia watu bilioni 10 kufikia mwaka 2050,wakati nchini Tanzania idadi ya watu inatarajiwa kufikia 137 milioni.Idadi hii kubwa ya watu itahitaji chakula kingi ukilinganisha na chakula kinachozalishwa kwa sasa. Idadi kubwa ya watu inahitaji fursa za ajira pamoja na huduma zingine za msingi kama vile afya, elimu nakadhalika.Mwaka 1932 alipochaguliwa Franklin D. Roosevelt kuwa Raisi wa Marekani,kulikua na ukosefu wa ajira zipatazo 13,000,000 huku mabenki na huduma zingine wakifunga huduma.Katika siku mia moja za uongozi wake alikuja na wazo la kufufua uchumi kwa kushawishi bunge la marekani kuzipitia sheria za biashara na kilimo.Ni katika kipindi hiki kulianzishwa Mamlaka ya Bonde la Tenesse (Tenessee Valley Authority) (1).Kilimo na biashara ni maeneo muhimu sana ya kuongeza uchumi kwa nchi ambazo uchumi umeshuka.Rais Franklin alifanikiwa kwa kiwango cha juu kuongeza ajira pamoja na biashara kwa kubadili sera na kuanzisha maeneo mbalimbali ya kilimo.
Sera za Mh Rais Dr.Samia Suluhu Hassan za kufungua uchumi,kukipa kilimo nafasi yake zitatatua changamoto za ajira kwa vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa,zitaiweka Tanzania salama kwa kuwa na chakula kingi,na kuleta uchumi wa kati kwa idadi kubwa ya watu.
Tuendelee kumuunga mkono Mh Rais kwa nia yake njema ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.