Sababu zipi zinazopelekea magari kuuzwa kwa bei ya chini sana katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma (Songea), na Rukwa?

ministrant

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
554
1,134
Wasalaam..
Nimekuwa nikipitia kurasa mbalimbali zinazouza magari yaliyotumika hapa nchini, ila nimeshangazwa sana na bei za magari kuwa chini sana hasa kwa Mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu.
Ningependa kupata uzoefu kwa walionunua magari katika Mikoa hiyo kwa kuzingatia maeneo mbalimbali juu ya biashara hiyo;
1. Je, hizo ni bei halisi kama wanavyotangaza?
2. Hakuna utapeli kutoka kwa wauzaji hao?
3. Gari hizo hazina matatizo makubwa ya kiufundi?
4. Gari hizo zimeingizwa nchini na kusajiliwa kihalali kiasi cha kutompa usumbufu mnunuaji kutoka katika Mamlaka za Serikali kama TRA na Polisi?
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom