Mafuriko makubwa Kyela: Misaada ya kibinadamu ya hali na mali inahitajika haraka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,105
Karibu magazeti yote yameripoti kuhusu mafuriko yaliyotokea Wilayani Kyela , tunawashukuru sana wana habari mlioweka habari hii maana imerahisisha dunia kujua kinachoendelea nyumbani kwetu .

Lakini ukweli ni kwamba hali ni mbaya mno kuliko inavyoripotiwa , maeneo kama Kajunjumele , Katumbasongwe , Talatala , Mwaya na makwale hali ni mbaya kupita kiasi , vifo vya watu watano vinavyoripotiwa kutokea vyaweza kuongezeka muda wowote , maana kuna idadi kubwa mno ya watu ambao hawajulikani walipo , waweza kuwa salama lakini pia waweza kukwama kwenye tope baada ya kusombwa na maji .

Natoa wito kwa mamlaka kuongeza juhudi za uokozi na kuongeza maeneo ya dharula ili kupunguza msongamano kwenye maeneo machache yaliyotengwa , niwaombe sana Watu wa Kyela waliojazana DSM na kwingineko na waliobarikiwa kuangalia namna ya kuji organise na kupeleka misaada ya dharula nyumbani ili kuokoa ndugu zetu na kuwalinda na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu nk.

Mungu ibariki Kyela

Naomba kuwailisha .

picha kwa hisani ya Mgirik
IMG-20190511-WA0044.jpeg
 
Ungeweka na picha kabsa, isije kua ni mradi wa siri unatengenezwa kama wa kagera.
natambua jinsi mlivyokwazika na tetemeko la kagera lakini niwaombe sana muamini taarifa hii ambayo magazeti mengi yameripoti , picha najaribu kuziweka zinanigomea
 
Sasa mbona mbunge wenu jana ndio alikaimu nafasi ya waziri mkuu bungeni si heri angetumia nafasi hiyo kuomba msaada kupitia bunge?

Poleni sana!
mkuu kila binadamu ana utashi wake , nisingependa kuingiza siasa kwenye hili
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom