Magereza ambayo Scorpion mtoboa macho anafaa apelekwe

Magereza ambayo Scorpion mtoboa macho anafaa apelekwe

Kama atafungwa miaka mingi bado ni hasara kwetu maana hatokua anatoka nje kwenda kulima au kupasua mawe atakuwa anacheza mpira tu ndani. Mimi napendekeza watuachie tu huku kitaani tutajua cha kumfanya nadhani tutatoa adhabu inayoendana naye.
Mbona mlishindwa kumuadhibu kipindi yupo uraiani?
 
Sheria zinasemaje? Tunataka utawala wa sheria na siyo kukurupuka na kulipiza visasi. Mafisadi wameua watu wangapi kwa kuiba mamilioni ambayo yangetumika kununulia madawa ambayo yangeokoa maelfu ya watu masikini? Mbona haya majizi hatujasema yanyongwe?

Kwa mawazo haya nakuombea kamwe usiwe rais wala mtu mwenye dhamana juu ya maisha ya wengine. Hufai!

Amani iwe nawe!.

Muandishi hajui kama tuna sheria kama hiyo anayoitaka,Umemuelewesha vyema.
 
Kifungo cha miaka 30 kina mtosha ni bora azidi kuishi sero angalau ashuhudie Tanzania ya viwanda
Aliyetobolewa macho hataona tena maishani sasa inatakiwa scorpion mtoboa macho nae akae magereza maisha yake yote yaliobaki hapa dunian
 
Laiti mm ningekuwa rais yule jamaa aliyemtoboa macho mwenzake ningeamuru anyongwe pale jangwani tena mchana kweupe bila pazia kila mwananchi ajionee

Mahakama ndo chombo cha kutoa haki kwa mjibu katiba yetu, raisi angeamuru vp wakati hasikilizi kesi? Au siku hizi ndo kazi ya raisi kufanya kila kitu? Raisi anayo nafasi ya kusaini kunyongwa kama mahakama imempata na hatia na ikamhukumu kifo,
Kutokujua ni tatizo sana.
 
wamsamehe makosa yake na kumleta tena uraiani tumuoneshe kwa nin kuiva kwa maharage ni mpka yaruke ruke mammae! namtan kinyama huyo **** aisee.
 
Habar wadau,
Nimetafakari kwa ukatili wa scorpion mtoboa macho aliokuwa nao napendekeza hukumu ikitoka huyu muuwaji nashauri apelekwe kwenye magereza yafuatayo:-

1.KITENGULE-KAGERA
2.ISANGA-DODOMA
3.RUKARANGA-KILIMANJARO
4.BUTIMBA-MWANZA
5.MAWENI-TANGA

NAWE MDAU ONGEZEA GEREZA LINALOMSTAHILI HUYU KATILI MTOA MACHO MUUWAJI.
NAWASILISHA
Yaani hayo ndio magereza ya kibishoo Tanzania, magereza mepesi yenye maisha ya raha, magereza hayo ndio mazuri kuliko yote.
 
apelekwe gereza la jahanam_.......teh teh tehh kaka scorpion mi natania tu usije ukanitafuta bureee!! mi sipendi kushitakiwa kwa kosa la kumuua mtu maarufu kama wewe kaka jambazi
 
Nawahurumia wafungwa....nahis nao atawatoboa macho hukohuko gerezani.
 
Mkuu hata me inanishangaza sana kuhusu huyu mtu, hata makosa aliyoshitakiwa nasikia ni unyang'anyi wa kutumia silaha, wala hakuna shitaka la kudhuru mwili, kujaribu kuua na kumsababishia kijana wa watu upofu wa kudumu... Na.... Na... Daah, inasikitisha kwakweli.

Ikiwa hakukutwa na silaha wala vitu vinavyosadikika alivipora si ni kumtoa dismiss mahakamani huko?
Hapo inabidi ujiulize!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom