Mafua yananisumbua long time

Da jamani hata mimi nna aleji mafua toka nna 14 mpaka sahii nakimbilia 30 halafu nyingine nikioga nawashwa sana ugoko niambieni dokta mzuri niende

Pole sana mkuu
Ngoja tusikie wadau hapa wanasemaje, JF ni jungu kuu halikosi ukoko tutapata dawa tu, worry not
 
Kaka Mziwanda
Huo urojo nipake kwenye nyao za miguu halafu zitasaidia kuondoa mafua? Naomba unifafanulie zaidi binamu ili nisikosee instructions

ninavyosikia ni kuwa unachukua vitunguu saumu unaviponda then unapaka kwenye nyayo. you smear. ni hivyo tu, nadhani ni mpaka majogoo
 
aSANTE aRSENE
ila naomba kama ungeweza kunisaidia hospital ambayo ulienda wewe mkuu ila nami nipate hiyo dawa. Pia ningefurahi kama hungeniandikia aina ya dawa hiyo ya matone ili nikamuone daktari kama atai-recommend kwangu
samahani sana mkuu kwa kuchelewa kukujibu ,unajua sometimes tunakuwa tunafatialia posts nyingi kiasi tunajisahau.i hope sijachelewa sana na kama umeshapata ufumbuzi ni heri.
dawa ambayo niliotumia mimi ni hii hapa "RHINOCORT AQUA NASAL SPRAY" .AstraZeneca Pharmaceuticals - U.S. Home Page.
 
Pole sana ndugu sipo,
Mafua yanaweza kuwa una chronic infection na dawa utumiazo ni relief tu ya mafua na si tiba ya infection.
Pili yawezekana una ugonjwa uitwao Sinusitis au sinus infection, huu ugonjwa huambatana na headache na wakati mwingine kuziba masikio kwa sababu ya kupiga sana chafya. Nina ndugu yangu ilibidi afanyiwe operation kuclear vijinyama puani.
Sinus iliyokomaa sana huzaa cancer,hivyo ndugu yetu usipuuze na kunywa painkiller tu Onana na daktari bingwa wa ENT hospitali yoyote (Muhumbili, KCMC, REGENCY, AGAKHAN) na utapata vipimo na matibabu.
Get well soon.
 
Mfumwa
Nashukuru sana kwa maelelezo na ushauri ulionipa kwanza MUNGU akubariki sana ndugu yangu.
Pili naomba kama una access na huyo dada tafadhali umuulize kama kuna dawa alitumia kumaliza hilo tatizo lake.
Tatu nashukuru tena kwa haya mawazo yako na ukweli ni kwamba nime-print down ili kufanya implementation

Be blessed
Hapo ndiyo unapokesea sasa.

Pole sana ndugu sipo,
Mafua yanaweza kuwa una chronic infection na dawa utumiazo ni relief tu ya mafua na si tiba ya infection.
Pili yawezekana una ugonjwa uitwao Sinusitis au sinus infection, huu ugonjwa huambatana na headache na wakati mwingine kuziba masikio kwa sababu ya kupiga sana chafya. Nina ndugu yangu ilibidi afanyiwe operation kuclear vijinyama puani.
Sinus iliyokomaa sana huzaa cancer,hivyo ndugu yetu usipuuze na kunywa painkiller tu Onana na daktari bingwa wa ENT hospitali yoyote (Muhumbili, KCMC, REGENCY, AGAKHAN) na utapata vipimo na matibabu.
Get well soon.
Hiyo naona kama ni tatizo la tofauti na alilonalo Sipo?
Sinusitis.inahusishwa na kutokwa 'mafua' ya kijani.
 
Kuna dada alisumbuliwa na mafua tulipokuwa kidato cha 5 mpaka cha 6. Na kabla ya hapo alisema kuwa alikuwa nayo. Alitumia dawa tofauti tofauti (sizikumbuki labda nimtafute), lakini Mafua yake yaliisha aliposhauriwa yafuatayo na Daktari mmoja.

Moja, kila akilala alalae na nguo, hasa inayofunika sehemu ya kifua. Hata kama kuna joto, manake aliambiwa asubuhi kunakuwa na baridi ambayo yeye atahisi ni ndogo na hata jifunika shuka, lakini inamuathiri (alikuwa anaishi Dar).

Pili, anywe maji vuguvugu, na aepukane na maji, juice (sharubati) ama vinywaji vyovyote baridi.

Tatu, asioge maji baridi hata kama kuna joto. Muda wowote akitaka kuoga aoge na maji moto (vuguvugu).

Nne, ajihadhari vitu vinavyotoa vumbi ama moshi (hii ilimsaidia shuleni hakupangwa kwa vitu hivyo).

Ninavyokumbuka kwa kuwa Daktari aliyomshauri hayo hakumpa dawa yoyote, yule dada alimdharau yule Daktari. Lakini aliamua kujaribu hayo aliyoambiwa. Baada ya siku chache mafua yakaanza kuondoka, na hadi nilipoonana naye baada ya kumaliza shule alikuwa hana tena hayo Mafua.

Nakushauri jaribu kufuata hayo mambo niliyoandika, na pia ufuate na waliokushauri wengine. Lakini muhimu ni kuwaona wataalamu wa afya. Lakini nahisi sijakumbuka yote ila kwa uchache nimekumbuka.

Mola akupe nafuu haraka na POLE.
Hilo ni la muhimu sana watu wenye allergy kufahamu. Mara nyingi madaktari hushindwa kuelimisha vizuri waathirika kuhusu allergy, what it is, what to expect and what not to expect. Mimi niliamini kwamba dawa alizonipa daktari kazi yake ni kutibu, kumbe sio.

Vumbi la ndani huwaathiri watu wengi wenye matatizo ya allergy (Vumbi lililo kwenye mazingira ya binadamu ambalo halipati kuchomwa na jua). Sio rahisi kuepuka kabisa vumbi, ila kuna maeneo ambayo watu huyasahau mfano, carpets, frame za picha ukutani, juu ya kabati, magodoro (wengine hulazimika kuweka cover maalum kwenye godoro na mito).

Naweza kuongezea kwamba chumba unacholala upunguze vitu vilivyohifadhiwa humo (books, boxes, etc). Chumba kipate hewa ya kutosha inayoingia na kutoka, ikiwezekana hata wakati wa kulala. Asubuhi fungua mapazia chumba kipate mwanga.

It is not uncommon for someone to be allergic to a more than two or three things. Ngozi yangu hupatwa na vipele wiki mbili kabla mvua za mwanzo za masika hazijaanza. Is that not wierd?

Soma hapa taratibu.
 
Lazydog
Nashukuru sana kwa maelezo yako pia hiyo link uliyonitumia ni nzuri sana imenisaidia na kupanua uelewa wangu kwa kiasi kikubwa kuliko mwanzo. Nitatumia ushauri wako na uliopo ndani ya hiyo link kwa kupata advice ya daktari pia.

Thanks in advance
 
Hapo ndiyo unapokesea sasa.
Hiyo naona kama ni tatizo la tofauti na alilonalo Sipo?
Sinusitis.inahusishwa na kutokwa 'mafua' ya kijani.

Kama alivyosema Lazydog mafua yangu hayana ukijani wowote, ni ya kawaida kabisa ila ninachoweza kusema kinachoniumiza zaidi ni chafya kwani wakati mwingine zinapelekea hadi headche pamoja na chest pain. Ila i will turn back kwa a daktari pamoja na ushauri huu hapa then namwamini MUNGU atanitatulia tatizo langu. I see the bright time
 
Pole sana ndugu sipo,
Mafua yanaweza kuwa una chronic infection na dawa utumiazo ni relief tu ya mafua na si tiba ya infection.
Pili yawezekana una ugonjwa uitwao Sinusitis au sinus infection, huu ugonjwa huambatana na headache na wakati mwingine kuziba masikio kwa sababu ya kupiga sana chafya. Nina ndugu yangu ilibidi afanyiwe operation kuclear vijinyama puani.
Sinus iliyokomaa sana huzaa cancer,hivyo ndugu yetu usipuuze na kunywa painkiller tu Onana na daktari bingwa wa ENT hospitali yoyote (Muhumbili, KCMC, REGENCY, AGAKHAN) na utapata vipimo na matibabu.
Get well soon.

Mkuu Kinyau nashukuru sana kwa ushauri wako
Nitafanya kila niwezalo kuwaona madaktari
Ila namuomba MUNGU aniepushie mbali na hilo balaa la Cancer na mengineyo. MUNGU wangu ni mwaminifu naamini atasikia na sala zangu pia

thanks alot
 
samahani sana mkuu kwa kuchelewa kukujibu ,unajua sometimes tunakuwa tunafatialia posts nyingi kiasi tunajisahau.i hope sijachelewa sana na kama umeshapata ufumbuzi ni heri.
dawa ambayo niliotumia mimi ni hii hapa "RHINOCORT AQUA NASAL SPRAY" .AstraZeneca Pharmaceuticals - U.S. Home Page.

Kaka Arsene nashukuru nimepata jina la hiyo dawa, kesho nitaenda kumcheki daktari nione atai-recommend vipi kama itakwenda na mimi au la. Otherwise thanks alot comrade
 
Sipo, pole sana wakati unatafuta suluhu ya tatizo lako tumia dawa inaitwa CETIRIZINE, meza kidonge kimoja cha 10mg mara moja kwa kutwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom