Magazeti ya Shigongo yatuombe radhi Watanzania tuliobarikiwa kuwa na akili kubwa na za maono

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,556
108,897
Tunapokuwa tunakuja humu Jamvini ( JamiiForums ) na kutoa mawazo yetu ya ' Kitaalam ' kabisa ambayo huwa hayalengi ' ushabiki ' wa upande wowote ule bali huwa tunasimamia ' uhalisia ' katika kutokana na kubobea Kwetu katika kufuatilia mambo ya dunia muwe mnatuelewa.

Kwa takribani nusu mwaka sasa kama hata siyo mwaka kamili Magazeti pendwa ya ' Udaku ' yanayomilikiwa na Mtu ' mjanja mjanja ' Erick Shigongo ya Kiu, Ijumaa na mengineyo yamekuwa yakija na taarifa za Kuizihaki nchi ya Marekani kwa kuipendelea nchi ya Korea ya Kaskazini ( DPRK ) huku kila mara wakisema kuwa Marekani itapigwa na mara nyingine waliandika Marekani ' ndembendembe ' na mengineyo mengi tu.

Kila siku nimekuwa nikisema kuwa kwa sasa hakuna nchi yoyote duniani ambayo ' Kijeshi ' inaweza ikapambana au hata tu kuitisha Marekani na kama zipo basi jua tu ya kwamba inachokifanya hizo nchi ni Kujambisha tu / Kupiga Mkwara ila kiukweli hata wenyewe wanajua kuwa ' mziki ' wa Marekani hawauwezi na hauwezekaniki.

Hatimaye sasa Yule Yule Mtu ambaye alikuwa ni Kipenzi cha Magazeti ya Shigongo na waliyekuwa wakimtumia kama ' Nguzo ' yao Kuu ya Kibiashara hasa baada ya kugundua Udhaifu mkubwa wa Watanzania wengi katika kufuatilia mambo ya Kimataifa Kiongozi wa Korea Kaskazini amesalimi amri kwa Marekani na sasa ameomba kuonana na Rais wa Marekani mwezi May ili afanye nae mazungumzo ya kumuomba ' Msamaha / Radhi ' kwa yote aliyokuwa akiyasema na mikwara yake mbuzi kwa Marekani.

Hivi kama Mataifa yanayosifika kwa Vita Urusi na Iran na yenyewe yameufyata kwa Marekani huyo ' Mpuuzi ' wa Korea Kaskazini angeweza kufanya lolote kwa Marekani? Ama hakika hatua hii ya Kiongozi wa Korea Kaskazini kuomba ' po ' kwa Marekani imemuumbua mno Shigongo na Magazeti yake ya ' Udaku ' na sasa sijui kuanzia siku zijazo watakuwa wanakuja na taarifa gani kwani walikuwa wakiitumia mno ' mikwara ' mbuzi ya Kiongozi wa Korea Kaskazini ili wauze Magazeti yao.

Ni vyema sasa na Wao ( Magazeti ya Shigongo ) watuombe radhi upesi kama siyo haraka akina siye tuliobarikiwa akili na maono kwani ni mapema sana tulijua kuwa Korea Kaskazini kuna mahala tu tena padogo ' watategwa ' na Marekani na watapaingia na kweli wamepaingia na sasa wanajuta na wanahaha kuwalamba miguu Marekani.

Marekani haina ' Mbabe ' duniani.

Nawasilisha.
 
waache na kukopi story za JF na kuweka kwenye magazeti yao, bila kutaja chanzo cha hizo habari, huwa wanaandika na mwandishi wetu....

Niliwadharau Kitambo sana Mkuu na kuna Siku moja nilianzisha humu humu Uzi wa Kuwasema kwamba waache kila mara kuja na machapisho yao ya Vitisho na Kiuchochezi dhidi ya Marekani huku muda mwingi na nadhani hata sasa 99.9% ya ' machapisho ' yao ni ya Kuibeba na Kuisifia Korea Kaskazini huku wakiinanga / wakiisiliba kwa nguvu zao zote Marekani. Na hii ndiyo hasara ya kuwa na Media Outlet halafu haina Waandishi ' Wachambuzi Wabobezi ' ambao wangeweza kuwasaidia sana katika kufanya ' analysis ' ya hii ' diplomatic row ' iliyokuwepo kati ya DPRK na US.
 
Asante Genta kwa concern yako, wengine tulilisema hili mapema lakini kwa vile serikali inachagua yupi hayuko upande wao walikaa kimya. Habari kwenye magazeti ya Shigongo zilikuwa ni uchochezi kamili na ufitinishaji kati ya Tanzania na USA, na sikushangaa walipotishia kutuwekea vikwazo ingawaje sababu walizotoa ni tofauti. Ni Shigongo na wadhabiki wake maandazi humu kina YEHODAYA and the like waliokuwa wakianzisha nyuzi za kumsifu waliyemwita "KIDUKU" lakini baada ya kuufyata wamepotea. Aibu yao.
 
Hebu acha ukilaza

Kim alikuwa anajaribisha makombora yake ya masafa marefu ,hydrogen bomb na zaidi ya mara kibao alikuwa anayarusha licha ya kuzuiliwa na vitisho kedekede za Trump

Juzi tu hapo alirusha kombora lililopita anga la Japan na kutua kisiwa karibu na US kiufasaha na akarusha lingine lililofanikiwa 100% hapo Kiduku kajiridhisha makombora yake yapo accurate 100% ya masafa marefu ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya nucleur sasa anasema nipo tayari kwa meza ya mazungumzo

Ukiwa na akili za kimbayuwayu utasema kaomba Poo

Ila baada ya mission kumaliza na uhakika 100% na nuckeur ,makombora yapo kwenye ghala yenye uhakika 100% baada ya kufanya test ..kakubali meza ya makubaliano

Hapa sisi wataalamu tunasema

Kim=10
Trump=1
 
Back
Top Bottom