Magari: Toyota Porte na Siènta

askarikambi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
246
263
Habari wandugu.

Mwezi wa kumi mwaka huu, nakusudia kuchukua usafiri.

Bajeti yangu haizidi 10M. Nimejaribu kupita kwenye yard na website za kampuni zinazouza used cars hapa Tz kuangalia bei za magari. Gari zote zilizonivutia nimekuta bei yake siiwezi kwa sasa.

Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Na mimi urefu wangu hauzidi sh. 10 M

Gari za Toyota nilizokuta zinaangukia humu ni Porte na Sienta. IST na spacio sijazizingatia kwasababu zimejaa mno mtaani kwetu na mimi nahitaji kitu tofauti.

Sasa nahitaji msaada kwa anayezijua hizi gari, Porte na Sienta. Zina uzuri gari au shida zipi za msingi ili zinisaidia kufikia maamuzi ya gari ipi kuchukua.

Najua humu wapo wataalam wa magari na wale ambao wametumia au wanatumia hizi gari. Nategemea msaada wenu.

Ahsante.

1600228050058.png

Toyota Porte

1600228078613.png

Sienta
 
Habari wandugu.

Mwezi wa kumi mwaka huu, nakusudia kuchukua usafiri.

Bajeti yangu haizidi 10M. Nimejaribu kupita kwenye yard na website za kampuni zinazouza used cars hapa Tz kuangalia bei za magari. Gari zote zilizonivutia nimekuta bei yake siiwezi kwa sasa.

Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Na mimi urefu wangu hauzidi sh. 10 M

Gari za Toyota nilizokuta zinaangukia humu ni Porte na Sienta. IST na spacio sijazizingatia kwasababu zimejaa mno mtaani kwetu na mimi nahitaji kitu tofauti.

Sasa nahitaji msaada kwa anayezijua hizi gari, Porte na Sienta. Zina uzuri gari au shida zipi za msingi ili zinisaidia kufikia maamuzi ya gari ipi kuchukua.

Najua humu wapo wataalam wa magari na wale ambao wametumia au wanatumia hizi gari. Nategemea msaada wenu.

Ahsante.
Mmh sikushauri hizo gari ni nyanya mno ...hiyo pesa unaweza pata Toyota nzuri tu mbona?tofauti na hizo gari za sokoni (my apology)
 
Hapo hamna yenye tatizo maana engine zake zote ni economy, hazili mafuta!

Ila kwa capacity Sienta ina ukumbi mkubwa ndani. Porte ni nyembamba hivyo haiko na nafasi ya kujiachia.

Tatizo litakuwa mfuko wako tu labda kutegemea ni sh.ngapi utaongeza kwenye hela yako, ila pia unaweza ukaweka 9M ukachukua namba DU ya ambayo ni namba current kwa sasa, ukapata gari ambayo haijatembea hata miezi 4 nchini na ilio in excellent condition!

Hapo utakwepa kero ya kodi ambayo inafanya gari ya 4M japan kuchajiwa 6.5M un-neccessarily! Matokeo yake ndio gari inauzwa 11.5M showrooms.
 
Bajeti ya 9M nitaimudu.
Lkn kwa maelezo yako, kama nimekuelewa, hiyo gari naweza kuipata nje ya show room. Hapa sasa upate dalali wanaomuogopa Mungu, vinginevyo!!
Na unahisi hicho kiasi kinaweza kucover malipo yote na kuimiliki au nitegemee costs nyingine?
 
kwa usawa huu iyo pesa unapata gari nzur tu tulia fatuta pole pole usiwe na haraka
Maneno ya kutia moyo. Nimeanza kutafuta kama wiki tatu zilizopita, na pesa naitegemea mwishoni mwa Oktoba.
Kwa wiki hizo tatu, nilizunguuka yard na websites za wauzaji, ndio nikaishia kwa sienta na porte.

Sasa naufanyia kazi ushauri niliopewa humu, naweza kupata gari nyingine nzuri.
 
Hayo Magari yote mawili yanafanana Kwa asilimia kubwa kuanzia engine ni 1NZ,CC 1490,body material.
Sasa Kwa ushauri wangu ni Bora uchukue sienta kuliko huo mkate(Porte) pia sienta transmission ya sienta ni CVT utafurah jinsi gar yako inavyokuwa smooth pale Gia vinavyobadilika...
Ila yote Kwa yote kama utanunua sienta tafadhali usikubali kupakia watu wengi kulingana na siti zake maana sienta ina siti nyingi pia inapakia watu 7 kwahiyo kama utakuwa unabeba watu 7 utazidi kuichosha engine na body yake...
 
IFAHAMU GARI AMBAYO INAENDANA NA KIPATO CHA UCHUMI WA KATI

TOYOTA SIENTA

SECOND GENERETION

Toyota sienta ni gari ambalo kwa sasa watanzania wengi wameanza kulifikiria kutokana na hali ya uchumi imekaza sana halafu pia linatoa ushirikiano wa kutosha hhasa kipindi hiki cha uchumi wa kati lipo katika kundi la magari mvp ,gari hili ni dogo kwa umbo likiwa na urefu wa 5.5 m....likiwa na milango 5.kwa nini liliitwa toyota sienta ,sienta ni neno ambalo asili yake ni kutoka hispania ..maana ya neno ni saba ,kwa lugha ya wanachato tunaita (seven) kama ulivyo uwezo wake wa kubeba abiria ..kwa ndani hii ggari inanafasi ya kutosha kinachonipa burudani katika hii gari mkiwa ndani dash board yake ipo katika ili kila mtu anapata fursa ya kuona mwenendo wa dreva lakini hata wese likikata wote mnaona
Baadhi ya vifaa vilivyo katila gari hii ni

Station Wagon
Extras:Electric Doors
Safety Features:ABS, brake assist, Curtain Airbags,
EBD, side airbags, SRS Airbags
Exterior Features:Alloy Rims(optional), Fog
Lights(optional)
Interior Features:7 Seater, CD/DVD Player

Utake nini sasa kwa vyuma vilivyokaza hivi hii gari inatisha kabisa hata kama haufati uzazi wa mpango unafamilia kubwa bado inakufaa tu

Toyota Sienta Toyota sienta imezalishwa kwa vizazi viwili tangu mwaka 2003 hadi leo , first generation kilijulikana kama XP8 na kilianza mwaka 2003 hadi 2015 na second generation kilijulikan kama XP17 kilianza mwaka 2015 hadi 2018. Toyota Sienta imeundwa na NBC platform ambayo inachangia na Vitz, Platz, Porte na nyingine.

Muundo wa gari hili ulijipatia umaarufu saana kwenye soko la Japan kutokana na kuwa na nafasi ya kubwa ndani huku nje likiwa na muonekano mdogo ambau unarahisisha uendeshaji hasa kwenye mjini ya Japan ,na hispania walilipokea vizuri sana na kulibatiza jina
sienta !! Hivyo kutatua changamoto ya msongamano mkubwa wa magari.

Toyota Sienta comes inakuja na 1.5 Litre 1NZ-FE engine ambayo inakuwa na Super CVT transmission na inakuwa na chaguo la 2WD models or a Super ECT transmission kwa 4WD models.

Gari hili likiwa na injini yenye cc1496 uwezo wa injini ukiwa ni Tarque 136,
Nguvu hp 109, ukikutana na sienta usiwaze sana andaa hela ya kuja tank lita za mafuta 42 tu full tank ,
Huku gari hili likiwa na uzito wa kg 1310...uzito huu unaifanya gari kuwa na stability kubwa na kuwa na utumiaji mzuri wa mafuta

oGeneretion ya sienta iliyopo bongo inatumia injini ya 1NZ FE.14 HUKU likitumia mafuta aina ya petrol ...na kufanya liwe na matumizi ya kawaida
wastani wa 14km kwa lita mjini na 18km kwa lita ukiwa highway kutegemeana na uendeshaji wako....a.k.a mapigo yako

Mfumo wake wa break ni ABS , Mfumo rafiki kabisa kwa usalama wa chombo chako ..unaweza kujiuliza ABS ni nini ni kifupi cha ant lock breaking system mfumo huu unafanyaje kazi katika gari

Abs huu ni mfumo wa break ambao umewekwa katika gari
ili kukusaidia wewe dereva pale unapopata mshtuko wa
ghafla au hatari
Jisnsi ABS inavofanya kazi
Abs pale unapoendesha gari yako sehemu ya break
Hasa namaanisha kwa magari ya auto
unashaurisha kushika au kukanyaga taratibu ili kusudi usiweze
kuruhusu abs system kufanya kazi
Unapokanyanga kwa ghafla automatically abs ina sense kwamba
Hapa kuna tukio au ajali kitakacha tokea ni kwamba
abs itafunga break ghafla na gari kusimama papo hapo

Abs mara nyingi huwachanganya watu wengi pele unapoona
kitu cha ghafla mbele yako

Wewe unayeendesha magari ya auto

Ni muhimu sana uwe umefunga mkanda kwa safari ya kuanzia
5km na kundelea
tumia breki ya gari yako kwa manufafaa na sio
kukusababishia ajali\damage.....mfumo huu ni rafiki na unaepusha ajali hivyo

Sienta inakuja na mfumo huu

Uzuri wa gari hili

The goods

* Nafasi ya kutosha ndani kulinganisha na magari mengi madogo. Watu saba wanaweza kukaa vizuri kwa safari ndefu. It is comfortable enough for its size and price. Pia dereva anaweza kutoka kwenye siti yake ya mbele mpaka siti ya nyuma kwa urahisi bila kushuka kwenye gari.mfano ile safu ya pili inasehemu ukivua viatu unaviweka kwenye droo chini ya kiti

* Mfumo wake wa rear sliding doors kwa upande wa abiria na dereva unawezesha abiria wa size tofauti kuingia na kutoka kirahisi kwenye gari. Siti ya mbele ya abiria inaweza kukunjwa kwa mbele na kuacha nafasi kubwa zaidi kwa abiria na mizigo.

* Low maintenance cost, vile utumiaji wake wa mafuta naoweza sema kuwa ni relatively good kwa aina ya gari hili. Pia engine yake imetumika kwa magari mengi saana, so spare zinapatikana kirahisi. Vile vile SIENTA inashare parts nyingi na magari mengi madogo ya Toyota...ukienda dukani taja spare part no.

* Muonekano wake ni wa kisasa, linafaa kwa matumizi binafsi na biashara pia. Linapendwa na jinsia zote, japo wakaka wanalipenda zaidi, sijui kwa nini? Wenda ni vile wanapenda kusafiri na kundi la watu....kama kupendaa kampan kwenda kula bata viwanja mbalimbali

Upande wa grade

Toyota Sienta Grades inakuja na grade 3

Toyota Sienta X – Toleo hili linakuja na steel rims with plastic covers, key start, 2WD/4WD, Radio Player and Manual AC.

Toyota Sienta DICE – Toleo hili ni mid-level na linakuja na steel rims with plastic covers, key start,2WD/4WD, Radio/DVD Player and Automatic AC. Specified further by DICE Limited grade that comes with genuine leather-wrapped shift knob na a sophisticated interior furnishing.

Toyota Sienta G – Toleo hili ni luxury liko vizuri mno linakuja na alloy rims, Radio/DVD Player, Automatic AC, genuine leather wrapped shift, knob, fog lights na mart start

katika grade hizi grade ambayo ni bora kuliko zote ni G inafatiwa DICE uamuzi ni wako

Upande wa mafuta hapa ndipo wengi hupenda sana kukodoa macho haswaa
Toyota Sienta Fuel Consumption

Toyota Sienta 1.5L inatumia km : 19.2 Kwa lita 1

hapa sienta wamenifurahisha mno kwa kweli ina sifa zinastahili kabisa inafaa kwa familia ,biashara ,hata ujasiriamali iko poa sana ni moja kati ya gari za mjapani nazizimikia

Toyota Sienta Acceleration

Toyota Sienta inatoka 0-100 km/h kwa12.3 sec.

UBAYA WAKE

* Power sliding door mechanism ya upande wa abiria huwa inaharibika mapema, hasa pale jamaa wanapotumia nguvu kufungua badala ya kuacha mlango ufunguke wenyewe....Unahitaji umakini mkubwa

*Ni kuwa inabeba abiria7 kumbe ni 5 watu wazima na watoto2 ...watoto wanakamilisha list ya watu 7

* Kwenye spare zipo ila baadhi ni mtihani kuzipatw mpk wanafanya modification hivyo kuwapelekea wengi kufanya ubunifu kwa kuangalia spare inayoingiliana ili mambo yaende

* Halifai sana barabara za vumbi na zenye mashimo na mabonde mengi hasa mashimo ....miguu huwa inawahi kugonga

* ingawa muonekano wa nje haivutii ni gari safi sana ndani.wale wazee wa kuangalia muonekano kwa nje ...haina sura nzuri ....wabunifu naona hawakutaka kuumiza kichwa ila kwa ndani aisee kiko poa ila kwa toleo la 2013 ni nzuri mno inakuja na umbo lenye kuvutia zaidi tofauti na kizazi cha kwanza

GROUND CLEARENCE

Inakuja na ground clearence ya 5.5 inch sawa na 140 mm kwa barabara zetu inashauriw gari liwe angalau lipo na 6.5 inch ili kulifanya lipite hata katika barabara mbovu hivyo nakushauri kama ukilinunua peleka liinuliwe juu kidogo lisogee 6.5 inch ili uweze kwenda nalo barabara yoyote na ulinde bodi yake idumu zaidi

Matatizo ya gari hili ni

1. Transmission failure( gear box yake bwana kuharibika ni kugusa tu ) mengi ukiyakuta gereji ugonjwa ni gear box hasa kwa wageee wa kuunga unga oil badala ya kutumia oil maalumu iliyoshauriwa na watengenezaji wa gari

2. Electric door failure..milango ile ya kujifungua yenyewe kwa umeme si imara

3. Loss of power.

4. Oil consumption.....kuna wakati oili inakuwa inapungua ni vyema uwe na kanuni yabkulikagua ukikuta imeshuka unaongezea

Vizuri ni kuwa pamoja na sienta kuwa na hizo changamoto ila nyingi zinasababishwa na matunzo mabaya kutokusoma manual book


Unapokuja kulinagnisha na port

Port ina bodi nyepesi sana
Port viti vyake ni vyepesi havina mito mizito maana imetengenezwa kwa ajiili ya town trip
Haina stability nzuri barabran , ukiwa katika mwemdo mkubwa inapepesuka angalau sienta
Umbo la port halivutiii kabisa bora sienta


Kwa ushauri wangu nunua sienta mkuuu utaifurahia na hauwezi kujuta hata kidogo
 
Toyota raum ni moja ya gari zuri utakalopata kwa bei hiyo straight from Japan, japo fasheni yake imepita kidogo
 
IFAHAMU GARI AMBAYO INAENDANA NA KIPATO CHA UCHUMI WA KATI

TOYOTA SIENTA

SECOND GENERETION

Toyota sienta ni gari ambalo kwa sasa watanzania wengi wameanza kulifikiria kutokana na hali ya uchumi imekaza sana halafu pia linatoa ushirikiano wa kutosha hhasa kipindi hiki cha uchumi wa kati lipo katika kundi la magari mvp ,gari hili ni dogo kwa umbo likiwa na urefu wa 5.5 m..
Duh! Ahsante Boss. Hapa nimepata elimu ya kutosha, mambo mengi nimejifunza mengine hata sikuwa nahisi kama yapo kwenye magari.
Japo na mm nimehamia kwangu ni nje ya mji, lkn naweza kuliinua kama ulivyoshauri.
Ahsante.
 
1. Zote hazina common problem
2. Muonekano: They are all ugly
3. Space: Sienta inamzidi porte, ina nafas zaidi ukicompare na porte
4. Uimara: angalau sienta japo sio sana
5. Fuel consumption: they are all good
 
Back
Top Bottom