dah nijambo la kumuomba sana Mungu atusaidie kwani haya ni majanga tu ambayo hata tukitupia lawama upande mmoja matatizo yote bado tunakuwa hatujaliangalia kwa mapana yake! Unajua hata nchi zilizo endelea nako huwa majanga kama haya yanatokea na hata kama sijasahau kuna nchi moja majuzi tu hapa imekuwa katika majanga ambayo hayana tofauti sana na haya japo kuwa yakwao yalikuwa makubwa kiasi kwamba watu wengi zaidi walipoteza maisha, nijuavyo mimi kiuchumi tuko nyuma kiasi nikashawishika kuona kwamba nchi hizo kiuchumi zimetuacha na katika swala zima la majanga hazikufanya chochote zaidi ya kumuomba Mungu awasaidie hivyo basi watanzania tumuombeni Mungu atusaidie ili hali kama hii isijirudie lakini pia tuwe na utamaduni wakuyapokea matatizo tukaona niyakwetu na tukatafuta njia ya kuyatatua kuliko kukaa na kuanza kuhamishia wengine, Mungu ibariki Tanzania.