Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 12, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia idara ya Maelezo leo inatarajiwa kutoa tamko kuhusu mwelekeo wa uandishi wa vyombo vya habari kufuatia malumbano na migongano ya maneno yenye kuashiria kuvunjika kwa maadili ya kiundishi hususan kuingilia habari za kibinafsi za maisha ya watu jambo ambalo linaonekana kuanza kuwakera viongozi mbalimbali. Pamoja na serikali baraza la vyombo vya habari nchini (MCT) nalo linatarajiwa kutoa tamko katika kile kinachoonekana kuitikia wito wa mmiliki wa vyombo vya IPP aliotoa juzi kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu madai ya kuzushiwa habari mbalimbali za uongo.

  Matamshi hayo ambayo yanatarajiwa kutolewa muda si mrefu ujao yanatarajiwa kutoa maangalizo kuhusu haja ya vyombo vya habari kuheshimu uhuru wa watu na maadili ya jamii yetu.

  Msimamo wa KLHN ni kuwa uamuzi huo wa kutoa matamko umechelewa na inaonekana unakuja baada ya moto wa malumbano hayo kuanza kuunguza pabaya. Siku za hivi karibuni magazeti mbalimbali ambayo yanadaiwa kuwa na watu wakubwa nyuma yake yamekuwa yakitumika kurushiana madongo, kashfa, uzushi na madai ambayo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ataona kuwa yana walakini.

  Kwa muda mrefu tumeandika na kupiga kelele kuhusu suala hili na hata katika kijarida chetu cha Cheche tumelitolea maoni jambo hili tena. Tunasikitishwa kuwa kwa muda mrefu serikali imekaa kimya ikiangalia na kukodolewa uchafuzi wa hewa ya habari nchini ambapo watu wachache wenye nguvu za kisiasa na kiuchumi wamewageuza watanzania kuwa vikaragosi vyao kwa kuwatupia kila aina ya habari huko wao wenyewe wakitengeneza mamilioni ya fedha. Tunasikitika kuwa kwa muda mrefu baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kinyume na kundi moja huku vikiamini kuwa vina kinga na baraka ya watawala.

  Licha ya kutambua mabadiliko yaliyotokea siku chache zilizopita ambapo vyombo vingine vimeibuka kuanza kujibu mapigo, tunasikitika kuwa kuna watu wameona kuwa jambo hilo ni la lazima baada ya serikali kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuchukua hatua. Wakati serikali haikuweza kuvumilia mara tatu suala la MwanaHalisi na habari ya kumng'oa Rais Kikwete, kwenye masuala haya ya vitandani mwa watu na kwenye vyumba vya watu yamevumiliwa kwa muda mrefu kana kwamba hakuna utawala wa sheria nchini.

  Wito wetu leo siyo tu kwenye masuala haya ya watu binafsi wanaogombana kupitia vyombo vya habari bali pia vyombo vile ambavyo vinatumika kutangaza habari za kingono na mambo ya ufuska kama kwa kuyatukuza huku vikiweka picha mbalimbali ambazo ni wazi zinavunja kanuni za Adhabu na sheria mbalimbal zinazohusiana na masuala ya uchapishaji, utangazaji n.k

  Haitoshi kwa serikali leo kutoa matamko ya kumuonya mtu au kukemea, tunachotarajia ni kuona serikali ikichukua hatua madhubuti ya kufungia vyombo vyote vya habari ambavyo vimevuka mpaka wa maoni huru na kuwa katika eneo la kukashfiana na kuharibu maadili ya watoto (deliquency of minors). Tunatumaini kama serikali inaona kuwa mambo yanayofanywa ni sehemu ya uhuru wa maoni au habari, basi wakati umefika kwa serikali kuanzisha sera na hatimaye sera itakayoratibu habari za kingono, filamu, na vitu kama hivyo kwa watu wazima ili vipatikane katika mazingira yanayotakiwa, vikiratibiwa na kusimaiwa kisheria kuliko ilivyo sasa ambapo badala ya kuita kuwa ni mambo ya kingono (pornography) tumeamua kuvipatia jina la "udaku".

  Hata katika nchi ambazo wengi wetu tunaonekana kuziiga mambo ya kingono yanaongozwa na sheria sawia na majarida au magazeti yenye habari za namna hiyo hayapatikana kiurahisi au waziwazi kama ilivyo nchini. Tunarajia serikali itahakikisha kuwa watu wazima wanapata uhuru wa kuona na kusoma kile wanachotaka kwa mujibu wa sheria na ya kuwa watoto wetu na public square or airwaves haviharibiwi kwa kuacha kundi la watu wachache kutawala hadi kwenye macho na masikio yetu.

  Tunachotarajia leo siyo maneno matupu, bali hatua kali na za mfano, ili hatimaye kwa kutumia sheria kulazimisha kina cha uandishi, habari za kuvutia, na maadili yanazingatiwa katika fani hii. Vinginevyo, kama wanachotaka ni kukemea "tabia iliyojitokeza" tumeona kuwa sisi tutanguliwe kuwakemea kwa uzembe na kufumbia macho uposhaji mkubwa wa maadili.
   
  Last edited by a moderator: Feb 13, 2009
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji: I don't want to sound cynical but that is what I am about to write will sound like: Newspapers like other commodities is demnad and supply. Kama watanzania tunapenda kusoma malumbano ya wakubwa au kuangalia picha za ngono na ufuska, wacha tuendelee kuangalia, why? Because unapokataza ndo inazidi kuwa object of desire. Mi nadhani censorship imepitwa na wakati, kama watu wasingenunua magazeti haya wasingeyachapisha.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wizara na maelezo waache uwoga, wachukue hatua kwa mujibu wa sheria
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mimi naona wananchi wayaysusie tu...kigazeti kama kile sema usikike kipo kuharibu na kuchochea uhasama baina ya watu kwa kulipa kisasi...Mmiliki wake R.Mengi ndio mhariri,mwandishi,msambazaji na kila kitu........
  ......mimi naona waayache yatajifia taratibu.......kama kuanza kufungia waanze na mauchafu ya shigongo.....
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tusipojua undani wa watu wetu vizuri ndio tunaishia kuchagua VIONGOZI wabovu, wala rushwa, mafisadi, ... Acha magazeti yaandike tuwafahamu kuanzia vitandani, vyumbani, sebuleni, mtaani,....Tumekuwa tukiangalia mazuri yao tuuuu mpaka basi.
   
 6. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaforum,

  Hivi tumejiuliza kwamba hili tamko linaigusa na JF? Kwa mtizamo wangu mimi, JF ni chombo cha habari tena kilichotukuka. Nauliza hivi kwa maana kuna wanachama huku ndani ya forum wako mstari wa mbele kuwakashifu (tena bila ushahidi) viongozi mbalimbali wa kisiasa na kijamii. JF imekuwa ni sehemu ambayo mtu akibandikwa jina lake tu, basi ujue kuna wachache watakuja na mazuri, na kuna wengi watakuja na kashfa zisizo na kichwa wala miguu. Watu wengi sana wamepakwa matope kupitia JF.

  Kwa mantiki hiyo basi, habari za kukashifiana ndio zinamake news miongoni mwa Watanzania wengi. Kila habari ili iwe habari lazima iambatane na kashfa kidogo. Lakini labda tujiulize, nini maana ya neno kashfa? Je, kusema flani ni jambazi ni kashfa? Jibu laweza kuwa ndio au hapana. Jibu linakuwa ndio kama kweli flani amekamatwa akiwa anaiba. Kama hatuna ushahidi juu ya wizi huu, basi ni kashfa kusema flani ni jambazi. Kwa wana JF wote, tuache kashfa. Tukitoa habari za mtu, basi ziendane na ushahidi uliotukuka ili habari yenyewe isiwe kashfa.

  Tukirudi kwa bwana Mengi. We do not have to sympathize with him kama yale anayokashifiwa hata sisi hatujui kama ni kweli au uongo. Kwa mfano, kuna picha zilisambazwa kwenye internet over the past few weeks zikionyesha kile kinachoitwa "ndoa ya Mengi na Lilian". Hapa kuna mawili. Inawezekana picha sio za kweli. Na inawezekana picha ni za kweli. Ni juu yako kuchunguza na kujua lipi ni sahihi. Baada ya hapo ndio unaweza kusema for sure kwamba Mengi anakashifiwa ama la.

  Mwisho ni kwa Wizara husika (habari) na MCT. Je, ni mpaka Mengi alalamike ndio watu wakumbuke kazi zao?
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Cant agree with you more
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Susuviri, kama bidhaa nyingine au huduma habari nayo ni bidhaa inayotakiwa kuwa regulated. The market forces of demand and supply if unchecked might be a fuel to launch certain businesses ambazo hatuwezi kuzisema. Kwa vile kuna demand na supply ya kitu fulani haina maana tusiregulate kitu hicho. Watu wanapenda habari za kingono, umbeya na hata kuangalia mapicha ya kingono.. so we shouldn't we regulate them?
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Mkuchika aja juu "nawapa siku 7!"


  Thursday, 12 February 2009
  Kama tulivyodokeza leo kuwa serikali inatarajiwa kutoa tamko na kuchukua hatua za kudhibiti vyombo vya habari, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Kapt. George Mkuchika ametoa siku saba kwa wamiliki na vyombo vya habari vitatu kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua baada ya vyombo hivyo kuonekana vinaandika habari ambazo zinaendeleza malumbano binafsi. Kama tulivyodokeza katika tahariri yetu hiyo na maoni ya DaJessy kwenye kijarida ukipendacho cha Cheche, haitoshi kuvishughulikia vyombo hivi tu bali kusafisha kabisa sekta ya habari na matumizi ya vyombo vya habari nchini.
  Pichani, Kapt. Mkuchika akitolea mfano mojawapo ya habari zilizotoka kwenye gazeti la Taifa letu.

  Kwa mujibu wa tovuti ya Michuzi:

  Magazeti ya Taifa Tanzania, Taifa Letu na Sema Usikike yamepewa siku saba yajieleze kwa nini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuandika habari za kukashifiana, uzushi, uchochezi na uongo. Na yametakiwa kuwa yamefanya hivyo ifikapo Februari 19 mwaka huu saa 10 jioni.

  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, amesema hayo leo alipokuwa akitoa tamko la Serikali kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari nchini.
  Amesema Serikali imesikitishwa na mwenendo wa magazeti hayo na hairidhiki na mwenendo huo, kwani yanakiuka Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo alisistiza kuwa itaendelea kutumika hadi itungwe nyingine.
  Akifafanua, Mkuchika alitolea mfano wa Taifa Tanzania toleo la Februari 6-12 mwaka huu, lililomshambulia Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa kuandika kuwa harusi yake imezua utata na la Taifa Letu la Februari 9 mwaka huu, lililoandika kuwa Karamagi (Nazir) anadaiwa kudandia wake za vigogo wenzake.

  Pia Waziri alizungumzia Sema Usikike toleo la Februari 10 mwaka huu lililoandika kuwa Waziri "Mkuu wa zamani amweka kimada shoga...".

  Kutokana na hali hiyo, Waziri aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kutumia vyombo vyao kwa maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu.

  Pia aliwataka wahariri wa habari kuacha kuandika na kushabikia habari za watu binafsi ambazo hazina maslahi kwa Taifa.

  Waziri aliwataka wamiliki na wahariri hao kuzingatia kifungu cha 30(1)(2) cha Katiba ya nchi kisemacho: "...kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma, haviathiriwi na matumizi mabaya ya Uhuru na Haki za Watu Binafsi."
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Mkuchika aja juu "nawapa siku 7!"


  Thursday, 12 February 2009
  Kama tulivyodokeza leo kuwa serikali inatarajiwa kutoa tamko na kuchukua hatua za kudhibiti vyombo vya habari, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Kapt. George Mkuchika ametoa siku saba kwa wamiliki na vyombo vya habari vitatu kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua baada ya vyombo hivyo kuonekana vinaandika habari ambazo zinaendeleza malumbano binafsi. Kama tulivyodokeza katika tahariri yetu hiyo na maoni ya DaJessy kwenye kijarida ukipendacho cha Cheche, haitoshi kuvishughulikia vyombo hivi tu bali kusafisha kabisa sekta ya habari na matumizi ya vyombo vya habari nchini.
  Pichani, Kapt. Mkuchika akitolea mfano mojawapo ya habari zilizotoka kwenye gazeti la Taifa letu.

  Kwa mujibu wa tovuti ya Michuzi:

  Magazeti ya Taifa Tanzania, Taifa Letu na Sema Usikike yamepewa siku saba yajieleze kwa nini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuandika habari za kukashifiana, uzushi, uchochezi na uongo. Na yametakiwa kuwa yamefanya hivyo ifikapo Februari 19 mwaka huu saa 10 jioni.

  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, amesema hayo leo alipokuwa akitoa tamko la Serikali kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari nchini.
  Amesema Serikali imesikitishwa na mwenendo wa magazeti hayo na hairidhiki na mwenendo huo, kwani yanakiuka Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo alisistiza kuwa itaendelea kutumika hadi itungwe nyingine.
  Akifafanua, Mkuchika alitolea mfano wa Taifa Tanzania toleo la Februari 6-12 mwaka huu, lililomshambulia Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa kuandika kuwa harusi yake imezua utata na la Taifa Letu la Februari 9 mwaka huu, lililoandika kuwa Karamagi (Nazir) anadaiwa kudandia wake za vigogo wenzake.

  Pia Waziri alizungumzia Sema Usikike toleo la Februari 10 mwaka huu lililoandika kuwa Waziri "Mkuu wa zamani amweka kimada shoga...".

  Kutokana na hali hiyo, Waziri aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kutumia vyombo vyao kwa maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu.

  Pia aliwataka wahariri wa habari kuacha kuandika na kushabikia habari za watu binafsi ambazo hazina maslahi kwa Taifa.

  Waziri aliwataka wamiliki na wahariri hao kuzingatia kifungu cha 30(1)(2) cha Katiba ya nchi kisemacho: "...kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma, haviathiriwi na matumizi mabaya ya Uhuru na Haki za Watu Binafsi."
   
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #11
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Hiki ni kichekesho cha mwaka!

  Mimi nilimwona jamaa huyu kuwa mtu wa maana, pale alipowaweka benchi MwanaHalisi kwa siku 90. Sasa anakurupuka kusema kwamba kuna magazeti yanayowachafua watu kwa makusudi! Upuuzi!

  Tuangalie ni uchafuzi gani huu unaolalamikiwa?

  Wote mmeona zile picha zake Mengi na kimwana, kuhusu ndoa yenye utata mwingi. Kama si ndoa, alikuwa anafanya nini na binti wa watu? Viulizo na vishangao vitawale!

  Haya, ni picha, tena za kawaida. Hakutaka "uhuru wake wa faragha" uingiliwe?

  Mbona akina Kanumba, Vincent Jogosi, Blandina Chengula (Johari), Ndumbagwe Misayo (Thea), Nurdin (Chekibudi), na wengineo... ohooo, Norah ndio kabisaa, picha zake za utupu zilichapishwa na kugombewa kama mpira wa kona!

  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo alikuwa wapi siku zote, asilalamike wala kutoa amri kali, wakati vijana hawa, ndugu zangu, walipokashifiwa, leo hii anakurupuka na kuanza kutoa amri ya siku 21, kwamba wamiliki hao wa magazeti wajitetee, la sivyo, wafungiwe magazeti yao.

  Mengi mwenyewe alikuwa na gazeti lake la "Acha Umbea" ambalo nalo limechangia sana kuwachafua watu wengi. Hili la "Taifa Letu" si la Mengi hili?

  Tumwelewe vipi huyu Mkuchika? Yaani Tanzania tuna double standards, ukiwa msanii tu, akina Shigongo na wenzake wakakuandika uongo, wakakuchafua, basi, hujaingiliwa uhuru wako wa faragha, lakini akiandikwa Mengi, inakuwa noma?

  Mimi nasema hapana, hapa haki lazima itendeke. Nitawaandikia hawa wenye haya magazeti, watoe tamko la pamoja, Waziri achukue hatua yoyote aitakayo, kwani huu ni UNAFIKI!

  Maadili ya Kitaifa yalikiukwa, picha za Norah zilipochapishwa, tena za utupu! Leo zimechapishwa za Mengi, ndoa ya siri, tena siri sana, ndio Serikali ije kuu? Kwani Mengi ni NANI haswa?

  Nimesema HAPANA! Huu ni unafiki, si uzalendo! Sheria inapaswa kuwasimamia Watanzania wote! Kama ni suala la sheria, basi hata hao waliochapisha picha za Norah wawajibishwe!

  ./mwana wa haki
   
 12. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Udaku wa aina hii mbona tumeuzoea? au kwa vile Mzee Mengi kalalamika? Huyu waziri naona kapewa maagizo azungumzie habari hizi na hakuwa amefanya maandalizi akashia kujikanyagakanyaga.
   
 13. t

  tk JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani huyu ndugu Waziri Mkuchika bado hajajifunza. Kutokana na kukurupuka kwake kufungia Mwanahalisi akajikuta naye kafungiwa kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa kipindi hicho hicho alichokifungia Mwana Halisi.

  Tatizo la hivi sasa ni kuwa maandiko ya watu binafsi katika magazeti, hasa madogo madogo, yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miaka miwili sasa bila serikali kuingilia. Leo kuandikwa Mengi, Mawaziri na Wabunge imekuwa issue kubwa. Hapa Mkuchika hayuko peke yake. Hata Spika wa Bunge naye kaingilia. Muda wote huu walikuwa wapi wakina akina Amina Chifupa (Marehemu) na Zitto Kanbwe walipokuwa wakiandikwa?

  Mkuchika (pamoja na Spika) lazima wajifunze kuwa utatuzi wa mambo haya ni wale walioandikwa wakiona wameongopewa waende mahakamani. Huu ndio uhuru wa utoaji habari.
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Wacha nicheke tu, ndio mawaziri wetu na hii ndio nchi yetu!! Nikiamua kulia si nitalia mwaka mzima? ngoja nicheke tu, siku nyingine nikiwaambia wenzangu tunapopiga kura tunaweka rehani maisha yetu labda watanielewa.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Inaonekana watu mmekosa point inayoendelea.. Waziri kachukua hatua si kwa sababu Mengi kalalamika.. ni kwa sababu Karamagi na "Waziri Mkuu" wa zamani wameandikwa vibaya. Na kwa sababu muendelezo huo wa kuwagusa wakuu ndani ya serikali ulikuwa uendelee kesho na wiki ijayo. Wakati huo huo magazeti ya kina KALIKARO yamepanga kujibu mapigo na hivyo kuendelea kuchafuana.

  So, Mkuchika ameact for "Mkuki ulipoelekezwa kwa binadamu".
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Heshima Mbele,

  Ningependa kujua ni nani mmiliki wa haya magazeti matatu.

  1.Taifa Tanzania
  2.Taifa Letu
  3.Sema Usikike

  Asante.


   
 17. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  My understanding:
  1. Taifa Tanzania- Karamagi
  2. Taifa Letu - Mengi
  3. Sema usikike - Mengi
   
 18. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Nani namiliki haya magazeti Taifa Tanzania, Taifa Letu na Sema Usikike..

  Just curious!
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,068
  Trophy Points: 280
  kumbe ni vita vya mengi na mzee ya pesa mingi karamagi.
  Sasa ndo nimeelewa...
  Je kuna conflict of interest kati ya hawa mabwana wawili?
  Je ni zipi hizo??
  Mwenye nyeti tunaomba atumwagie.
  Pia hawa jamaa wana shea tabia za kupenda sana mabibi
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Taifa letu na sema usikike ni mali ya ippmedia hayo mengine sina uhakika nayo kwa sababu hawajajiweka wazi ila jana kuna chapisho lingine la gazeti jipya linaitwa tanga yetu hili linatoka tanga
   
Loading...