Ya ndani usiandike. Haitakuwa vizuri. Ila yale yalifanyika Public hayo waweza kutumegea ππNingeweza kuandika lakini kwa heshima a mamdogo nikae kimya..
Kwa u babe ilikuwa ni zaidi ya hapo na Kuna baadhi ya viongozi walisoma namba ile kauli unajua mi nani haijaanza leo.
Ni kweli Kuna vitu nimefaidi zaidi ya biscuits nadhani unajua kama watoto wa viongozi huwa wana package zao.
Miaka kadhaa alikosa ile hadhi ya vip sijui kilitokea nini.
Alasiri njema,, si vyema kutangaza mambo hata kama tunayajua...Ya ndani usiandike. Haitakuwa vizuri. Ila yale yalifanyika Public hayo waweza kutumegea ππ
Boss, JF ni social media ya kupashana habari pia kama vile instagram, FB, Twitter....don't take it personal....!Hata sisi tunafiwa pia.
Na hatuleti misiba mitandaoni.
Matatizo yenu na watu wenu wa karibu, msifikiri ni matatizo hayo ni ya kila mtu.
Mnapopata misiba, siyo kwamba inamhusu kila mtu.
Pole mzee wangu kwa msiba wa swahiba wako....Allah amlipe Firdaus.MAGAMBO MAKONGORO AMEFARIKI DUNIA
Kwa wanaomfahamu Magambo Makongoro amefariki leo hospitali ya muhimbili, maziko kesho Kisutu Alasiri.
Msiba upo nyumbani kwake Msasani opp na nyumba ya Mzee Rais Mwinyi Mikocheni.
Nimepokea taarifa hiyo hapo juu hivi punde.
Magambo tunajuana toka udogo wetu ni mtoto wa Chief Makongoro.
Tulipokuwa shule tukifanya picnic yeye akitupeleka Kigamboni nyumba ya mapumziko iliyokuwa ya Gavana wakati wa ukoloni na kwa wakati ule baada ya uhuru ikawa iko chini ya Mwalimu Nyerere kama Rais wa Tanzania.
Mwalimu alikuwa haitumii nyumba hii na Magambo yeye kwa ule usuhuba uliokuwa baina ya baba yake na Nyerere alikuwa mtoto wa nyumbani State House.
Nakumbuka siku zile hata jina hili la Ikulu lilikuwa bado.
Magambo alikuwa mwenzetu na mchezo wetu ulikuwa mmoja pamoja na Kleist na mdogo wake Ebby, Yusuf Zialor, Wendo Mwapachu, Bubby Bokhari, Christopher Faraj, Abdallah Mohamed Saleh (Tambaza), Abdul Mtemvu, Edward Makwaia (sasa Chief wa Siha), Abdallah Mgambo, Eyshe na Mariam Max, Erica Kisa, Janet Zebedayo, Haitham Rashid, Esther Mzena wenzetu wengine wengi siwakumbuki.
Wenyewe tukijiita Scorpions na wengi tulikuwa wanafunzi St. Joseph's Convent.
Baadhi wemetangulia mbele ya haki.
Miaka ya kati Magambo alikuwa akifanya kazi Inter King iko Mbezi wanafuga kuku.
Mara ya mwisho miaka michache nyuma mwezi wa Ramadhani tulikutana Masjid Ngazija alikuwa na Abraham Sykes.
Nakumbuka siku ile walinishambulia sana kwa kunichangia ati mie najidai sana na Msikiti Ngazija nauona kama mali yangu nikiwaona wao wanakuja kusali pale roho inaniuma.
Haya ndiyo yalikuwa mapenzi yetu tulikutana lazima tubwatizane huku tunacheka.
Nilipoteana na Magambo kwa muda hatujaonana.
Allah amsamehe na amtie Firdaus.
Amin.
View attachment 3339866
Magambo Makongoro
inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Nimesoma mama mtoto wake akimuombolezea. Mwenyeze Mungu awape subra familia na wote walioguswa na msiba huu
View attachment 3342049View attachment 3342050View attachment 3342051View attachment 3342052
Ni jambo jema sana kukumbukwa kwa wema haswa na mzazi mwenza
Baba yake (au babu yake?) Magambo, Chifu Makongoro, ndiye mtu aliyemuambia baba yake Julius Nyerere, Chifu Nyerere Burito, kwamba huyu mtoto (Kambarage Nyerere) ana akili sana, anafaa kupelekwa shule.Alipata Heshima zote Kama Mtoto wa Nyerere lakini. Alisomeshwa USA na alikuwa afanye Kazi World Bank ila sikumbuki nini kilimsibu.
Mimi nilimuona miaka ya 90 mwanzonj, alikuwa ni Mbabe sana hapo Interchick na BANDAG.
Haya na mimi nilifiwa.Boss, JF ni social media ya kupashana habari pia kama vile instagram, FB, Twitter....don't take it personal....!
Kama umefiwa na unataka msiba wako ujulikane, na wewe una haki ya kuleta uzi wa msiba wako mtandaoni.Haya na mimi nilifiwa.
Huyo jamaa actually sijawahi kumsikia kabla ya uzi huu,,ila Nina uhakika ukoo wa makwaia kina kidaha waliokuwa ni waislamu,sema baadae waingereza walikua wanamuundaa kidaha kuwa kiongozi wa nchi,wakambatiza na kumwita David kidaha makwaia Kama sikosei,Bado hujajibu swali langu, umeongelea dhana tu, hapo Ikizu na Zanaki hakukuwa na Uislamu kabisa, kuna watu wa asili sijui ndio mnawaita wapagani na Wakristo, makao makuu ya Wasabato Tanzania yalijengwa Zanaki pale Busegwe kwa kina Nimrod Mkono.
Hapa nieleweke sina interest na dini yoyote, lakini najaribu kutafiti huyu marehemu chimbuko la uislamu wake, nataka kujuwa tu maanda yule Linda aliyezaa naye najuwa alikuwa mkristo akasilimu sasa ni mwislamu.
Kwasababu huzuni zao siyo huzuni za kila mtu.Kama umefiwa na unataka msiba wako ujulikane, na wewe una haki ya kuleta uzi wa nsiba wako mtandaoni.
Kwa nini unaona vibaya watu wakiomboleza misiba ya watu wanaowajua hapa JF?
Mkuu,Huyo jamaa actually sijawahi kumsikia kabla ya uzi huu,,ila Nina uhakika ukoo wa makwaia kina kidaha waliokuwa ni waislamu,sema baadae waingereza walikua wanamuundaa kidaha kuwa kiongozi wa nchi,wakambatiza na kumwita David kidaha makwaia Kama sikosei,
So nahisi hata chief makongoro alikuwa ukoo wa makwaia
Huzuni zao si huzuni za kila mtu.Kwasababu huzuni zao siyo huzuni za kila mtu.
Ni namba zinazogawanyika kwa moja na zenyewe tu πππIla mpaka leo watoto, wajukuu za nyerere huwa siwaelewielewi π
Ova
Kuna mmoja alikuwaga denmark alirudi bongo kutokana na 1,2,3 chengaNi namba zinazogawanyika kwa moja na zenyewe tu πππ
Ukoo mkubwa una watu wengi hauwezi kukosa characters wa kila aina.Kuna mmoja alikuwaga denmark alirudi bongo kutokana na 1,2,3 chenga
Kuna wale jamaa zangu pale msasani wana kibar chao na chenga alafu lile eneo la wazi
La mama nyerere, wale akili zao nao wanazijua wenyewe
Kuna shida mahali naona π
Ova