Magazeti kutoa taarifa za uongo/uzushi!!

sir echa

Member
May 28, 2010
85
3
Hellow!

Mara kadhaa kumekuwa na taarifa ambazo zinachapishwa kwenye magazeti yetu ambazo aidha ni za uongo au zimepotoshwa ukweli,naomba wadau mnisaidie hivi taratibu/kanuni/sheria zinasemaje kuhusu magazeti ya namna hiyo?
 
Toa mfano wa upotoshaji !

Ok Sir,
Gazeti la Risasi 9th july 2011,lilikuwa na habari "BIBI KIZEE AFUMANIWA NA MUME WA MTU" then the same gazeti tarehe 12th july 2011 likatoa taarifa"KUMBE BIBI KIZEE ALIYEFUMANIWA NI MLOKOLE"sasa ukisoma taarifa hii ya pili inaonesha kuwa taarifa ya kwanza haina ukweli na muandishi hakuwepo eneo la tukio bali alipelekewa picha na stori aiendike...
kwa upande wangu naona ni udhalilishaji mkubwa uliofanyika kwa mama yule(Bibi Kizee)..Sio hiyo tu,sikumbuki tarehe ngapi ila ni mwezi uliopita ni gazeti la mwananchi (kama sijakosea) lilitoa taarifa ya mchungaji mmoja kuvuruga ndoa ya muumini wake,siku chache baadae gazeti hilohilo likatoa taarifa ya kukanusha taarifa ya awali kwamba sio sahihi,lakini kwa namna moja ama nyingine kuna usumbufu ambao atakuwa ameupata muhusika kutokana na habari hiyo..

Hiyo ni mifano michache najua ipo mingi,thats why nikauliza taratibu/kanuni/sheria zinasemaje?au miiko ya uandishi inaruhusu kuchapisha taarifa ambayo bado haijathibitishwa??
 
Kweli mkuu ukizingatia habari zenyewe ni za kufumaniwa halafu kapigwa picha mtu mmoja. Naona habari ililenga kumdhalilisha mama wa watu ingawa sijasoma lakini kwa kuangalia picha tu inaonyesha hivyo.
 
Kwa aliyedhuriwa na anachoamini ni uwongo katika gazeti au chombo kingine cha habari, anaweza kuwasiliana nao ili wayamalize, na ikishindikana aende mahakamani.
 
Tanzania hamna waandishi wa habari makini wengi wao wapo kwenye maslahi zaidi! Wanatumkika
 
Back
Top Bottom