Magari maarufu, yenye sura mbayaaaa..!

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
3,359
2,000
Najua baadhi yetu tunamiliki magari haya, ila kwakweli dah.. hapana. Inapokuja kwenye sura, magari haya inabidi yaturudishie chenji. Yaani hayana mvuto kabisaa! Inaelekea hata walioyatengeneza hawakuamini kuna mtu angeyanunua!!

1. Toyota Will V. Hiki kigari mi sijui designer wake alikuwa anafikiria nini? yaani hata hakieleweki! Yaani ni kama uchukue vitz uikate makalio uunganishie VW beetle kwa nyuma!

Toyota-Will-Vi.jpg

2. Ford Ka. Ukikionan hiki kigari kwa mara ya kwanza unaweza ukaangua kicheko. Yani kama kimdudu flani hivi.. Kibayaa..!
03 Ford Ka 03.jpg

3. Honda insight. Mtu unaendaje show room unachagua gari hii? Halafu ndio nyie mkishagundua mmeingia chaka baada ya mwezi mnaanza kutangaza kuuza. Nani anunue?
honda_insight-6324.jpg

4. Nissan Cube: Hawa jamaa na wenzao Toyota Bb naona walikosa kazi. Nini hiki? Huyu designer ni wakufukuza kazi mara moja!!
Worlds_ugliest_car_in_Pattaya_2.jpg

5. Toyota prius: Hili tatizo ni kubwa! Hata sijui nisemeje..
032_toyota_prius.jpg

6. Hiki nacho ni kituko kingine. Toyota Platz.. Yani vitairi vidogooo.. Mvuto sifuri. Wadada wanavipendaje?
1295660895_148126418_1-Pictures-of--TOYOTA-PLATZ-200001-Reg-2006-As-in-Original-and-Good-Conditi.jpg

7. Toyota Spacio. Jamani, hii gari ni kama walisahau kitu wakaja kukiongezea mwishoni..! Yani ipo ipo tu.. Na kuna nyingine inaitwa FunCargo ndio kichekesho kabisa..
toyota_corolla_spacio_2815186.jpg

8. Daihatsu Terios. Ni gari nzuri, ila shapeless! Halafu kembambaa.. yani mtu ukitaka kubadilisha mawazo inabidi upaki pembeni, utoke nje!
terios.jpg

9. Christler PT Cruiser. Mi siongei. Jionee mwenyewe. Utadhani inajiandaa kupiga chafya!
chrisler pt cruiser.jpg

10. Toyota Opa. The fact kwamba kila mtu analo, haiondoi ukweli kwamba huu mgari una sura mbaya kama nini!
opa.jpg

11. Toyota Vista sedan. Bora wangeacha tu ile Vista Ardeo. Sasa hapa ndio wamefanya nini? Hata kama unayo, kubali hii gari haina mvuto!

vista.png

13. Toyota Verossa: Hii gari ikiwa inakuja kwa mbele, unaweza ukadhani inatania. kumbe iko serious!! Cha ajabu watu wanaipenda
toyota_verossa_3143964_orig_F9F_PakWheels(com).jpg

14. Hummer. Hivi hii midubwasha watu wanaipendea nini? Sawa, inauzwa gali, kwahiyo? Hata kipofu anaweza kuona jinsi hii gari ilivyo mbaya..!
hummer-h2-safari.jpg


"Babaako analo?"
 

zimwimtu

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
1,989
2,000
jaman, unachokichukia au kukipenda sio kwamba itakuwa vivo hivyo kwa mtu mwingine. waache watu na magali yao wew tafta unaloona linapendeza.
 

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,979
2,000
Dah! Umenikatisha tamaa, yaani mimi sahizi najikusanya ninunue SPACIO......
we ji kusanye tu mkubwa kwani kila ukipendacho lazima kipendwe na wengine!!!!mi nina Funcargo na ninaipenda balaaa!!wife mwenyewe anataka nimnunulie nissan cube ndo mtima wake ulipo!!go for your choice!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom