Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,635
- 218,068
Mvua Kubwa inayonyesha Wilayani Kyela , huko Mkoani Mbeya imesababisha Mafuriko Makubwa ambayo yameleta maafa makubwa sana , Makazi ya watu karibu kila kijiji yamesambaratishwa vibaya huku Mashamba ya Mpunga yakifunikwa na maji kiasi cha kuharibu kabisa mpunga wenyewe , Hali ni mbaya sana .
Kivuko Maarufu na Muhimu sana kinachounganisha vijiji vya Lupembe , Ibungu na Mji wa Kyela kinachojulikana kama KITYEPUTYEPU kimesombwa na mafuriko hayo huku wananchi wasijue la kufanya .
Kivuko hicho kinaunganisha Mji wa Kyela na baadhi ya vijiji na kinaanzia kwenye Taasisi ya Mango Tree , hili ni pigo lisilo na mbadala , Daraja la Ipyana nalo limepigwa na miti iliyong'olewa na Mafuriko na kupinda , huku watumiaji wa daraja hilo wakikumbwa na wasiwasi kama waendelee kutumia daraja hilo au la .
Kwa ujumla vijiji vingi vimepigwa na Mafuriko na kiukweli msaada wa haraka unahitajika , ukianzia kijiji changu cha Kajunjumele , Bujesi , ipyana , bujonde , Ndandalo , maeneo yote ya Kyela Mjini yanayotazamana na Hospitali ya Wilaya yote yamezama baada ya mto kiwira kutapika , zipo taarifa kwamba Mamba wameishaingia kwenye makazi ya watu .
Katumbasongwe , Kabanga na Isaki hali ni mbaya sana baada ya Mto Songwe kutapika , huko Mwaya , Tenende na Talatala hali haisemeki baada ya mto Mbaka nao kutapikia makazi ya watu na kusababisha Mafuriko ya Kutisha , kiasi cha kufunika barabara ya Nkuyu - Matema .
Bado hatujajua Juhudi zinazofanya na Serikali ya Wilaya hiyo ili kusaidia wananchi , Japo Gari la Mkuu wa Wilaya linaonekana kuzunguka huku na huko .
Mungu ibariki Kyela .