Mafua yananisumbua long time | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafua yananisumbua long time

Discussion in 'JF Doctor' started by Sipo, Jul 18, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  nimekuwa na tatizo la mafua kwa muda mrefu sana toka niko form three mpaka nimemaliza chuo, nimeanza na kazi bado. Hapo kitambo niliwahi kwenda hospitali mbali mbali nikaambiwa kuwa nina aleji. Nimejaribu kuepuka hivyo vitu nilivyoambiwa kuwa ni chanzo lakini bado naona siku zinavyokwenda ndio na mafua yanakuwa juu. Sasa unajua yananinyima raha sana tena kipindi hiki cha mafua ya KTM ndio kabisa watu wananinyanyapaa.

  Naombeni dawa tafadhali hata ya kienyeji mie powa tu nitakomaa nayo
   
 2. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pole sana Sipo, unaweza kuniambia walikuambia una aleji na kitu gani? nakuuliza hivi kwani mimi pia niliwahi kupatwa na tatizo kama lako kwa takribani miako mitano hivi.na sasa nipo fit kabisa sisumbuliwi tena na mafua ya mara kwa mara.Unaweza kunipa historia yako kwa kifupi labda mafua ya likuanza kipindi gani na kabla ya hapo ulikuwa unasumbuliwa na ugonjwa gani?na weza kukupa njia nilizotumia mimi
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante sana Josm
  Walinaimbia kuwa nina aleji na vinywaji vya baridi, vumbia la ndani au nguo zilizokaa muda mrefu na kuweka harufu fulani,

  kama nilivyosema toka nikiwa form three, i think 1999 ndio nilianzwa, huwa kuna kipindi yanakata ila niwe natumia sana PIRITON, au COLDAUR, au COLDRIL na nyinginezo.

  Sasa juzi naona mshikaji wa Michael Jackson kaondoka kwa kile kinachosemekana umezaji wa dawa mara kwa mara. Ndio maana taa ya hatari imewaka kichwani nikasema nije hapa naweza pata dawa ya kudumu na kuachana na uteja,

  ukweli ni kuwa kila mara lazima nitembee na dawa z mafua mfukoni kwangu, ni sawa na kuathirika uku ndugu zangu

  Nisaidieni
   
 4. araway

  araway JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 498
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  pole bwana sipo!natumaini hapa utapata ushauri unaouhitaji!
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante sana, i hope so
   
 6. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana ,Sipo,
  mimi pia nina dogo anashida kama hiyo tushaenda hospital sana tuu lkn hamna nafuu.
  Wenye utaalamu au ufahamu kuhusiana na hili jambo tushirikianae jamani inasumbua sana.
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mafua yanatokana na sababu nyingi sana na ni vizuri kujaribu kupata ufumbuzi wa daktari kama yanakusumbua kwa mda mrefu.mimi mwenyewe niliugua sana na sasa nashukuru mungu nimepona.kuna dawa za haina nyingi kuanzia vidonge mpaka za kunyunyizia kwenye mto au za kuweka vitone puani moja kwa moja.kuna hio ya kuweka vitone puani daktari aliniandikia ndio imetatua matatizo yangu.ninge kushauri urudi tena kwa daktari ambae ni bora zaidi hili wafanye uchunguzi wa kina na ujaribu dawa zingine.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  aSANTE aRSENE
  ila naomba kama ungeweza kunisaidia hospital ambayo ulienda wewe mkuu ila nami nipate hiyo dawa. Pia ningefurahi kama hungeniandikia aina ya dawa hiyo ya matone ili nikamuone daktari kama atai-recommend kwangu
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante sana
  Mpe pole na dogo pia hapo
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani jana sijaweza kabisa kulala, mafua yaliyoandamana na chafya yalinisummbua sana please, tusaidiane dawa
   
 11. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna dada alisumbuliwa na mafua tulipokuwa kidato cha 5 mpaka cha 6. Na kabla ya hapo alisema kuwa alikuwa nayo. Alitumia dawa tofauti tofauti (sizikumbuki labda nimtafute), lakini Mafua yake yaliisha aliposhauriwa yafuatayo na Daktari mmoja.

  Moja, kila akilala alalae na nguo, hasa inayofunika sehemu ya kifua. Hata kama kuna joto, manake aliambiwa asubuhi kunakuwa na baridi ambayo yeye atahisi ni ndogo na hata jifunika shuka, lakini inamuathiri (alikuwa anaishi Dar).

  Pili, anywe maji vuguvugu, na aepukane na maji, juice (sharubati) ama vinywaji vyovyote baridi.

  Tatu, asioge maji baridi hata kama kuna joto. Muda wowote akitaka kuoga aoge na maji moto (vuguvugu).

  Nne, ajihadhari vitu vinavyotoa vumbi ama moshi (hii ilimsaidia shuleni hakupangwa kwa vitu hivyo).

  Ninavyokumbuka kwa kuwa Daktari aliyomshauri hayo hakumpa dawa yoyote, yule dada alimdharau yule Daktari. Lakini aliamua kujaribu hayo aliyoambiwa. Baada ya siku chache mafua yakaanza kuondoka, na hadi nilipoonana naye baada ya kumaliza shule alikuwa hana tena hayo Mafua.

  Nakushauri jaribu kufuata hayo mambo niliyoandika, na pia ufuate na waliokushauri wengine. Lakini muhimu ni kuwaona wataalamu wa afya. Lakini nahisi sijakumbuka yote ila kwa uchache nimekumbuka.

  Mola akupe nafuu haraka na POLE.
   
 12. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Pole Mkuu Sipo
  Mafua yanakera pia sana tena hizo chafya ndo usiseme. Mwenyewe naamka kila siku na mafua pia aleji na vitu kadhaa kama manukato makali,vumbi na spices za vyakula.
  Nilikuwa natumia sana piriton, nimetumia celestamine,nimechemsha maji na kuweka nusu ndoo na kujifungia bafuni ili kupata mvuke kwa wingi vilevile nimelowesha kitambaa kwa maji ya moto na kuweka kwenye paji la uso mpaka puani..
  Zote hizo hazijasaidia na mafua daily sikosi..Chafya ninafanya mpaka kichwa kiwe kinauma..Naishia kuwa na handkerchief kibao,yakianza nijifute tu ila sinywi dawa siku hizi kabisaa.
  Hope Tutapata mwangaza kupitia wataalam hapa, pole sana Sipo!..
   
 13. tzengo

  tzengo Member

  #13
  Jul 19, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  pole sana mkuu sipo,
  kweli ukizungumzia mafua,hiyo ni kero kubwa kwani hupunguza utulivu wa mtu kwa kiasi kikubwa.
  kutokana na maelezo yako ni kweli kuwa kuna uwezekano mkubwa sana mafua yako yanasababishwa na allergy ya vitu fulani ambavyo mara nyingi unakutana navyo hasa inawezekana kuwa vumbi na baridi ama vinywaji vya baridi,si rahisi kuwa mafua yako yanasababishwa na infection kwani kwa kawaida mafua yanayotokana na infection huwa hayadumu kwa muda muda mrefu hata bila ya dawa yoyote huweza kuondoka yenyewe.je kwako huna pets au wanyama wengine unaofuga?kama una mbwa,paka,sungura epuka kuwasogelea karibu kwani manyoya yao yanasumbua kwa wenye allergy.jitahidi pia kuwa makini zaidi na vumbi la ndani,hii inaweza kutokana na carpets,magodoro au mito unayotumia ikawa na vumbi ambalo katika hali ya kawaida si rahisi kuliona.epuka vinywaji baridi na baridi yenyewe,kunywa maji kwa wingi ila yasiwe ya baridi ni vema zaidi kama yatakuwa vuguvugu.naamini tatizo lako halihitaji sana matibabu ya dawa kwani allergy ni ngumu sana kuitibu kwa kumeza dawa bali dawa ni kuepuka allergens.kama ukiweza kuepuka allergens unakuwa na uhakika wa kupona tatizo lako kwa karibu 100%.Zaidi ya hapo nakushauri uonane na daktari kwa uchunguzi zaidi na ushauri kulingana na mazingira uliyopo.kila la kheri mkuu.
   
 14. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa maelezo mazuri na mchanganuo mahiri, kusema kweli mengi uliyosema hapa ndio yanayonisumbua kwa kiasi kikubwa. Nitafuata ushauri wako ndugu yangu
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Belinda
  Kweli mafua yanakera kwanza yanaondoa confidence
  Pili yanakuondoa kwenye discussion table kwenye mambo muhimu ya kazi, familia na shule pia

  Juzi usiku nilijaribu hiyo ya kujifudikiza maji ya moto ili nipate mvuke, at least ilinisadia kwa muda nikapata japo kausingizi. Ila chafya ndio zimekuwa zinaniumiza kuliko mafua yenyewe kuna kipindi napiga chafya mpaka nyama zote za mwili kuanzia kifuani zinauma, pia kichwa kinauma sana, unajua kupiga chafya unatumia nguvu sana

  Naomba kukuuliza kitu Belinda, umesema umeacha kutumia dawa kabisa, umewezaje? Kwani mimi nimeshindwa kabisa na nisipomeza piriton au dawa nyingine ya mafua siku hiyo sikai ofisini kwa raha kabisa, yaani in-short nimekuwa teja.

  Otherwise asante sana
   
 16. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mfumwa
  Nashukuru sana kwa maelelezo na ushauri ulionipa kwanza MUNGU akubariki sana ndugu yangu.
  Pili naomba kama una access na huyo dada tafadhali umuulize kama kuna dawa alitumia kumaliza hilo tatizo lake.
  Tatu nashukuru tena kwa haya mawazo yako na ukweli ni kwamba nime-print down ili kufanya implementation

  Be blessed
   
 17. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani nashukuru sana kwa ushauri wenu
  Shukrani za pekee mpaka sasa ziwaendee
  -Josm
  -BelindaJacob
  -Mfumwa
  -tzengo
  -Arsene Wenger

  Na wengineo wengi walionisaidia kwa mawazo yao hapa

  MUNGU AWABARIKI SANA

  NB: please bado naendelea kupokea ushauri
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  pia nasikia kuwa vitunguu saumu vinasaidia sana. hebu jaribu kila wakati wa kulala usugue nyao zako vizuri na kisha upake urojo wa vitunguu saumu kwenye nyao zote, itaweza kusaidia kupunguza au kuondoa tatizo
   
 19. I

  Ivilikinge Member

  #19
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Da jamani hata mimi nna aleji mafua toka nna 14 mpaka sahii nakimbilia 30 halafu nyingine nikioga nawashwa sana ugoko niambieni dokta mzuri niende
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kaka Mziwanda
  Huo urojo nipake kwenye nyao za miguu halafu zitasaidia kuondoa mafua? Naomba unifafanulie zaidi binamu ili nisikosee instructions
   
Loading...