Moja ya mapungufu ya serikali hii ni kutokuwa serious na hili suala la ugaidi unaoota mizizi hapa nchii. Bunge limetumia muda mwingi kupitisha dili za mafisadi ndani ya serikali na kusahau kabisa kuweka sheria za kuidhibiti hali hii. Wahalifu hawa wameachwa wakirandaranda tu, mara Morogoro, Arusha, Tanga na sasa Dar Es Salaam! Inashangaza sana, sijui kigugumizi kiko wapi hapa, nyumba za ibada wanazotumia zinafahamika, wahusika wanafahamika na hata kama hawafahamiki waliokamatwa wakiwa hai wangetosha kuwa mtaji wa kuwanasa wengine walio kwenye mtandao huu. Je inawezekana wahalifu hawa wanalindwa na baadhi ya wana mtandao wao waliopo ndani ya serikali?