Magereji - tegeta: Kuna tetesi za kuondolewa wafanyabiashara leo/kesho-kunani paleee!!?


D

dukebrain

Senior Member
Joined
Feb 19, 2013
Messages
113
Likes
0
Points
0
D

dukebrain

Senior Member
Joined Feb 19, 2013
113 0 0
Kwa wanaofuatilia maswala ya ardhi hasa kwa wilaya ya Kinondoni hususani eneo la Tegeta, watakumbuka Kanali Massawe (sasa mkuu wa mkoa wa Kagera) aliwahi kukimbizwa na wananchi alipotaka kuwahadaa watanganyika kuhusu eneo linalosemwa ni la kiwannda cha Cement (Twiga) ila kulikuwa na sintofahamu eneo likihusishwa pia na mgeni kutoka India akidai ni lake. Baada ya Kanali kukimbizwa na kuokolewa na wapambe wake na polisi eneo hilo lilitulia na watu wanaendesha biashara na pamejengwa vizuri tu na kuna watanzania wanaendeleza maisha yao kupitia eneo hilo ambalo kwa sasa linafahamika kama 'MAGEREJI' na limeendelezwa vizuri tu.

Hivi majuzi (last week) kumekuwa na wadodosaji kutoka vyombo vya usalama wakipita huku na kule kudodosa wananchi wamejiandaaje na tetesi za kutaka kuchukuliwa (tena) eneo hilo na wakati huu likiwa na mmiliki mwingine tofauti na muhindi na/au Twiga cement. Inasemekana leo au kesho itatoka STOP ORDER ili kuwataarifu wakazi wa eneo hli kuacha kuendesha shughuli yoyte ndani eneo husika na ulinzi mkali utatolewa ili kupambana na yeyote atakaye kaidi amri hiyo.

My take: Eneo lenyewe ni eneo muruwa kwa biashara ya aina yoyote na liko sehemu nyeti na kwa historia hiyo hapo juu inaonekana anayelitaka halali analiwaza na sasa anataka kuonyesha kuwa ana uwezo wa kulichukua kwa udi na uvumba. Angalizo ni kwa wakazi wa Tegeta, Boko, Bunju na wote wanaotumia njia ya Bagamoyo hasa baada ya daraja la Tegeta kuelekea maeneo tajwa kuwa makini hasa kwa kuangalia vyombo vya habari mchana wa leo na kesho na kupata taarifa kutoka vyanzo husika hasa watu wanaowafahamu waliopo maeneo ya tegeta kujua hali ilivyo na yanayosemwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Messages
3,846
Likes
57
Points
145
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2010
3,846 57 145
Hii serikali bana wakomae mpaka tupate utawala mpya ili mambo yawe sawa
 

Forum statistics

Threads 1,274,693
Members 490,736
Posts 30,521,144