Nimedhulumiwa Makazi yangu na Mtumishi wa Halmashauri ya Singida

Snadareal

Member
Jun 18, 2016
21
12
MAKALA YA WAZI KWA WATU WOTE

Kwa jina naitwa John Hassan mkazi wa kijiji cha nduu kata ya kijota tarafa ya Mtinko, mkoa wa Singida . Nimezaliwa miaka 25 iliyopita. Katika familia yetu mimi ni mtoto wa mwisho ndugu zangu wote wakike na wakiume wote wanafamilia zao. Kwa sasa siishi nao.

Nilifiwa na wazazi wangu wote ningali bado mwanafunzi. Mwaka 2005 nilifiwa na Baba yangu mzazi na mwaka 2015 mama yangu mzazi ambaye nilikuwa naishi naye myumbani ambaye ndiye alikua msaada wang mkubwa alifariki.

Baada ya msiba wa mama yangu tulikaaa kikao cha familia na ukoo nikateuliwa kuwa mrithi wa mali zote nyumbani kwani nilikuwa bado sijaweza kujitegemea hivyo niwe chini ya uangalizi wa kaka yangu Daniel Hassan kama msimamizi wa mali za marehemu. Nilifaulu kidato cha sita na kubahatika kuchaguliwa chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka huo huo 2015 ambako hivi punde nimemaaliza masomo yangu. Maisha yangu ni magumu Kwani hakuna mtu mwingine nayemtegemeaa zaid ya mimi mwenyewe ili mambo yangu yaende.

Mnamo mwaka 2017 mwishoni ,Mjomba wetu aitwaye Emmanuel Nkungu ambaye walizaliwa wawili na mama yangu Elineema Ntandu alishawishiwa na Ibrahim na kumuuzia mji na shamba ambalo ni makazi yangu niliyoachiwa na marehemu wazazi wangu. Shamba hili ndilo linalonipatia fedha kwa mahitaji ya hapa na pale ikiwemo mahitaji ya shule.

Ndani yake kuna nyumba ambayo naitumia kwa makazi yangu na vitu vyangu vyote viko mle. Pia kuna makaburi moja la baba na mengine ya ndugu zangu. Aidha, ndani ya eneo langu, kuna mizinga, na miti pia. Mjomba hatuna ukaribu naye maana hatuishi naye. Katika maisha yangu nimewahi kumuona mara nne tuu.

Ameamua kuuza eneo ambalo sio lake kwa sababu Mimi nilikuwa chuoni. Aliyenunua eneo ni Bwana. IBRAHIMU JEREMIA ARONI ambaye ni jirani yetu na anafahamu fika kuwa tumezaliwa nakukulia pale. Yeye ni mkusanya kodi na ushuru halimashauri ya wilaya ya Singida. Kaka yangu Daniel Hassan alienda kulima msimu ulipofika ili mazao yanisaidie kwa baadae akiwa hajui kuwamakazi yangu yameuzwa akakamatwa na polisi wa mjini kati kwa maagizo ya Ibrahimu Aroni kulima eneo ambalo sio lake.

Akapandikiziwa kesi ya jinai bahati mbaya mahakama ya Mwanzo ya Utemini ikamhukumu kifungo cha miezi 6 jela au faini 200,000. Tulikataa rufaaa mahakama ya Wilaya Singida lakini nayo pia imesema sisi hatuna haki Ndugu IBRAHIMU ARONI anahaki kwenye eneo ambalo familia yetu imeishi zaidi ya miaka 35.Vifo cha wazazi wangu wote ndio mateso haya.

Mahakama zimeamuru kuwa Bwana Ibrahimu ana haki katika eneo langu kwani yeye ni mnunuzi halali wakati kwa uhalisia mpaka sasa hivi hajaidhinishiwa mara baada ya familia kupinga kitendo cha Ofisi ya kijiji kwenda kumuidhinishia eneo langu kinyume na sheria. Naamini haki haikutendeka kwani hawajafika kwenye eneo lenye mgogoro wameamua vile ili kumtengenezea mazingira ndugu IBRAHIMU kwani ni mtu mwenye pesa na amedai kuwa siwezi kushindana na mtoto wa mjini.

Yeye anapesa hivo nisidhubutu kushindana naye atahakikisha ananiteketeza.
Vilevile pia nilimwendea Mkuu wa Wilaya ya Singida kipindi nipo likizo mwezi wa tatu, alinisaidia sana kwani alijitahidi mno kwa nafasi yake kwani alitoa maagizo kwa ofisi ya ya kijiji, ofisi ya kata chini ya diwani kuhakikisha kuwa ninarejeshewa eneo na makazi yangu pia na eneo lilouzwa lirudi mikononi mwangu, mjomba achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuuza eneo kinyemela lakini ofisi ya kijiji na ofisi ya kata haikutekeleza hata kidogo kwani haikunipa ushirikiano hata kidogo kwani ilidiriki kwenda kuidhinisha eneo hilo bila kuzingatia kuwa mimi nitaishi wapi.

Mara baada ya kuona mahakama na baadhi ya viongozi wa kijiji na kata kutokunipa ushirikiano pia kutokunitendea haki nilirudi chuoni kuendeleea na masomo kwani nilikuwa mwaka wa mwisho mnamo mwezi wa tano ndipo nilipoandika makala yangu ya kuomba msaada wa kisheria pia msaada wa kunisaidia mimi kupata haki yangu AMBAO ULISOMEKA HIVI

“NIMEDHULUMIWA MAKAZI YANGU NA BW. IBRAHIM ARON, MTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA SINGIDA NIKIWA CHUONI.

Kwa jina naitwa John Hassan mkazi wa kijiji cha nduu kata ya kijota tarafa ya mtinko, mkoa wa Singida . Nimezaliwa miaka 25 iliyopita. Katika familia yetu mimi ni mtoto wa mwisho ndugu zangu wote wakike na wakiume wote wanafamilia zao. Kwa sasa siishi nao. Nilifiwa na wazazi wangu wote ningali bado mwanafunzi.

Mwaka 2005 nilifiwa na Baba yang mzazi na mwaka 2015 mama yang mzazi ambaye nilikuwa naishi naye myumbani alifariki. Baada ya msiba wa mama yangu tulikaaa kikao cha familia na ukoo nikateuliwa kuwa mrithi wa mali zote nyumbani kwani nilikuwa bado sijaweza kujitegemea.

Nilifaulu kidato cha sita na kubahatika kuchaguliwa chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka huo huo 2015 ambako mpaka sasa bado nasoma. Maisha yangu ni magumu Kwan hakuna mtu mwingine nayemtegemeaa zaid ya mimi mwnyewe ili mambo yangu yaende.

Mwaka 2017 mwishoni
Mjomba wetu ambaye walizaliwa wawili na mama alishawishiwa na Ibrahim na kumuuzia mji na shamba ambalo ni makazi yangu niliyoachwa na marehemu wazazi wangu. Shamba hili ndilo linalonipatia fedha kwa mahitaji ya hapa na pale ikiwemo mahitaji ya shule.

Ndani yake kuna nyumba ambayo naitumia kwa makazi yang na vitu vyangu vyote viko mle. Pia kuna makaburi moja la baba na mengine ya ndg zangu. Aidha, ndani ya eneo lang, kuna mizinga, na miti pia.

Mjomba hatuna ukaribu naye maana hatuishi naye. Ktk maisha yangu nimewahi kumuona mara nne tuu. ameamua kuuza eneo ambalo sio lake kwa sababu Mimi nipo mbali shuleni. Aliyenunua eneo ni Bw. IBRAHIMU ARONI AMBAYE NI JIRANI YETU NA ANAFAHAMU FIKA KUWA TUMEZALIWA NAKUKULIA PALE. HUYU IBRAHIM NI MKUSANYA KODI NA USHURU HALIMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA.
huyu mtu ameapa kuniteketeza endapo nitafuatilia swala hili.

Kaka yangu alienda kulima msimu ulipofika ili mazao yanisaidie akiwa hajui kuwa limeuzwa akakamatwa na polisi wa mjini kati kwa maagizo ya Ibrahimu Aroni kuwa how eneo ambalo sio lake.

Akapandikiziwa kesi ya jinai bahati mbaya mahkama ya Mwanzo Utemini ikamhukumu kifungo cha miezi 6 jela au faini 200,000. tulikataa rufaaa mahakama ya Wilaya Singida lkn nayo pia imesema sisi hatuna haki Ndugu IBRAHIMU ARONI ANAHAKI KWANYE AMBALO FAMILIA YETU IMEISHI ZAIDI YA MIAKA 45. KIFO CHA WAZAZI WOTE NDIO MATESO HAYA.

NDUGU ZANGU NILIPO SINA MSAADA MWINGINE ZAIDI YA KUWAOMBA MSAADA WOWOTE ULE KWANI MPAKA SASA IVI SINA PAKUFIKIA mahakama imeamuru hivo. Naamini haki haikutendeka kwani hawajafika kwenye eneo lenye mgogoro wameamua vile ili kumtengenezea mazingira ndugu IBRAHIMU kwan ni mtu mwenye pesa na amedai kuwa siwez kushindana na mtoto wa mjini. Yeye anapesa hivo nisidhubutu kushindana naye.......

Kwa yeyote atakayeguswa na swala hili na mwenye uwezo wa kunisaidia ktk kupata hii haki yangu naomba msaada na Mungu ndiye awezaye kukulipa. Kwa sasa nipo njiapanda hata shule inakuwa ngumu.

NILIIAMINI MAHAKAMA KUWA INGENITENDEA HAKI NDIYO IMENIFIKISHA HAPA. LEO HII MIMI NIMEKUWA MVAMIZI KWENYE ENEO NILILOZALIWA ??? LEO HII MIMI SINA HAKI KISA WAZAZI WANGU WAMEFARIKI???

NISAIDIENI NDUGU ZANGU.

Sambaza hiyo kadri uwezavyo ifike mahali panapostahili

Mimi ni John HASSAN.

075809769”

Waraka huu
ulisambaa mtandaoni ndipo mkuu wa wilaya akauona tena na akamwagiza Afisa tarafa ya Mtinko kulifuatiliaa jambo hilo ndipo afisa tarafa aliponipigia simu nikamuelezea kisa na mkasa wa jambo hilo na akaahidi kunisaidia na nikweli alinisaidia kwani aliweza kumtafuta aliyenunuaa eneo langu na pia kuwafikisha kwa mkuu wa wilaya kwa hatua zaidi.

Nikiwa chuoni mkuu wa Wilaya kwa kipindi hicho aliwaita wote akiwemo mjomba na aliyeuziwa eneo ndugu Ibrahim Jeremiah, ndugu zangu waliokuwepo nyumbani pia na diwani wa Kata ya Kijota Ndugu Maulid Daffi aliyekiri kuwa lile ni eneo langu na pia walikuwepo watendaji wa ofisi ya mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya alisikiliza maelezo ya pande zote mbili, na mwishowe aliamua kuwa muuzaji na muuziwaji wa eneo kuwa wote ni wezi na Matapeli kwani waliuziana eneo kinyemela bila kushirikisha wenye eneo na pia bila kuidhinishiwa .

Maamuzi ya mkuu huyo Wa Wilaya aliagiza hao watu waliachie eneo mara moja lakini ndugu Ibrahim alikataa Kuliachia eneo huku akidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa eneo hilo kama tunataka kulichukua nimpe million 6.5 wakati yeye aliuziwa kwa shillingi laki nne pia aliahidi mbele ya mkuu wa Wilaya kuwa ataniteketeza kwa namna yeyote ile na kuniharibia masomo yangu. Hatimaye Mkuu wa Wilaya alipanga siku hiyo hiyo siku ya kwenda Kutembelea eneo ambayo ilikuwa ni siku ya Jumatano na akaagiza kuwa viongozi wote pia wahusika wote wawepo siku hiyo.

Kwa bahati mbaya siku hiyo alitoa udhuru kuwa asingeweza kufika kwani alienda Kutatua mgogoro mwingine hivo akatuahidi kuwa angekuja siku nyingine. Kwa bahati mbaya pia mkuu huyo wa Wilaya amestafu kuhudumu kama mkuu wa Wilaya na pia afisa tarafa wa Mtinko Naye ameshahamishwa kwa sasa .

Mpaka muda huu nimemaliza masomo yangu nimerudi nyumbani na sina msaada kwa sasa sina pakufikia kwa ajili ya makazi yangu na hata kufanya shughuli za hapa na pale nikiwa nyumbani kwani bado mgogoro huu hujatatuliwa hali inayonifanya nishindwe kuingia kwangu kulingana na vitisho na dhihaka za Ibrahim Jeremiah Aroni ni miezi 9 sasa tangu nimalize chuo Nipo tuu nahangaika na suala hili pia sina sehemu ya kufikiaa kwa makazi yangu.

Mnamo mwezi wa 8 /2018 mimi pamoja na kaka yangu tuliamuriwa na Mwenyekiti wa baraza la ardhi Wilaya kuwa tufungue shauri letu baraza la kata na tulifanya hivyo ila Diwani wa kata yetu Maulid Daffi kutokana na ukaribu na Ibarahim Jeremia aliiamuru Baraza la ardhi Kata kuwa lisisikilize shauri letu na kama ikitokea wametusikiliza atawaondoa wote katika baraza hilo.

Tuliushirikisha uongozi husika juu ya suala hilo ndipo baraza likaamuaa kutusikiliza shauri letu. Katika shauri letu tuliwalalamikia Emmanuel Nkungu na Ibrahim kwa kuuziana eneo kinyemela. Wakaomba turudi kifamilia ndipo tulipo rudi kifamilia Mjomba alikiri kuwa Aliuza eneo kimakosa hivyo yeye atarudisha gharama alizopewa na Ibrahim ila hakufanya vile ndipo tukarud tena barazan na alipoulizwa akakiri kuwa yeye yupo tayari kutoa gharama hizo ila mwishowe akagoma na hakuwa anahudhuria barazani ndipo baraza likaamua kumuweka chini ya ulinzi kwa zaidi ya mara mbili na aliporudi akagoma kutoa maelezo mbele ya baraza hivyo baraza likaendeleea na shauri kwa upande mmoja siku ya kutembelea eneo tarehe 27/12/2018 ndugu zake na Ibrahim wakamtengenezea kaka kesi ya kuwa alimpiga Ndugu yake na Ibrahim Mbele ya baraza na uongozi wa kijiji hakumchukulia hatua hila hii pia ilifanya kaka angu aje akamatwe tena kwa mara nyingine na polisi kutoka mjini na kumuweka ndani bila hatia kesi ilienda mahakamani na baraza lote pamoja na uongozi wa kijiji uliitwa kutoa ushahidi mbele ya mahakama na kukiri kuwa Huyu mtu hakupigwa hata kidogo wala ugomvi haukutokea ila ChakushangaZa Mahakama ili mhukumu kaka miezi miwili au alipe 250,000 kwan waliridhika na PF3 aliyoipeleka mlalamikaji huyo.

Tuliona tuwalipe kwan hatukuwa na kosa ili kuepuka usumbufu. Tarehe 14/1/2019 Baraza la aridhi lilitusomea hukum ambapo sisi tulipewa haki siku hiyo hiyo Diwani Maulid Daffi alilivunja baraza hilo kwa kutupatia haki na kumtaka Katibu wa baraza ampe nyaraka zote za shauri letu pia alimwamuru Emanuel Nkungu kumwandikia Mwenyekiti wa Baraza la Aridhi Wilaya ya Singida kuwa yeye hakutendewa haki hivyo akaomba haki tuliyoipewa ifutwe .

Hatukupata sababu za msingi kwann yeye Avunje baraza tulipoulizia hao wajumbe wa Baraza ni kwann baraza livunjwe wakasema kuwa sababu ni wao kusikiliza shauri letu ambalo walikwisha zuiwa na Diwani mwenyewe. Mwenyekiti wa Baraza la Aridhi Wilaya naye akatengua hukumu ama kuifuta haki yetu pasipo kutushirikisha pia ameamuru tufungue shauri hili tena katika baraza la kata ambalo tayari diwani ameweka watu wake wapya ili watupotezee haki yetu kama bado tuna uhitaji na eneo hili. kwani mwanzoni yeye alituagiza tuakafungue shauri hili Baraza la ardhi kata.

Mnamo tarehe 12/02/2019 hawa watu wakaenda kufanya uharibifu ndani ya eneo langu kwa kuweka uzio, kuchungisha miti, kukanyagisha makaburi na Mifugo yao hali iliyopelekea tuwachukulie hatua stahiki kwa dhuluma zao zote kwa kuwaripoti ofisi ya kijiji, kata na hatimaye polisi na leo hii kesi ipo mahakamani.

Kwa namna jambo hili lilivyo na kona kona nyingi na harufu ya rushwa nimeona kuwa haki yangu ishapotea tayari sina imani tena kwa maana nimeshapitia ofisi hadi ofisi, hatua hadi hatua nimepoteza pesa nyingi na haki imeyumbishwa mimi sina pa kuishi .

Vielelezo vyote ninavyo ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa, vyeti vya vifo vya wazazi wangu ambapo walifariki na kuzikwa ndani ya eneo, hilo Hati ya miradhi, barua ya ofisi ya kijiji ikinitambua kama mwenye eneo, hukumu iliyonipa haki kutoka baraza la kata ,ushahidi wa picha na videoclips kuhusu kila hatua niliyopitia na kuhusu Diwani ambaye pia hata viongozi wamekwisha kiri kuwa yeye ndio Engineer wa Mambo haya yote ya mimi kutokupata haki yangu pia niliwahi mwendea anisaidie akadai nimuwezeshe hela ili anisaidie niliposhindwa akasema yeye hayuko tayari kunisiaidia kwani yeye kama kiongozi wa wananchi ameshindwa kunitetea na kusababisha mimi kupoteZa makazi yangu


Hivyo basi naombeni tena msaada wenu ndugu zangu ikiwa ni pamoja na maombi, msaada wa kisheria na pia maoni kwani makala hii haina chembe chembe za kumchafua mtu bali kueleza ukweli pia kupata msaada wa kupata haki yangu ya kuishi kwani mimi ni yatima ukizingatia pia vitisho ninavyopewa na hawa watu kuwa nitakuja kujutia kwani wao hawapo tayari kuliachia eneo langu.

19/02/2019
JOHN HASSAN

0758097069


NAOMBENI MNISAIDIE KUSAMBAZA KADRI MTAKAVYO WEZA ILI LIFIKE MAHALI HUSIKA NAMI NIWEZE KUPATA HAKI YANGU KWANI KUPITIA ANDIKO LA AWALI NILIPATA MSAADA


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pole sana ndugu...
Dunia hii imejaa dhuluma na uonevu wa kila aina.
 
Aseee....!! Pole sana ndugu , naamini haki itatendeka

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Mkuu as long as umeweka hapa,utapata msaada..

Maana humu kuna wengi sana wakukusaidia..

Yani hii mbaya sana,watu wanatumia pesa na madaraka kudhurumu wasio na kitu
 
Kiukweli mkoa wa Singida mwenyekiti wa baraza la ardhi sio mtenda haki mie nina ndugu yangu kafanyiwa jambo kama hilo ilihali hati anayo vibali vya ujenzi anavyo kutoka dodoma huyo anayeambiwa mwenye eneo kamkuta ndugu yangu
Tayari ameshapatiwa usajili wote huo ukiangalia kwa undani ni mtu anayependa sana rushwa
Nimemshauri ndugu aende dodoma mahakama kuu
Tunaomba sana mh. Lukuvi apamulike Singida hasa huyo mwenyekiti wa baraza
 
Wananchi wengi wa Tanzania wana migogoro ya namna hii. Cha ajabu sana Mpaka Mh. Rais atamke ndio haki ipatikane sijui mamlaka nyingine huwa wanafanya nn
 
Pole sana. Jf ni jukwaa kubwa, utapata tu maaada unaohitajika. Hapa pia kuna kitu nimejifunza. Kuandika/kuacha wosia kabla ya kuondoka hapa duniani kwa wale wahusika wanaostahili, ingawa wengi tumekua na imani potofu ya kuhisi tunajichulia kifo.
 
Wee ni msomi ila unababaishwa na watu wasiokwenda shule,diwani ndio takataka gani???

Huyo uncle ungempiga viboko akiri zikae sawa.
 
Umedhulimiwa na Ndugu zako waliouza kwa shida zao acha kumchafua huyo mnunuzi we msomi
 
Umedhulimiwa na Ndugu zako waliouza kwa shida zao acha kumchafua huyo mnunuzi we msomi

Ukisoma kwa undani huyo mnunuzi ana kiburi, na aliahidi mbele ya mkuu wa wilaya kuwa atamharibia hadi katika masomo yake.
Kwa mnunuzi mwenye hekima huwa anajitoa anapogundua eneo lina mgogoro na kuomba kurudishiwa gharama zake. Lakini huyu kakaa kishiri sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwenye makosa hapo ni mjomba wako tu na si mnunuzi,pia inaonekana ndugu zako (kaka,dada) wamekutenga,nikimaanisha hii vita kuishinda ni changamoto pia;mfungulie kesi mjomba wako ingawa hawezikukulipa chochote,cha zaidi wewe ni mtoto wa kiume na una nguvu pambana unaweza kufanikiwa zaidi bila kutegemea urithi .Nadhani wanaojua sheria zaidi watakusaidia
 
Back
Top Bottom