Magaidi wawili wauawa Mbagala Kilungule

Magaidi wawili wauawa Mbagala Kilungule

Mgodo Mgodoki

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
1,399
Reaction score
1,368
Tukio hili limetokea jioni hii Mbagala Kilungule Jijini Dar ni baada ya Magaidi hao walipotaka kumpora SMG Askari Polisi aliekuwa anapita maeneo hayo bahati nzuri kulikuwa na Askari kanzu aliekuwa na Pistol kwa mbali alipoona tukio ndipo alipowapiga Risasi hao Magaidi.

Gaidi mmoja kabla hajafa akatoka taarifa kuwa kuna wenzake wapo nyumba fulani ndipo kikosi kamili cha askari kilipokuja na kuzingira hiyo nyumba na kuwakuta watu watano ndani, watatu wa kiume na wawili wakike, zimekutwa silaha na mabomu 15,walipoulizwa motive yao wakasema wanapigania Dola ya kiislam Nchini.
 
Habari hiii umeipata wapi??!! Unaonaje ikiweka picha kama wewe ndio source?!!
 
Hapo ndio utajua upeo wa Tanzania Maan watanzania ni mabingwa wa uzushi
 
Mimi nimekuta tukio ndio linamalizikia kwenye hiyo Nyumba na sikuweza kupiga picha kutokana na mazingira yalivyokuwa.
 
Kamakweli nijambo jemasana kufika kesho tutakuwa tushafahamu ukweli
 
Aman inakuwasha sasa wataka magaid...waulize kenya wenzako...
 
Hao ni wezi mkubwa hakuna maggaidi wanaiba silaha maana wale kwanza hawakosei tukio maana hawana cha kupoteza
 
Tunavyoelekea uchaguzi tutasikia mengi.....alafu mie nakereka...jambazi utamwitaje gaidi?...tuwaulize jirani zetu kenya naona unahamu na hao jamaa....haya yangu masikiooo
 
Back
Top Bottom