Mafuta ni ya Wazanzibari: Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta ni ya Wazanzibari: Zitto Kabwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Junius, Sep 30, 2010.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ahoji Zanzibar kutofaidika na madini ya Bara

  Na Salum Vuai, Maelezo

  MGOMBEA ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema iwapo atarudi tena bungeni, atasimamia kwa nguvu zake zote ili suala la mafuta na gesi liondoshwe katika orodha ya mambo ya Muungano.

  Kabwe alikuwa akijibu suala kuhusu Muungano katika mdahalo uliowakutanisha wagombea wa kundi la vijana uliofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV juzi usiku.

  Katika mdahalo huo ulioshirikisha wagombea wa vyama vya CUF na CHADEMA kutoka majimbo ya mikoa mbalimbali chini ya uenyekiti wa Jenerali Ulimwengu, Kabwe alisema kimsingi anakubaliana na hoja kuwa iwapo Zanzibar kuna mafuta, basi hiyo ni mali yake na haijuzu kutiwa mkono na Serikali ya Muungano.

  Alifahamisha kuwa, kwa vile Zanzibar haifaidiki na rasilimali za madini zinazopatikana Tanzania Bara, ni haki ya wananchi wa huko kudai mafuta yanayoaminika kuwepo visiwani yasiingizwe katika mambo ya Muungano.

  "Suala la mafuta yanayokisiwa kuwepo Zanzibar, limezua mjadala mkubwa bungeni, mimi sioni mantiki ya kuwanyima Wazanzibari haki yao, kwani nao pia hawafaidiki na rasilimali za madini zilizoko Bara, nitajitahidi kuona mafuta yanaondoshwa kwenye mambo ya Muungano", alieleza msimamo wake.

  Aidha alieleza kuwa mbali na suala hilo, zipo Wizara nyingi zilizo chini ya mwamvuli wa muungano wa Tanzania lakini haziihusu Zanzibar ingawa ina wabunge.

  Hata hivyo, mgombea huyo alisema muungano wa Tanzania ni kitu cha thamani kubwa ambacho nchi nyingi duniani zinatamani kuwa na umoja kama huo lakini zimeshindwa.

  Aliwasifia waasisi wa muungano huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na marehemu Abeid Amani Karume, akisema wameweka misingi imara ya udugu kati ya watu wa pande mbili hizo, ambayo inahitaji kuimarishwa kwa kutoruhusu mgawanyiko.

  Ili kufikia azma hiyo, alishauri kuweko na haki sawa kwa wananchi wa nchi hizo kwa kutozusha mifarakano katika mambo yanayoweza kupatiwa ufumbuzi bila kusuguana.

  Alifahamisha kuwa, muungano wa Tanzania uliasisiwa kama njia ya kuelekea umoja wa Afrika nzima ambao waasisi wake na viongozi wa zamani wa nchi mbalimbali wakiwemo Kwame Nkrumah wa Ghana na Gamal Abdelnasser wa Misri walikusudia kuunda.

  "Pamoja na kasoro zinazojitokeza, lakini muungano wetu ni urithi mzuri tulioachiwa na waasisi wa taifa letu, hivyo changamoto zilizopo zitufunze namna bora ya kuuimarisha na kuuenzi na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunawaenzi waanzilishi wake", alifahamisha.

  Nao wagombea wa CUF kutoka baadhi ya majimbo ya Morogoro na Dar es Salaam, walisisitiza msimamo wa chama chao kuunda serikali tatu iwapo watashinda katika nafasi ya uraisi wa Tanzania.

  Walisema chama chao hakioni sababu ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili, na kuelezea jambo hilo linaridhiwa na wananchi wengi wa Tanzania Bara, ambao wanaona njia hiyo tu ndiyo itakayosaidia kuondosha baadhi ya kero za muungano huo.

  Mwenyekiti mwenza wa mjadala huo Jenerali Ulimwengu, alisema utaratibu huo utaendelea katika maeneo mbalimbali ili kuwapa wananchi fursa ya kufahamu kwa undani mwelekeo wa wagombea wao kabla kuingia katika uchaguzi mkuu Oktoba 31, mwaka huu.

  Aliwapongeza wagombea walioshiriki kikao hicho kwa kusema hiyo ni miongoni mwa dalili za kukua kwa demokrasia nchini.
  SOURCE: IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR VIA JIKUMBUKE WEB BLOG
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hoja nzito hii...!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na hoja ya Mheshimiwa Zitto kama mafuta yakigunduliwa Zanzibar yanapaswa kuwa ya wazanzibar lakini pia nataka kujua iwapo Zanzibar inatoa mchango kuendesha serekali ya Muungano.Napinga mfumo wa serekali tatu kwasababu Zanzibar ni nchi ndogo sana ukilinganisha na Tanzania bara laiti ingekuwa mungano baina ya Tanzania na kenya nadhani serekali tatu ingefaa zaidi.Tanznaia bara ina watu zaidi ya 40 milion Zanzibar watu 1 milioni Zanzibar itakuwa tayari kuchangia gharama za uendesha wa serekali yake na ile ya Muungano au mzigo wote utaendelea kubakia kwa watanganyika pekee.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kumbe Znz haifaidi madini!basi wale mafuta yao!kwani shida ipo wapi?
   
 5. m

  mcongo Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hakuna ubishi katika hilo zito kasema kweli
   
 6. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye mkataba wa muungano swala la mafuta halikuwa swala la muungano, liliingizwa kinyemela 1977 na CCM, na ndo pale linapokuja swala la katiba mpya! yanaitajika majadiliano na mkataba mpya!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hata bara haifaidi madini. "Wawekezaji" wamekwapua kila kitu.
   
 8. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Madini gani?
   
 9. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yes hatutaki mafuta ya watu..!
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wamezowea kutafutiwa mtu mwenye kuburuzwa ili watimize miradi yao ili ukileta ubishi unaambiwa unapigwa chini inabidi uwe mpole, na ndio maana safari hii wamewawekea sheni maana dr bilal asingekubali mambo yasiyo na maslahi na nchi yake.

  Wazanzibar nawapeni pole lakini mnayataka wenyewe rais wenu kuchaguliwa dodoma na kuja kuongoza zanzibar kwahiyo msilalame na nyie watafute wajanja wakizenji ili waliingize swala la madini kinyemela kwenye mambo ya muungano.

  Msipo amka mtaendelea kudhihakiwa kwa kuitwa mdebwedo ilhali nchi yenu ndio nchi ya kwanza Africa kuwa kituo cha biashara, na ndio nchi za mwanzo kustaarabika ya kwanza africa kuwa na televisheni ya rangi, ya kwanza africa kuwa na nyumba ya lift ( beit el ajab ) ya kwanza africa kuwa na taa za barabarani. leo nadhani mmekuwa nchi ya mwisho kwa yote hayo mpaka ustaarabu maana hakuna tena yale yaliyokuwa yanwafanya muwe kwenye kundi la walistaarabika. Si tumeona watu wakipaka vinyesi kwenye visima vya maji? Ukahaba ulivyo kidhiri pale kwa bonny stone town na kiwengwa? au hamuoni uozo huu? nyie ndio mna dhamana ya kuuondoa kwahiyo msiwe mdembwedo mnatakiwa mgangamare.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wazenji msiwe na wasiwasi.

  Soon mtakuwa na nchi yenu wenyewe.

  Mtajiamulia mambo wenyewe na nina imani tutakuja huko tuwe Wanyamwezi wenu.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Zito hilo haliwezi na kubwa zaidi nyie wabangaizaji wengine mliomo humu ,hivi yale makeke yapo wapi ? mbona hamsemi kama ni hivyo muungano na ufe ?? au kwa kuwa aliesema ni zitto
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwiba, wee kumbe kipofu. Si nimeandika hapo juu kuwa si muda mrefu mtakuwa na nchi yenu?

  Muungano utakufa sasa hivi, wee subiri tu uone. Mtakipata mlichokuwa mkikililia kwa miaka mingi.

  Watakuja Wazungu na Waarabu na mtakuwa MATAJIRI saana.

  TO HELL WITH MUUNGANO.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  ..hivi umeme tunaowapa bure wa-Zenj huwa tunatofautisha kwamba umezalishwa na gesi,maji,au mafuta?

  ..pia mishahara inayolipiwa SMZ huwa wanatofautisha kwamba pesa zake hazitokani na mapato ya madini?

  ..marupurupu na mafao ya wabunge wa Zenj ktk bunge la muungano pesa zake huhakikiwa kwamba hazitokani na mapato ya madini ya Tanganyika?

  ..kama wa-Zenj hawafaidiki na madini ya Tanganyika, basi wanafaidika na kahawa,chai,mahindi, etc etc ambavyo ni vya Tanganyika.

  ..zaidi mbona wanaishi huku Tanganyika bila bugudha yoyote ile,wakati wa-Tanganyika wakienda Zenj wanadaiwa passport na vibali vya kazi?

  ..wa-Zenj wapewe mafuta yao na nchi yao bila mjadala wala kuchelewa. kama kuna ulazima wa kushirikiana nao basi tufanye hivyo kupitia JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi mpaka sasa mnajidanganya kuwa watanganyika tunautaka sana huu Muungano? Kwa wengine kama mimi hata ungevunjika jana ingekuwa imechelewa!

  Amandla......
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hayo mafuta yapo kweli au ni mizengwe ya wanasiasa waliokosa agenda ya kuombea kura?
   
 17. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu hiyo nchi unayosema ilikuwa maarufu kibiashara mipaka yake iliishia wapi au na wewe ni mfuasi wa berlin conference. Kama sio basi usifuatilie sana mipaka tuliyowekewa na wakoloni
   
 18. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sana sana naona mafuta yapo bara
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  hata bara haifaidiki na madini, ile asilimia 3 opppssss 1.5 oppsssss 0.5 inaliwa juu kwa juu hata kabla haijawafikia wananchi.
   
Loading...